Maneno ya Dkt. Bashiru ni shambulizi kwa Rais Samia na yenye ajenda ya siri. Aitwe haraka na kuhojiwa na chama

Kaka ni kweli umeshindwa kufikiri in deep na kuona ni nini kinachoendelea kwa watanganyika kaka
NIMESIKIA MANENO HAYA KWENYE KIJIWE CHA KAHAWA PALE MSIMBAZI NA SHAURIMOYO!!...Iko hivi:- kama hujaenda Z'bar karibuni:-
Ukipita mitaa karibu yote ya z'bar hukosi kuona site zaidi ya 5 zimezungushiwa mabati!!...Ni hivi wazanzibar wanamwita rais wao MWINYI MABATI...(Mikopo ya serikali kuu yaani TZ)
Kuhusu afya Z'bar wanafanya kumpatia bima kila mzanzibar(sio mtanganyika)
Kipindi ukimpambania na kumpigia chapuo alimwambia PETER wewe ni primitive
....wale wachovu walilalamika sana tena wakitupa lawama bila kujali hadi kusema mnyiramba anawafukuza wenye nchi waende kule mara masoko kuungua mara machinga kafukuzwa.... niliondoka mapema kuwahi mishemishe zangu nikatafute kadi za watu!
 
Bashiru kakosea sana huo ndiyo ukweli , hara kama hakuwa akiunga mkono habari za awamu hii angekaa kimya tu ,mbona walikuwa hawataki mtu awakisoe zama za utawala wa Magufuli?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa mwana CCM huna tofauti na zezeta......akili zako unazikabidhi kwa mwenyekiti wewe kazi yako ni kusifu na kuabudu huku ukirushiwa mifupa ya vijipande vya kama paka ili uendelee kuwa msukule.........
 
Sijasoma ila najua tu umeandika pumba.
 
Hoja gani upuuzi mtupu. Rais ndio anatakiwa aitwe ahojiwe kwanini umeme umemshinda, na maji hakuna. Mnaona jambo la maana kumtetea rais aliyefaulu baada ya kutetea nchi kwenye mambo ya msingi.
Hakuna mambo ya msingi na yanayogusa maisha ya watanzania ambayo mh Rais hajayafanyia kazi kwa kutafutiwa majibu,
 
Wewe kijana unaesema unanipenda nchi yako, hebu acha taarabu halafu uje na facts ambazo zinaweza kumtetea huyo mwanamke ili asifiwe na kuunga mkono juhudi zake! Katika uongozi mbovu na duni ni huu wa huyu mwanamke hakuna kitu kafanya zaidi ya kulipa taifa hasara maji hakuna,umeme wa shida, wananchi wanalalamika bei ya bidhaa kupanda juu, ugumu wa maisha na changamoto za ajira zimekuwa maradufu, miradi inacheleweshwa kutokana na ulegevu wa serikali iliopo madarakani, amekopa pesa nyingi sana ambazo hatuoni manufaa ya pesa hizo, kila siku mnatuimbia tarabu nchi ipo ktk mikono salama naomba kuuliza ni usalama upi mnaosemea hasa kama mtu anaweza kusimama ktk jukwa na kuwaambia umma wa watanzania kuwa tutakopa mpaka pale tutakapaojiweza 'Shame on you Samia' unaonesha dhahiri kwamba hukupemdezwa na mtawala wako aliekutangulia ndio maana umepokea kijiti ukaanza kupangua yale aliyokataza, leo unaenda kulipa wagushi vyeti kupitia PSSSF kupitia kodi za wale maskini walipa kodi, umerudisha maduka ya kubadili fedha za kigeni, umeruhusu chakula kiuzwe nje ya nchi umeshindwa kupigania mafuta ambayo ndio main entity ya serikali ya Tanzania na Africa ktk kuendesha majukumu na kufanikisha ya serikali. Umeweka ruzuku ambayo bado ni mchongo wa upigaji pesa. Serikali yako imeshindwa kabisa kubana matumizi yake. Waziri wa uchumi anakazi kuzunguka kuongeza madeni halafu mnataka tuunge mkono juhudi hivi mnaongelea juhudi zipi hasa? Ewe kijana mwenye mapenzi na nchi yako haya mambo umeyaona au babaako ni kijakazi wa serikali unakula na kulala kupitia kodi zetu sisi wanyonge ilihali raisi wako kawaachia huru wafanyabiashara kama awali kwa yule mwenzie kikwete alieshindwa hata kuzuia mianya ya rushwa, shame on you Samia shame on you sisiemu.
 
