Fans wenzangu wa hii timu mpooo au mmekimbia mafichoni. Nilishasema kuwa zile mid table team na zinazokaribia kushuka daraja zinakuja kutufundisha mpira namna wachezaji wa kulipwa wanavyotakiwa kuwa Kwa maana ya kuwa na desire, commitment, focus, discipline.

Mmeona Sasa matokeo ya kulea mifumo mibovu?, binafsi matokeo yakiwa hivi nafurahi kidogo, kwanini?, Ili basi tuone uozo wote yaani uozo wote, kwamba Kuna watu wao wanalipwa na kulipana pesa nyingi lakini wanachotoa ni sifuri kabisa, Sasa hivi United kufungwa si stori, hili mtakubaliana na Mimi. Nitaendelea kusema kuwa shida ya United ni wachezaji na nani aliyewaleta hao wachezaji?, tunarudi juu kule Kwa mgt.

Angalia garnacho kule anapoteza mipira hovyo hovyo si wa kuanza lakini una nani nje?, wa ndani ndio wana afadhali kubwa kweli kweli kuliko wa nje. Nakubaliana na kocha kuwa hii ndio United mbovu kuliko zote kabisa na nadhani tumejiandaa Kwa hili, Kwa Sasa Kama jezi yako itie kabatini kwanza maana umefanya timing mbovu ya kununua jezi yako.

Nazidi kusema kuwa tatizo letu si kocha hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…