Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Wewe ndiyo Mropokaji mkuu na mnafiki, unataka uonekane upo sawa kila sehemu, you have to choose your side, praising dictators or against these oppressors. Wewe unataka uwe kote.

Nyie ndiyo wasaliti, hili bandiko lako umetumwa uwakatishe tamaa watia nia wa maandamano.

Wewe ni among hao wasaliti

Full stop
Usijidanganye, hakuna maandamano tarehe 29/10. Hakuna Watanzania wa kuingia barabarani, wapo wa mtandao tu
 
Wewe ndiyo Mropokaji mkuu na mnafiki, unataka uonekane upo sawa kila sehemu, you have to choose your side, praising dictators or against these oppressors. Wewe unataka uwe kote.

Nyie ndiyo wasaliti, hili bandiko lako umetumwa uwakatishe tamaa watia nia wa maandamano.

Wewe ni among hao wasaliti

Full stop
Huyu kijana kama popo. Sifa za ndege zimo sifa za unyama zipo.
 
Wabongo kwa kukosoa hatujambo, wenzako wanatumia majina yao na wanajulikana we anonymous hapa JF unajifanya fundi wa kurekebisha, kupika na kupakua, ingia tu jikoni mkuu tuone umartin luther king wako!

Kuimba kupokezana ujue...
Ndo jambo nawaambia watu kila siku kama unaona wenzako hawafai ingia mzigoni

Huyu jamaa huwa simuelewi
  • Mara yeye sio mbuzi wa kafara
  • Mara watanzania sio watu wa kuwasaidia
  • Mara anawalaumu wakina mange
  • Mara anapenda haki ila hataki kuipigania

Ni mtu anayetafuta attention kwa nguvu zote na mbaya zaidi ni ndumi la kuwili yaani hana consistency kabisa

Unaona wanaharakati hawawezi kuwa wewe mwanaharakati
Unakaa nyuma ya keyboard unaandika ujinga ujinga mambo sio marahisi hata kidogo
 
MANGE KIMAMBI NA MARIA SARUNGI WAMEHUSIKA KUHUJUMU MAANDAMANO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kukosa Uongozi wa Kitaalamu na Kimaadili

Watu wenye tabia ya kuropoka au kutumia lugha ya matusi mtaani na mitandaoni mara nyingi hukosa uaminifu wa kijamii.
Wafuasi wanaposhuhudia matusi, kejeli, au hasira zisizodhibitiwa, hamasa hubadilika kuwa utani au hofu.
Kwa mfano:

Mange Kimambi amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya watu tofauti, matusi ya nguoni hii imewafanya baadhi ya wafuasi na watu kumwona kama msemaji mwenye hasira na asiye na maadili badala ya kiongozi wa mabadiliko.

Uongozi wa maandamano unahitaji hekima, nidhamu, na heshima ya hoja; si kelele za hasira na matusi.

Kiongozi ambaye anaendana na culture ya jamii husika. Kutumia matusi mitandaoni na kutukana watu bila kujali ni mkubwa au mdogo inapunguza ushawishi wa mtu kwenye mambo ya maana.

2. Kuitisha Maandamano kwa Muda Mrefu (Zaidi ya Miezi Miwili)

Haya ni makosa ya kimkakati. Hili nilieleza kwenye post za nyuma.
Maandamano ni kama moto kwenye nyasi au mabua. ukichelewesha kuwasha, moto unazima kabla hujawasha kiberiti.
Watu hupoteza:
hamasa, imani, na kipaumbele (kwani maisha yao ya kila siku yanahitaji kuendelea). Na vipaombele vinabadilika. Zaidi ya yote unampa adui (ambaye hapa ni serikali) kujipanga namna ya kuyadhibiti.

3. Kukosa Muunganiko na Viongozi wa Ndani (Ground Movement)

Maandamano yenye mafanikio huhitaji muungano wa ndani: vyama, viongozi wa kijamii, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali n.k. Viongozi walioko nje ya nchi, na wanaharakati kama Mange, hukosa:
a) kugusa uhalisia wa hofu za wananchi.
Ukiwa nje ya nchi ukawa kiongozi wa maandamano hasa kwenye nchi kama Tanzania kisaikolojia utaonekana wewe sio mmoja wao. Ila unawasakizia wenzako.
na kuwajibika moja kwa moja iwapo vurugu au hatari ikitokea.
Matokeo yake wananchi wa ndani ya nchi hawaoni uhalisia wa uongozi huo, bali wanaona mtu aliyekimbia nchi anawaambia wapambane yeye akiwa salama.

