Maneno yaliyoandikwa kwenye geti la kuingia Chuo Kikuu cha Cape Town, yana funzo kubwa!

UCT wanaelewa. . Tz je?
 
Tatizo kwetu hatujui cha kuchagua japo nasikia tu kupanga ni kuchagua:
i. Quality hatutaki, watu wakitaka quality education utasikia wengine wanapiga kelele si waachiwe tu wote waendelee Mara kutafutwe namna F iwe C kwa kushusha kidogo "-" katikayi ili kuunda "[" ambayo sir tutaita "C" na hapa ndo tunasimama mbele ya kamera na kusema wamefaulu vizuri wakati F ndo imekuwa C.
ii. Quantity, wale wa quantity education wanapenda mamba kubwa hali watoto wao wako nje
 
Samahani mleta uzi, unaweza kuweka picha ya hilo BANGO hapa kwenye hii thread?
 
Mie ndo maana niliamua kujielimisha mwenyewe.ningetegemea elimu ya kumezeshwa darasani na hizi sylabus chovu nisingekuwa najua ninayoyajua hivi sasa.
 
Ikiwa viongozi wanaotawala waliopata elimu hii hii inamaanisha vichwani ni sifuri, na km wao wenyewe ni sifuri watapata wapi ujuzi wa kutambua kuboresha elimu!?
aiseeeee
 
Neno kuntu
 
Shule yetu ya Kata hapa mjini imerundika watoto 3000 kwenye miundombinu ya watoto 400 sasa hivi wanasoma kwa shift, mwakani tunategemea "Zero" (isome kama kiswahili) 300. Hii ndiyo elimu bila malipo,, halafu mipumbavu inazuia shule za private zisikaririshe ng'ombe!
 
Nafikiri kwa upande wa elimu ya chuo. Tuache kutumia written examinations kama njia ya kupima uelewa na ufaulu wa wanafunzi. Tubase kwenye kupima competence, ya mwanafunzi kwa oral examinations na practicals.
 
Nafikiri kwa upande wa elimu ya chuo. Tuache kutumia written examinations kama njia ya kupima uelewa na ufaulu wa wanafunzi. Tubase kwenye kupima competence, ya mwanafunzi kwa oral examinations na practicals.
Oral examinations na practicals ndio zilikua zinanifanya nisome wakati niko chuoni,.
Oral examination ya kwanza nilifanya nikiwa std 7 wakati nafanya mtihani wa kujiunga na Seminary.Ni mfumo mzuri sana wa kutahini
 
mkuu una uhakika na hayo? wewe umesoma hesabu? kuchagua ni kubaya, mbona vyuo vikuu yapo na watu hawafaulu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…