Mandela halisi aliuwawa na makaburu huyu ni feki

Mandela halisi aliuwawa na makaburu huyu ni feki

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
447
Inavyosemekana katika mitaa ya weusi waliokata tamaa pale SA, wanaamini mandela halisi alishafia jela (walimuua kwa siri) na makaburu wakatafuta mtu aliye shabihiana naye waka mtrain kwa kipindi kirefu kumwakilisha mandela halisi! wanachodai ni. ...pointi kubwa juu ya dai hili ni
  1. kuwa kunatofauti kubwa ya kifalsafa kati ya mandela aliyeingia gerezani na mandela aliyetoka gerezani.
  2. Mandela aliyetoka gerezani alifika kijijini kwao mara chache sana, ila hakuweza kupaform baadhi ya ceremonial rituals.
  3. Hakuweza kukutana kimwili na mke wake winnie ambaye angeweza kugundua tofauti za mwilini, na mazingira yalishaandaliwa yaliyopelekea kuvunjika kwa uhusiano huo!
  4. mateso ya jela za makaburu hasa kwa wapigania uhuru kama mandela na Salomon malhangu, ni vigumu kutoka jela na kuwa na afya na uwezo wakuishi na kufikia umri aliofikia 'mzee madiba'! wengi waliuwawa jela
  5. ANC ya mandela aliyetoka gerezani haikuwa na mwelekeo wa ukombozi wa weusi .............
 
Acha hiyo maneno mbovumbovu
Miaka yote leo ndiyo wanasema haya ?

Acha upandikizi wako Mkuu mleta mada.
 
Kweli kazi mnayo, kwa jinsi Dunia ilivyo haina siri mpaka leo ingekuwa ishajulikana
 
Mkuu SLAA ANAWEZA naona leo umeamua kuja na mada yenye akili, vipi hapo mbozi wazima?

Back to topic:
Nakuunga mkono kwa 100% kuwa huyu ni Mandela feki na si yule tuliyemfahamu hapo mwanzo kupitia maandishi na vitabu vya kihistoria.
 
Na waliompokea chamani na watoto wake pia ilikuwa wakutane naye kimwili ndio wamjue au wamkatae (samahani kwa wazo hili)? ????!!!!

Syenzi zao!!!!!
Hebu amsha akili kama waliweza kumtengeneza walishindwa nini juu ya culture and rituals???!!
 
Hata Nyerere alipofariki kuna waliodai ana asili ya Ethiopia. Ni kawaida kwa Afrika au mtaani kwenu haipo hiyo tabia pindi mtu anapofariki kuzushiwa?
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini habari kama hii....

Huwa kinachonisikitisha ni jinsi ambavyo Mandela na Winie walishindwa kuishi pamoja kwa raha na amani baada ya kupambana pamoja....

Mambo mengine tuyaache yalivyo kwani ukiamua kufuata maneno ya mitaani hata mzazi wako mwenyewe unaweza kumkana!!
 
...mmmh!...maneno iko mingi sana...hivi kumbe mtu unaemwona kuna uwezekano mkubwa akawa sio yule unayemtazama au kumwangalia!?...hapa inabidi kutafuta tofauti ya mbili mara mbili na mbili jumlisha na mbili,ukipata jibu itakuwia raisi kujua nini kilitangulia kati kuku na yai...
 
Back
Top Bottom