umenijibu kwa matusi lakini hujajibu hoja zangu, shijaa awe kama Luther martin, au yule dada wa sudan enzi za Omar bashir, sasa yeye anakaaa nairobi anakuambia wewe toka tu toka usiwe na wasiwasi jikaze mbona haji kuwa ring leader wetu, maandamano ya Arusha 2010 nilikuwepo mbele alikuwepo askofu yule marehemu wa kkkt Arusha, mbowe , dr slaaa, ndesamburo na viongozi kama 300 ili make sense , na baadae ikageuka vurugu kituo cha polisi kikatakwa kuchomwa moto ndo watu 5 wakauawa , hawa wa sasahivi kwa nini wao wakae mbali? tujiongezeni na sisi tusiwe mazwazwa walionogewa togwa,
Kuna malalamiko mengi sana ya kutekwa bora hata tungeandamana kumdai Polepole wetu na Mdude, kwangu mimi tena akina Soka na wenzake hao nitajitokeza kuongezea nguvu , mdude kuna kauli alishawahi kuzitoa niliandika humu humu kuwa tuna kupinga , kukemea lakini kuna lugha za hekima kutumika,
Mwabukusi alivyonzisha kupinga kuuzwa bandari nilitoka na kugha yake ni kali lakini ya staha , Ya mdude mimi ningekuwa Amiri jeshi ningemweka ndani miaka 30 , ili athibitishe kuwa yeye huwa anawanyoaga marais kama aliyetangulia