4. Kuchonganisha Taasisi za Ulinzi (Jeshi na Polisi)

Uongozi wa maandamano unahitaji mkakati wa kisaikolojia na diplomasia. Kusema maneno yanayochonganisha jeshi, polisi, au taasisi za dola ni sawa na:

a) kuamsha tahadhari za usalama,
Hapa ni sawa na kushawishi jeshi liasi na lipindue serikali kwa kudhibiti Polisi. Hivyo serikali lazima ichukue tahadhari kubwa kukabiliana na uchonganishi huo.

b) kupunguza uhalali wa maandamano, Kupindua serikali ikiwa ni sehemu ya agenda za kuandamana kabla hata ya maandamano automatically yanapoteza uhalali.

Hata kama kungekuwa na mpango wa kuipindua serikali haikupaswa usemwe waziwazi hivi. Ingepaswa ifanyike wakati maandamano yanafanyika na yamekolea.
Kutaka kupindua serikali ni kosa la uhaini.

c) Kutoa nafasi ya serikali kutumia nguvu kwa uhalali wa kisheria.
Hivyo, badala ya maandamano kuwa sauti ya umma, yanaonekana kama uchochezi wa kuvuruga amani.

5. Kufeli kwa MANGE zaidi ya mara mbili katika kuhamasisha maandamano. Kwenye siasa na utawala kuna msemo usemao Once a loser, Always a Loser.
Ukikubali kushindwa mara moja kwenye siasa upo kwenye nafasi ya kushindwa daima. Hiyo ni kanuni. Ndio maana kwenye siasa ukiingia lazima uwe na hesabu kali hasa kwenye pigano au pambano la kwanza kwa sababu hilo ndio limebeba msingi wako. Unaweza mtazama Raila Odinga, Edward Lowasa na wengineo.

Mange kimambi tayari anarekodi ya kushindwa kuhamasisha maandamano zaidi ya mara mbili.
Hakupaswa kwenye maandamano haya awe kinara. Yeye angetakiwa atokee pembeni.

Kuongozwa na kiongozi aliyeshindwa kwenye siasa lazima ushindwe tuu. Labda muujiza utokee lakini siasa hazitegemei mara nyingi miujiza.

6. Kukosa Mkakati wa Baada ya Maandamano.

Wengi hushindwa kujibu swali rahisi: “Baada ya maandamano, tunataka nini hasa, na tutafikaje huko?”

Mara nyingi viongozi na wanaharakati wengi wenye kelele zaidi mtandaoni hawana mpango wa kisera, mikakati, bali huongozwa na mihemko na matumaini hewa kwa kujidanganya.

Hivyo, hata kama watu wangetoka barabarani, hakuna hatua za kimfumo za kufuatilia matokeo na kutekeleza mpango wenye tija ili kulinda maslahi na haki za watu wote.

Embu fikiria maandamano yamefanikiwa. Unafikiri nini kitatokea? Ngoja nikudokeze kwa sehemu nini kitatokea
a) Mauaji na visasi kwa viongozi wa serikali.
b) Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwani viongozi nao watakuwa wanajitetea kwa kutumia pesa zao na ikiwezekana kukimbia nchi.
c) uhalifu wa kuiba kwenye mabenki, kuchoma mali za matajiri maarufu waliokuwa wanasapoti mfumo.
d) Wageni na watu jamii ya wahindu na waarabu na machotara watakuwa kwenye wakati mgumu sana. Kwani baadhi ya waandamanaji wana mtazamo kuwa wao ndio wanaiba mali za hii nchi.

e) Kutokuwa na political stability hasa kujua nani anashika nchi kwa muda. Kama ni jeshi nani atashika nafasi hiyo ukizingatia mpaka sasa jeshi lipo upande wa serikali

6. Propaganda zenye kuleta machafuko kati ya Raia na wanajeshi. Kuna propaganda mbili zimetolewa kuhusu majeshi.
a) Majeshi ya Uganda yameingia Tanzania ili kuwapiga watanzania.
b) Majeshi ya Zanzibar yapo bara ili kuwapiga Watanzania.

