Mange Kimambi na Maria Sarungi wamehusika kuhujumu maandamano

Usijidanganye, hakuna maandamano tarehe 29/10. Hakuna Watanzania wa kuingia barabarani, wapo wa mtandao tu
 
Huyu kijana kama popo. Sifa za ndege zimo sifa za unyama zipo.
 
Hakuna kilicho hujumiwa hapo. Andamo lipo pale pale
 
Wabongo kwa kukosoa hatujambo, wenzako wanatumia majina yao na wanajulikana we anonymous hapa JF unajifanya fundi wa kurekebisha, kupika na kupakua, ingia tu jikoni mkuu tuone umartin luther king wako!

Kuimba kupokezana ujue...
Ndo jambo nawaambia watu kila siku kama unaona wenzako hawafai ingia mzigoni

Huyu jamaa huwa simuelewi
  • Mara yeye sio mbuzi wa kafara
  • Mara watanzania sio watu wa kuwasaidia
  • Mara anawalaumu wakina mange
  • Mara anapenda haki ila hataki kuipigania

Ni mtu anayetafuta attention kwa nguvu zote na mbaya zaidi ni ndumi la kuwili yaani hana consistency kabisa

Unaona wanaharakati hawawezi kuwa wewe mwanaharakati
Unakaa nyuma ya keyboard unaandika ujinga ujinga mambo sio marahisi hata kidogo
 
Huu ulikuwa uchambuzi uchwara, na lengo lako lilikuwa ni kuwakatisha tamaa wananchi ili waendelee kuburuzwa na ccm.
 
Huu ulikuwa uchambuzi uchwara, na lengo lako lilikuwa ni kuwakatisha tamaa wananchi ili waendelee kuburuzwa na ccm.

Mkuu maandamano yamehujumiwa.
Hilo andiko litabaki hapohapo kwenye ukweli.

Maandamano yalihusisha uhalifu mkubwa hata kabla ya makabiliano ya risasi kuanza.
Mpaka saa tano JW lilikuwa linahakikisha wananchi hawapigwi lakini baadhi ya wahusika wa maandamano walikuwa na interest na goals zingine ambazo zilikuwa ni uhalifu. Hapo yakatokea makundi mawili ndani ya waliokuwa kwenye maandamano. Wanaotaka maandamano ya amani na wanaotaka vurugu. Hapo ndio kila kitu kiliharibika.

Kufikia saa sita mambo yalishaharibika.

Tuongee bila mihemko;

Waandamanaji wanahoja zifuatazo;
1. Tume huru ya uchaguzi
2. Katiba mpya
3. Kumtoa Samia (kwenda Ikulu)
4. Kudai waliotekwa.
Hizo ndio hoja zilizokuwa zinaimbwa.

Sasa hoja hizo zinahusiana na nini na kuchoma vituo vya mafuta vya watu.
Kuvamia biashara za watu, maduka, bar n.k.
Kuchoma vituo vya mwendokasi na uharibifu mwingine.
Kuwakata vidole waliopiga Kura.

Utasema walikuwa na hasira au walionewa sana.
Sasa tofauti yao ni ipi na hao wanaoteka na kuua watu?
 
Hakuna maandamano ya kupinga serekali yasiyo na uharibifu. Usifananishe maandamano ya ekaristi takatifu na ya kupinga serekali. Uzi wako ilikuwa ni wa kukatisha watu tamaa. Punguza mabandiko mengi maana ww sio sehemu ya mabadiliko. Subiri mabadiliko yaletwe na wenye uthubutu uishie kuleta riwaya zako hapa za kung'ata na kupuliza.
 

So nawe ni wale wanaozuia wengine wasiotoe maoni au mnaopangia wengine namna ya kutoa maoni yao?

Uharibifu unapaswa uwe mdogo lakini sio kwa kiwango kilichotokea. Uharibifu labda wa kuchoma matairi barabarani haidhuru.

Unajua mpaka Kenya wenyewe na mataifa mengine yameshangazwa.
Huko South Afrika kwenyewe kwenye hekaheka hawakufikia kiwango chetu
 
Narudia tena, punguza kiherere, maana hata watu wakitekwa huna msaada zaidi ya kuweka riwaya zisizo na mashiko. Tumeshaumizwa vya kutosha, tunataka hiyo dunia ijue tulizibwa muda mrefu bila wao kusaidia lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…