Ms.Lincoln
Nimponde Mange kisa nini?Sio mara zote hua namkubali Mange, kuna wakati ananikera na hua nasema wazi, ila akifanya poa hua nasema pia.Sina haja ya kumchukia mtu kwa kila jambo, huo ni UNAFKI.Kila mwanadamu ana mema na mabaya yake.
Pia haya maisha kila mtu na lifestyle yake,wao walijichagulia maisha hayo, yakawakuta yaliyowakuta, sisi inatuhusu nini? Wenyewe wamevuna waliyoyapanda.
Hata hivyo Mange hajafanya vibaya kuwaanika maadui zake.Nilichopenda ni jinsi alivyoweka wazi kua wapo ambao yupo tayari kupatana nao na ambao hayupo tayari.
Ni nani asiyekua na maadui? Hata humu JF japo tunatumia fake id's tu lakini sidhani kama kuna ambaye hana adui yake japo tunatofautiana idadi.Hata mimi
nifah nina maadui chungu nzima wengine nawajua wengine siwajui hua nasikia wanasema huko pm's kua hawanipendi.
Sasa hapa tu natumia fake id's na bado watu wananichukia kisa misimamo yangu na vile ninavyojielezea, katika maisha ya kawaida hali ikoje?
Hao ni wanaonichukia, wapo ambao tuliwahi kukwaruzana sehemu fulani hadi sasa hatuquote each other.
Vipi huko nje ya JF katika maisha ya kawaida?
Kugombana ni jambo la kawaida tu.Hata huyo Mange siwezi kumlaumu kwa kua na idadi ile ya watu maana hakupenda kuishi kinafki na watu ili tu aonekane mtu mwema.Ndio maana kasema hata yeye alikua na mapungufu yake.
Pia kuongea mambo yaliyokua moyoni ni vyema kwani vinyongo vinaua! Ni wangapi wanakufa kwa kujinyonga/pressure kisa msongo wa mawazo?
Hivyo yeye kutoa yake ya rohoni sio mbaya hata kidogo.
HATA SISI TUNA MAADUI, HAKUNA ALIYE MWEMA KWA WATU WOTE.