Manchester United (Red Devils) | Special Thread
Spurs ni vibonde wetu hata sina wasiwasi nao
 
ok....tusubirie muda na wakati utapofika ndipo tutajua kwanini sie tupo ndani ya big 4 na wao hawamo....habari za kina lenon, mara modric mara pete crouch sie hatuzihitaji...tushazoea kelele za chura mwisho wa siku sie ngombe tunakunywa maji...kama mnabisha waulizeni wenzenu wa arsenal tuliwafanya nn
 
Kuna msimu season Spurs walitupiga 3 bila hadi half time kipindi cha pili tukawapiga 5 game ikaisha 5-3, msimu uliopita walitupiga 2-0 hadi half time kama kawaida second half tukawafunga 4-2
Huyo Lennon raha yake ni kumpiga chenga Evra but hana madhara
 
Wapenzi wa Man U inabidi tuiombee timu yetu coz Spurs wanatisha, wasije wakatutia aibu wik end hii...

Ni kweli!
Hii topic ungeipeleka kule kwenye Majadiliano ya timu ya Man U au Tottenham, usingeanzisha thread hii mpya.

Ni mtazamo tu!
 
Eti Tottenham who? Hivi nyie mmeanza kuangalia mpira lini maana naona history nayo inawapiga chenga. Spurs miaka yote vibonde tu ni sawa na Man City kwa Arsenal.
 
Man Utd kama kawaida wataibuka washindi dhidi ya Spurs.Kila msimu mpya unapoanza Man wana kawaida ya kuanza ligi kwa kusuasua.Mwaka jana msinakumbuka bwawa la maini walivyoanza kwa nguvu za soda lakini mwisho wa msimo bingwa alikuwa nani ????.

Mtajuta kuzipenda timu zinazowatia simanzi kila kukicha.
 
Man Utd kama kawaida wataibuka washindi dhidi ya Spurs.Kila msimu mpya unapoanza Man wana kawaida ya kuanza ligi kwa kusuasua.Mwaka jana msinakumbuka bwawa la maini walivyoanza kwa nguvu za soda lakini mwisho wa msimo bingwa alikuwa nani ????.

Mtajuta kuzipenda timu zinazowatia simanzi kila kukicha.
 
Haya wadau line up yetu ni kama ifuatavyo,
Foster, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, Scholes, Anderson, Giggs, Berbatov and Rooney.
Subs: Kuszczak, Owen, Carrick, Nani, Fabio Da Silva, Jonathan Evans, Valencia.
 
Mmeliona goli la Jermaine Defoe?, TOT 1 MANU 0, lilikuwa goli la tiktak.
 
...aaaaaah, MAN U msiniharibie siku jamani...

Usijali dk 90 zitadhihirisha raha yako siku ya leo au la!..hivi kweli wewe ushangilie MAN U, siamini mana msivyowapenda sijui kwanini..he he


Hawa kawaida yao kuanza kuongoza...uwa tukifika kipindi cha pili tunarudisha na kuwashindilia.

Na iwe hivyo mkuu Eqlypz mana kuanza tu wamefunga..Tuangalie itakuwaje in 90mn, ushindi wetu na imani!..
 
Back
Top Bottom