I bet, ccm is creating a naturalistic figure, soon Bashiru will be denied his party, he will Join Chadema, so his turn out will defect CDM in the coming general elections, mark my words.
 
Unamsifiaje mtu anayetimiza au kukamilisha kazi aliyoiomba na analipwa mshahara.....??? Huo na wenyewe ni upungufu wa akili
Wangapi wanalipwa mishahara lakini wanashindwa kutimiza wajibu wao? Kwani akina mobuti hawakuwa wanalipwa mishahara? Mbona wakifanya ufujaji mkubwa katika mataifa yao? Kwanini mh Rais asipongezwe kwa kufanya vizuri kazi zake za kuwatumikia watanzania? Kuna kosa gani kumpongeza Rais? Kwanini tuzo zilianzishwa Duniani na maeneo ya kazi kwa watu wanaofanya kazi vizuri?
 
Unamendea teuzi bila kupepesa macho,ushawahi kulima chochote?Dr kaongea na sisi wakulima wewe unapiga umbea ili kiwa Nini?

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Kuandika kote ukaweka na namba kumbe unatafuta mwanaume rijali


Nahitaji jua Ni kioo kina ukungu umekosea au ndo hiki ulitaka andika maana Ni utumbo
 
Kwani kipindi cha mkapa na jk hawakuwahi kufanya mazuri?mbona hii tabia haikuwepo imeibuka awamu ya tano,na ni kwanini sana sana utaisikia TZ tu,ni kutafuta teuzi tu,eti asante sana kwa pesa za mama!!mbona madeni yanakuwa yetu lakini pesa akikopa mnasema yake. basi na madeni muwe mnatanganza ni yake.HUO NI UCHAWA TU NDIO UNAOWASUMBUA,
 
Unamendea teuzi bila kupepesa macho,ushawahi kulima chochote?Dr kaongea na sisi wakulima wewe unapiga umbea ili kiwa Nini?

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Sasa na nyie wakulima hamjitambui,huko mtwara ni juzi tu walikuwa wanagomea kuuza korosho kutokana na bei kuwa ndogo lakini cha ajabu nao wamemshukia bashiru kuwa asiwagombanishe na mama wao hawana matatizo kabisa na mama kwani ktk marais walioisha wajari huyu anaongoza!!Hili linakuwaje sasa?!!
 
Hupo siriasi na huelewi hata kinachoendelea hapa nchini, kwamba hujaona Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea namna ilivyosaidia kupunguza Bei ya mbolea sokoni? Kwamba kwako ulitaka wakulima wanunue kwa Bei ya mwaka Jana? Kuhusu mafuta je hukuona serikali ikitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi? Hukuona ahueni iliyopatikana kutokana na hatua hiyo? Wakulima ulitaka wauze kwa hasara mazao yao mpaka lini? Unafahamu gharama za kilimo wewe? Umewahi kushika jembe wewe? Umewahi kwenda shambani wewe? Ulitaka wauze kwa Bei ipi hasa kwa kuzingatia Bei ya pembejeo ya mwaka Jana? Kuhusu ajira kwa vijana, kwamba hukuona serikali hii ikitoa ajira kwa vijana karibu elfu 42 katika secta zote zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya? Kwanini usimpongeze mh Rais kwa kufanikisha hayo ndani ya muda mfupi wa uongozi wake?
 
Ni mwiko kumsifia bbaba au mama majukumu ya baba kutafuta pesa ya ada na kula au kumsifia mama kukopa kila leo kwa riba hali resources zipo kibao
 
Kwa hiyo unataka asipongezwe tunapoona anafanya vizuri? Unataka asipongezwe tunapoona juhudi zake za kutaka kuona watoto wa kitanzania wakipata Elimu bure Hadi kidato Cha sita? Unataka asipongezwe tunapoona ujenzi wa vyumba vya madarasa na vituo vya Afya kila Kona ya nchi hii pasipo mwananchi kubughudhiwa na michango? Unataka Tusimpongeze tunapoona mkulima akipata mbolea kwa Bei nafuu? Unataka Tusimpongeze tunapoona ajira zikitolewa kwa vijana na hivyo Kuwasha taa ya Matumaini mioyoni mwa vijana?
 
Ni mwiko kumsifia bbaba au mama majukumu ya baba kutafuta pesa ya ada na kula au kumsifia mama kukopa kila leo kwa riba hali resources zipo kibao
Wazazi wangapi wanashindwa kuyamudu majukumu kutokana na Hali za kiuchumi? Wangapi wamewagi kushindwa kuwapeleka watoto wao shule kwa kukosa fedha? Kwanini asipongezwe na kutiwa moyo anayefanikiwa?
 
Huu ndio uchawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…