Maneno 'HAPA KAZI TU' yaondolewe kwenye mali za nchi, yanatia aibu na wala hayana maana yoyote

Maneno 'HAPA KAZI TU' yaondolewe kwenye mali za nchi, yanatia aibu na wala hayana maana yoyote

Nakushauri tena mkuu kwenye nchi yenye maskini wengi kama Tanzania, wewe kama kada wa Cdm usipende kulitumia kudhihaki ,
Utaharibu picha ya chama chako ambayo kinategemewa kuja na sera za kuwatoa kwenye umaskini,
Watanzania wengi Bado wako kwenye mapambano dhidi ya umaskini
Umasikini siyo baraka , ni laana , hakuna haja ya kuuficha wala kujivunia
 
Mkishindwa kuyaondoa kistaarabu yataondolewa na wananchi
Wananchi wataondoa vp? Wakati mwengine hebu punguzeni ujinga. Wananchi walishindwa kumuondoa madarakani huyo Magufuli na ndio lingekuwa jambo la msingi,wananchi kupata katiba mpya wameshindwa halafu leo waje kuondoa hayo maneno? Huo kama sio upumbavu ni nini?
 
Wala msihangaike , ondoeni tu hayo maneno mkayaweke vibarazani kwenu
Zile ndege sio za baba yako mzazi na ndio maana yaweza kuwa hukutaka zinunuluwe ila bado zikanunuliwa, halafu ndio uje kuamuru et yale maneno yatolewe we nani? Mwambie baba yako akununulie ndege kisha ndio utaweza kuandika chochote unachotaka wewe.
 
Utashindwa kujibu kwa kuwa kingereza chako ni hadi ule konyagi ndogo. Ila naunga mkono hoja wayafute waweke "LOWASA MABADILIKO, MADILIKO LOWASA"
Hivyo ni vibwagizo. Vibwagizo siyo kitu cha kudumu, ndiyo maana haviwekwi kwenye vitu vya kudumu.

Baadhi ya vibwagizo na tawala zake:

MWALIMU NYERERE

Uhuru na kazi - kililenga kuwahimiza watu wafanye kazi. Wasije wakafikiri kuwa huru maana yake ni kuwa na uhuru wa kutofanya kazi.

Siasa ni kilimo - kililenga watu wafahamu kuwa msingi wa siasa ni uchumi, na uchumi mkuu kwa nchi yetu ni kilimo.

MKAPA

Uwazi na ukweli = kililenga kuwahimiza viongozi kuwa wakweli kwa wananchi badala ya kuwalaghai.

JAKAYA

Maisha bora kwa wote - kililenga kuwapa hamasa watu kuwa kuna uwezekano wa wananchi wote kupata maisha bora

Ari mpya, kasi mpya = kililenga kuwahamasisha watu kuwa na mori na spidi mpya katika kuyatafuta maendeleo.

MAGUFULI

Hapa kazi tu - kililenga kuwaambia watu waache blabla, au kuwaeleza watu kuwa utawala wake hautakuwa wa blabla bali vitendo.

Hivi vyote ni vibwagizo ambavyo siyo sera wala siyo sheria. Ni vitu tu vinavyolenga kuamsha ari ya wananchi kwenye utawala fulani, siyo vitu vya kudumu, na wala havitakiwi kuwekwa kwenye vitu vya kudumu.

Lakini pia siamini kama Rais Magufuli aluwaamuru waandike mabebo hayo kwenye ndege au vivuko. Kwenye utawala ule, watu walikuwa wanashindana kusifu na kujipendekeza, hao ndio walioyafanya hayo.
 
Tumeshakubaliana Hilo Pia Twiga Naye Atupishe Maana Anatuchelewesha Kwenye Mengi Mno
Nyegere Anachukua Nafasi Ya Twiga Mpaka Tanesco Nao Watoe Nembo Yao Ile Umeme Uache Kukatika
Kwa Nyegere ni SAWA kabisa! Sema tutakua na wivu na mademu zetu sana, sema Nini?! Mademu wenyewe ndo hao walesbian na vijana wetu hawataki ndoa wanageuka kuwa mchicha pori
 
Meli Kubwa kuwahi kutokea Ziwa Victoria ndo inashuka majini. HAPA KAZI TU!! Viva JPM

Mwambie sasa huyo Mbelgiji aende Mwanza kumtukana Shujaa wa Africa.

Maneno HAPA KAZI yataendelea kuwepo wakati wote. KENGE
Argue sensiblly, utaonekana mtu sensible. Present hoja yako kwa hekima. Ukizoea kupresent mawazo yako kihovyo hovyo, baadaye itakujenga, na utakuwa wa hivyo hivyo.
 
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwa wahusika wote pamoja na wenye mali ambao ni wananchi.

Kuwepo kwa maneno haya ya kijinga kwenye ndege zilizonunuliwa kwa hela za wananchi, au unaweka maneno haya kwenye meli zetu ni upuuzi usio na mfano. Haya yanafanywa na makondakta wa daladala za DSM kwa lengo la kujiliwaza kutokana na foleni za mkoa huo.

Kama tunataka kuchorachora ndege zetu au meli zetu basi tuchore maandishi ya maana, kama Timu ya Simba imeweka nembo ya 'VISIT TANZANIA', kwanini msifanye hivyo kwenye mali za Taifa badala ya kutuwekea mavitu yasiyo na maana?

Hivi ukiulizwa na wageni maana ya 'HAPA KAZI TU' utajibu nini? mbona mnatudhalilisha kirahisi namna hii? Tafadhali sana TUHESHIMIANE.
Unaona huu upumbavu wako!!??, hakuna hata mmoja anaye kuunga mkono,comment zoote zinakutukana,
 
Hebu tupe mawazo ,tuandike nn,
Tusiwe na maandishi ya ajabu ajabu. Angalia angalao hata mashirika 10 ya ndege Duniani, wameandika nini kwenye ndege zao? Ni mara chache sana unapokuwa tofauti na watu wote, wote wakawa hawapo sahihi ila wewe tu mmoja ukawa sahihi.
 
Unaona huu upumbavu wako!!??, hakuna hata mmoja anaye kuunga mkono,comment zoote zinakutukana,
Mimi sijawahi kuomba kuungwa mkono na yeyote hapa JF , ninaandika ninachokiamini kwa lengo la kufundisha , pia sijawahi kuogopa matusi wala kulogwa
 
Acha utoto Chadema ni msingi iliwafikia wanachama million 6 ambao ndio wanasajiliwa pia kupitia Chadema digital. Hata CCM ilisema Ina wanachama million 16 kwani Ina kura million 16 uchaguzi wa 2020?? Hata wenye vitambulisho vya kupiga kura ni zaidi ya million 25 ila je Kuna siku wote hao wamepiga kura??

Usichanganye mambo, mwaka 2020 kwa mujibu wa NEC wagombea ubunge wa Chadema walizoa kura million 3 combined Sasa ulidhani hizo kura zimetoka wapi?

Na 2025 zitaongezeka maana tuna Rais dhaifu asiyeweza lolote so hakuna mwenye akili timamu atampigia kura.
Wewe mbona mzito mno kuelewa? Pamoja na uchache wa wanachama mtapata kura zaidi ya milioni moja ambazo nyingi ni kura za huruma. Bahati mbaya hazitawasaidia kushinda
 
Back
Top Bottom