Propaganda hizo lengo lake ni kuwapiganidha wananchi na wanajeshi. Kwamba wananchi wa Tanzania bara siku ya maandamano ikitokea wamepigwa na polisi au wanajeshi wasishangae kwani hao askari sio watanzania wenzao.

Hivyo wapambane kufa kupona kwani wanatetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya nchi nyingine.

Propaganda hii ingepaswa itolewe siku moja kabla ya maandamano ili kuchochea chuki na hasira ili Lengo la mange kimambi lifikiwe. Lakini halitafikiwa kwa sababu limetolewa wakati ambao sio sahihi ambapo serikali inaweza kuipotosha taarifa hiyo.

Lakini pia kusema kuna wanajeshi kutoka Uganda wamekuja Tanzania ni kulifanya jeshi la nchi liwe macho na kufuatilia kama ni kweli. Kama sio kweli Jeshi hata kama lingekuwa na mpango wa kuunga mkono maandamano mpango huo utafeli.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia Sabato Njema.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es Salaam
Huu ulikuwa uchambuzi uchwara, na lengo lako lilikuwa ni kuwakatisha tamaa wananchi ili waendelee kuburuzwa na ccm.
 
Huu ulikuwa uchambuzi uchwara, na lengo lako lilikuwa ni kuwakatisha tamaa wananchi ili waendelee kuburuzwa na ccm.

Mkuu maandamano yamehujumiwa.
Hilo andiko litabaki hapohapo kwenye ukweli.

Maandamano yalihusisha uhalifu mkubwa hata kabla ya makabiliano ya risasi kuanza.
Mpaka saa tano JW lilikuwa linahakikisha wananchi hawapigwi lakini baadhi ya wahusika wa maandamano walikuwa na interest na goals zingine ambazo zilikuwa ni uhalifu. Hapo yakatokea makundi mawili ndani ya waliokuwa kwenye maandamano. Wanaotaka maandamano ya amani na wanaotaka vurugu. Hapo ndio kila kitu kiliharibika.

Kufikia saa sita mambo yalishaharibika.

Tuongee bila mihemko;

Waandamanaji wanahoja zifuatazo;
1. Tume huru ya uchaguzi
2. Katiba mpya
3. Kumtoa Samia (kwenda Ikulu)
4. Kudai waliotekwa.
Hizo ndio hoja zilizokuwa zinaimbwa.

Sasa hoja hizo zinahusiana na nini na kuchoma vituo vya mafuta vya watu.
Kuvamia biashara za watu, maduka, bar n.k.
Kuchoma vituo vya mwendokasi na uharibifu mwingine.
Kuwakata vidole waliopiga Kura.

Utasema walikuwa na hasira au walionewa sana.
Sasa tofauti yao ni ipi na hao wanaoteka na kuua watu?
 
Hakuna maandamano ya kupinga serekali yasiyo na uharibifu. Usifananishe maandamano ya ekaristi takatifu na ya kupinga serekali. Uzi wako ilikuwa ni wa kukatisha watu tamaa. Punguza mabandiko mengi maana ww sio sehemu ya mabadiliko. Subiri mabadiliko yaletwe na wenye uthubutu uishie kuleta riwaya zako hapa za kung'ata na kupuliza.
 
So nawe ni wale wanaozuia wengine wasiotoe maoni au mnaopangia wengine namna ya kutoa maoni yao?

Uharibifu unapaswa uwe mdogo lakini sio kwa kiwango kilichotokea. Uharibifu labda wa kuchoma matairi barabarani haidhuru.

Unajua mpaka Kenya wenyewe na mataifa mengine yameshangazwa.
Huko South Afrika kwenyewe kwenye hekaheka hawakufikia kiwango chetu
 
Narudia tena, punguza kiherere, maana hata watu wakitekwa huna msaada zaidi ya kuweka riwaya zisizo na mashiko. Tumeshaumizwa vya kutosha, tunataka hiyo dunia ijue tulizibwa muda mrefu bila wao kusaidia lolote.
 
Back
Top Bottom