Mandonga na Dullah Mbabe Wamshukuru Rais Samia kwa Kuendelea Kusapoti Michezo Nchini

Mandonga na Dullah Mbabe Wamshukuru Rais Samia kwa Kuendelea Kusapoti Michezo Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.06.jpeg

Miaka minne kasoro ya Uongozi wa serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wetu mpendwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya michezo, sekta ambayo imebeba matumaini makubwa ya vijana waliojiajiri kupitia vipaji mbalimbali walivyonavyo.

Si tu katika michezo iliyozoeleka na wengi, kama mpira wa miguu, kikapu na pete, bali Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amegusa pia michezo ya Masumbwi (Boxing) kwa kuendelea kusapoti vijana wanaoshiriki michezo hiyo.

WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.08.jpeg

Mwishoni mwa wiki hii, tumeshuhudia Mheshimiwa Rais akitoa motisha kwa mabondia walioshiriki kwenye BOXING SAFARI iliyofanyika katika Uwanja wa Zimbihile, wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera. Motisha ya Tsh. 10,000,000/= ilikabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. Fatma Mwassa kwa niaba ya Mh. Rais Samia kwa washindi 10 waliopatikana katika mapambano 10 yaliyopigwa siku hiyo.

Washiriki wa mapambano hayo na mashabiki wa Masumbwi mkoani Kagera, kwa pamoja wanasema upendo wa Rais Samia kwao wataulipa kwa kura za kishindo 2025 ili kazi iendelee kwa nguvu kubwa zaidi.


MICHEZO NI AJIRA, MICHEZO NI AFYA🤛

WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.11 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.18.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.09.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.09.jpeg
    329.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.12.jpeg
    396 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.17.jpeg
    370 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.14.jpeg
    370.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-29 at 14.13.12.jpeg
    396 KB · Views: 2
Back
Top Bottom