Asalam Alaykum!
Nikiwa Shabiki wakutupwa wa Manchester United kuanzia mwaka wa 1966 hadi hii leo kwa kweli Sir Alex Ferguson anahitajia kupewa kila sifa kwa kuiwezesha team aliyoichukua wakiwemo walevi watupu kina MacGrath na wengineo hadi akaja akawapata kina Cantona na kuanza kuchukua mataji kila heko anastahili.
Hapa alipofika Ferguson kishagonga ukuta na hajui alifanyalo na inabidi Man Utd itafute replacement kwaharaka kabisa. Ukitaka kukubaliana na mie nikuanzia match ya Arsenal kuja ya Aston Villa. Huwezi ukaelewa huyu Tevez wanini kwenye team na lini anataka Nani akuwe. Alikubali kuwa na kina Gigs, Neviele, Beckehma hadi wakawa matured lakini leo kaleta watu anawaweka baoni kisha akiwapa fursa ategemee kuweza kufanya vizuri.
Ukiweka 1. Venders 2. P mtoto wa Brazil 3. Evra 4. Vidic 5. ferdinad 6. Anderson 7. Ronaldo 8. Nani 9. Berbatov 10. Barbatov 11. Rooney basi kikosi hichi kwa pale kwenye Premier labada Shetani ndio atakiweza. Huyu Park na Gigs wanini? Gigs nikucheza match baadhi tu tena second half, hawezi kucheza akenda na pace ya mchezo lakini kashikiliwa tu na dhana za kiajabu kuwa ni experience. Scholes akija ni sawa kwani bado anauwezo, kisha Gigs ni mroho wakutupwa hutaka kupiga Free Kick kwenye maeneo ya Ronaldo ni vipi? Angalia zamani kwenye maeneo ya hatari utamsikia mtangazaji Beckham Teritory kwa kuwa akenda kupiga kuna khatari leo Tritory za Ronaldo naye hujipeleka. Giggs of 1999 is no more existing, his days has gone.
Tutaendelea kuizungumza team yetu.
Thanks#
Mzee Panganyile