Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Mange Kimambi au kama watu wengine wanavyomuita Dada wa Taifa ni miongoni mwa Socialites wanaolipwa vizuri kwa kazi zao za mitandao.
Kwa wachache msiomjua, Mange Kimambi ni Mwanamke mwenye asili ya Tanzania aishie Marekani na mwanaharakati anayepinga vikali ufisadi na matendo yote mabaya yanayotendwa na serikali au wanajamii wanaotumia pesa au nguvu za kimamlaka kudhurumu haki za wengine, harakati zake zimepelekea kiasi kwamba ameshapigiwa muhuli wa wanted, na anaogopa kuingia nchini Tanzania akihofia maisha yake. Ameolewa na Mzungu na kubahatika kuwa na watoto wawili wa kiume.
Ukiachilia mbali kuwa mwanaharakati, Mange Kimambi ni mfanyabiashara wa habari za udaku na umbea kupitia Instagram na App yake ya Mange Kimambi ambapo uchapisha habari mbalimbali za udaku na umbea na muda mwingine kuvujisha video za siri kupitia mitandao hiyo jambo lililopelekea kuona fursa ya kuanzisha Malipo ya mwezi yani Monthly Subscription kwa wasomaji wa maudhui yake katika majukwaa anayomiliki. Kwa hivi sasa anatumia majukwaa mawili tu, Yani Instagram na Mange Kimambi App.
Nikichukulia Instagram tu, Subscription ya Mwezi kwenye Account ya Mange Kimambi ya Instagram yenye followers Million 1.6 mpaka hivi leo, anatiza shilling 2300 kwa mtu mmoja kujiunga kusoma habari zake kwa mwezi.
Sasa tuseme kati ya wafuasi hao Million 1 na laki 6, watu 50,000 ndio wawe wanalipia hiyo 2300.... kwa hiyo kwa Mwezi anakuwa na uhakika wa Shilingi za Kitanzania Milioni 115 (115,000,000).
Basi tuseme labda watu 100,000 tu ndio wanaolipia hiyo Subscription, kwa hiyo Mange Kimambi kwa mwezi anaweza kuwa anapokea Million 230 (230,000,000)
Na ukisema watu Laki 5 wote walipie hiyo Subscription ya Mwezi, unakuta anaingiza Billion 1.15 (1,150,000,000)
Pesa ambayo hakuna mfanyakazi wa serikali mwenye mshahara huo kwa mwezi.
Na ndio maana Mange Kimambi hana njaa, la sivyo angekuwa kashaongwa pesa ili hasiiponde serikali abaki kusifia na kuunga juhudi serikali. Lakini kutokana pesa anazopata hawezi kutetereka kwa sababu anawathamini wateja wake ambao ni followers wake.
Mitandao ukiitumia vizuri ni rahisi kupata mafanikio, na mitandao ukiitumia vibaya ni rahisi kuyumba kimaisha