Manchester United (Red Devils) | Special Thread
eneo moja ambalo tunafeli ni sera ya usajili na kipaombele cha usajili.
  • kulipa paundi millioni 60 kwa YORO haukuwa uamuzi sahihi, umri wake, uzoefu wake na nafasi yake haikuwa na ulazima wa kutumika hela kubwa kiasi hicho. United hatupo tena kwenye daraja la kumwaga paundi millioni 40 kwenda juu kwa kusubiria matunda ya mbeleni. Kipaji kipo lakini hela yake haikuwa muafaka, Papa perezi si mwendawazimu
  • Kosa hilo pia tumelifanya kwa Hojlund na matokeo yake licha baada ya kutumia euro millioni 120 kwa usajili wa washambuliaji wawili kwa sasa klabu inajiandaa kuingia tena sokoni kutafuta mshambuliaji mwengine.
  • tumetumia paundi millioni 95 kwa usajili wa mabeki wawili wa kati ndani ya dirisha moja na wote RCB, Inachekesha kwa timu inayoongozwa na watu wenye uzoefu. Sijui liverpool wana mwaka wa ngapi hawajasajili beki wa kati baada ya ujio wa KONATE. Wakati huo huo amesajiliwa Mazaroui anayeweza kucheza mlinzi wa kati.
 
Bwanyenye halitaki mchezo
1000021968.jpg
 
Back
Top Bottom