Mwanaharakati maarufu katika mitandao ya kijamii aishiye Marekani, Mange Kimambi na nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Isihaka Nassoro maarufu Aslay, wamefunguliwa kesi ya madai kortini, wakidaiwa fidia ya Sh5 bilioni.
Katika hati ya madai, Mange anatajwa kuwa mkazi wa Los Angeles, California nchini Marekani na Mbezi Beach, mkoani Dar es Salaam. Wito wa kuitwa kwake kortini unaweza pia kutangazwa kupitia vyombo vya habari.
Kesi hiyo ya madai namba 44359 ya mwaka 2025 iliyotajwa kwa mara ya kwanza Julai 15, 2025 mbele ya Jaji Awamu Mbagwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imefunguliwa na DJ maarufu nchini Tanzania, Hancy Mushy.
Katika hati ya madai, walalamikaji wanadai Februari 13, 2024, Mange akiwa na nia ovu alishapicha taarifa kupitia akaunti yake ya Instagram na Mange Kimambi App, ambazo si sahihi na kuwavunjia heshima na utu wao
Wanadai katika chapisho hilo la kashfa, Mange alidai DJ Mushy alikuwa akijihusisha na mapenzi kinyume cha maumbile na kuambatanisha sauti (audio clip), huku akifahamu taarifa hiyo ilikuwa ya uongo
Mdai wa pili, ambaye ni mwanamke anayejiheshimu anadai kuanzia mwaka 2020 alikuwa na mahusiano na mdaiwa wa pili (Aslay), lakini kati ya Aprili 11 na 12, 2024 alikumbana na jambo lililochafua heshima na utu wake
Anadai Mange akishirikiana na mdaiwa wa pili, kwa makusudi na bila uhalali wa kisheria alichapisha kipande cha video kilichorekodiwa kikimuhusisha mdaiwa pili kupitia mtandao wa kijamii wa mdaiwa wa kwanza wa Mange Kimambi App
Chanzo: Mwananchi_official