Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Unalinganisha serikali na Mange au Maria? Serikali yenye majeshi, tanks, ndege, bunduki na mapesa ya kumwaga!

Mange na Maria ni victims wa systematic oppression, huwezi kuanza kuleta arguments kua watu ambao hawana resources kama hawa ati washindane na serikali au na hiyo nguvu, They are Inspirers, they take the lead to inspire the movement with their meager resources, including the internet and their tactics.
 
Hizo ni agenda za chadema na haya maandamano sio ya chadema. Wananchi ndio hawataki kutoka, kuishinikiza serikali kupingq uovu wa kuteka na kuuwa raia. Kumbuka haya sio maandamano ya chadema, so mambo ya reforms hayapo.

Wananchi wanachanganywa huku na huku.
Wanachanganywa na waandaaji wa maandamano.
Wanachanganywa na serikali.
Yaani wamevurugwa.

Fikiria maandamano yamepangwa vizuri. Yalianza ni NO REFORMS NO ELECTION hiyo ni kauli mbiu ya CHADEMA.
Watu waliipokea vizuri bila kujali vyama vyao.

Baadaye agenda ya pili ikawa kupinga na kuzuia utekaji uliotokea na unaoendelea kutokea. Watu wakakubali.

Baadaye, kuitoa serikali na kuifuta CCM.
Hapo mambo yakaanza kuwa mvurugano.

Baadaye wengine wanachoma vituo na kuwalazimisha wasiotaka kuandamana.
Unaona!


Lakini pia ujue, kama wewe ulivyoipa mahakama ultimatum na haikuwa chochote, inawezekana mwingine nae akafanya kwa strategy yake na isifanikiwe.
Upo sahihi
 
Nguvu inayotumika kuzima maandamano hayo ni kubwa mno, propaganda ni nyingi, wanatumika mpaka viongozi wa dini na wa kijadi kuzima maandamano yasiyojulikana kama yapo kweli huko ni kujilisha upepo uvumao. Ujumbe wa maandamano umefika na walengwa wakaingizwa chaka kuyatangaza maandamano kwenye mikutano yao ya kampeni. Ni ushindi mkubwa kwa waliopanga mbinu hiyo kufikisha ujumbe kwa wananchi, hata yasipofanyika physically lengo limetimia ujumbe umefika
 
kwanye hi ishu hata wasomi mbele ya asali wanapga pambio tu.kuna mchambuz mmoja pale facebook anaitwa lugete gulu measter anahmza amani wafuatiliaj wake hawa-like wala kukoment maandiko yake
 
Unalinganisha serikali na Mange au Maria? Serikali yenye majeshi, tanks, ndege, bunduki na mapesa ya kumwaga!

Serikali kwako sio kikundi cha watu?


Mkuu so mtu akiwa sio serikali huruhusiwi kumkosoa?
Hauna haki ya kumkosoa?
 
The core point is, maandamano hayajaandaliwa na chama chochote cha upinzani, in this case CDM. Maria na Mange naamini wanafanya kwa nafasi yao kuhamasisha, na sisi tufanye wajibu wetu kwa sababu hii nchi ni yetu sote, sidhani kama yupo mzalendo anayefurahia kutekana na kuuwana kisa mitizamo na itikadi tofauti.

Pamoja na hayo, tayari ujumbe umefika juu, wanajua wananchi wana hasira na haya yanayoendelea, hii ndio dhima halisi ya maandamano, kuiambia serikali kuwa hatufurahishwi na namna wanavyotawala, rushwa, ufisadi, tofauti kati ya bwenyenye na masikini inazidi kuwa kubwa, kuteka na kuuwa, kudai haki za msingi kama mabadiiko ya katiba, kupunguza madaraka ya raisi kuwa mungu mtu.
 
kwanye hi ishu hata wasomi mbele ya asali wanapga pambio tu.kuna mchambuz mmoja pale facebook anaitwa lugete gulu measter anahmza amani wafuatiliaj wake hawa-like wala kukoment maandiko yake

Amani ni zao la haki.

Hata hivyo Haki ni ngumu sana. Kwani haki inaendana na kukubali ukweli na kuwapa wengine haki zao hata kama wewe huzipendi
 

Mkuu hivi mtu akudhulumu hela yako. Wewe utataka arudishe pesa yako au umfikishie ujumbe kuwa yeye ni mdhulumaji?

Mtu anapokudhulumu tangu siku ya kwanza anajua yeye ni mdhulumati. Huwezi ukampa ujumbe zaidi ya kumwambia na kumshinikiza akupe pesa yako.
Bila pesa yako kurudisha hakuna la maana ulilofanya
 
Anadhani hatumjui. Bora umempa makavu

Wanatumwa kutekenya humu ili wajue Viongozi wa maandamano kwa hapa Tanzania ni kina nani ili wawakamate na kuwaua.

Kinachowachanganya hawa washenzi ni kwamba maandamano ya sasa hayana kiongozi wala nini. Ni watanzania wote wanasema tutaandamana na namna ya kuandamana tunajua.


Ni mwendo wa Nepal ndo mana wanachanganyikiwa.
 
Uwe muda wakuwaangalia hao watu au post zao unaupata wapi? Jikite kwenye kulitafutia ufumbuzi masuala ya changamoto katika jamii yako.
 
kama unaona ana nguvu kubwa itabidi umpe ujumbe wa kumtishia atishike. Kitisho kina mshindo mtibeli.
 
Tusaidie wewe sasa ili tusonge mbele, maana naona umeandika uzi huu nao wa kiuchonganishi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…