SEHEMU YA TATU
Kama nilivyo ahidi hapo awali, Sehemu ya
TATU ya mjadala wangu inahusu aina kuu mbili za rushwa Tanzania – ya kwanza ikiwa ni Rushwa inayo tokana na
Rogue Individuals ndani ya Jamii, na aina ya pili ikiwa ni Rushwa ya KIMFUMO; Rushwa ya Kimfumo ndio tatizo kubwa zaidi kwa maana ya kwamba ndio inayozaa UFISADI; Na rushwa ya kimfumo kwa kiasi kikubwa sana, inakubalika Tanzania, even if not formally, lakini hii haijalishi kwani nchi yetu inaendeshwa zaidi na informal institutions kuliko formal institutions; tutaona hili baadae;
Tukianza na aina ya kwanza ya Rushwa i.e. inayotokana na Rogue individuals, Rushwa ya aina hii inatokana na hali ya watu/mtu mmoja mmoja kuamua kutumia ofisi ya UMMA kujilimbikizia mali; Watu hawa huwa ni watumishi wa umma (sio official members of CCM, Chadema n.k, kwa mujibu wa sheriaza ajira) na hufanya kazi kama
bureaucrats na
technocrats katika
bureaucracy system ya Tanzania; Such ‘State Officials' watatarajiwa na umma, kufanya shughuli zao kwa mujibu wa
rules, procedures, laws and the constitution;
On the one hand, a ‘state' is FIRM/IMARA pale watumishi wake wa umma wanapo ‘act' kwa mujibu wa rules, procedures and the constitution, hence provide a measure of certainty kwa umma as to what can be expected; Rushwa katika muktadha huu maana yake kuna violation of bureaucratic procedures, organizational norms, laws and larger societal expectations for the appropriate behavior of its public officials; On the other hand, a state is SOFT/DHAIFU watumishi wanapokiuka masuala haya, na hali hii kwa kiasi kikubwa sana inachangia Utawala wa sasa wa nchi kuonekana upo DHAIFU;
Aina ya Pili ya Rushwa has less to do with ROGUE INDIVIDUALS na badala yake, ni suala la MFUMO, whereby rushwa is embedded in society; Katika hili, rushwa
is institutionalized and becomes the NORM rather than the EXCEPTION;
Kama tulivyokwisha jadili awali, Nyerere alijaribu sana
to build and consolidate Tanganyika as a ‘STATE' kwa kuendeleza a ‘PUBLIC REALM' aliyorithi kutoka kwa mkoloni, yenye kutumia CIVIC INSTITUTIONS kukidhi mahitaji ya wananchi ‘COLLECTIVELY' (not as COMMUNITIES); Na ndio maana in the process, akafuta mfumo wa Kichifu n.k; Pamoja na jitihada zote hizi, Nyerere hakufanikiwa sana kwani katika Tanzania ya leo, KITAASISI, bado nguvu ya nchi ipo kwenye COMMUNITIES and their Local Institutions, sio kwenye CIVIC Institutions; Ushahidi wa hili upo kwenye udini na ukabila unaoendelea chini kwa chini, ambao pia unachochewa na viongozi fulani fulani; Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their
respect,
prestige and
social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Hii inaendana na mjadala wangu wa awali kuhusu Tanzania
as a Problematic State;
Viongozi husika ulazimika kuwa LOYAL zaidi to their communities kwani
ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Viongozi hawa kwa kawaida '
talk' about Civil Society, Civil Rights lakini when it comes to their '
walk', huwa zaidi upande local communities and relevant institutions in such communities; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE and its civic institutions, ni kawaida yao Kutumia The STATE as a PREY and milk it feed their communities kama mawaziri n.k, na hili litaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu;
Kabla ya kuingia kwenye sehemu ya NNE ya mjadala huu, ni muhimu nikasema kwamba katika aina mbili za rushwa tulizo jadili, the Common Denominator ni "
ULIMBIKIZAJI BINAFSI WA MALI";
SEHEMU YA NNE
Katika sehemu ya nne, nitajadili kwa undani zaidi kwanini nasema Ufisadi Tanzania unakubalika; nitatumia framework ya ECONOMY OF AFFECTION/Uchumi wa Mahaba katika analysis yangu; Tutajadili hili kwa undani baadae kidogo lakini kiuchumi, huu ndio mfumo mkubwa na ulio rasmi Tanzania kuliko UCHUMI Unaofuata RATIONAL BEHAVIOUR AND CHOICE; Pia katika muktadha huu, nitajadili masuala ya Social and Economic Exchanges/Mfumo wa ubadilishanaji Kiuchumi na Kijamii nchini, ambao umetawaliwa zaidi na informal processes and institutions, na jinsi gani masuala haya kwa pamoja yanachochea na ku ‘entertain' rushwa na ufisadi Tanzania;
Sehemu kubwa ya maelezo juu ya tabia hii yapo katika Cultural Forces, ambazo nitajaribu kuzijadili; Nchini Tanzania (na pengine sehemu nyingi za Afrika),
STATUS & WEALTH always depends on the ability to accumulate
Dependents and
Followers; Kwahiyo njia kuu for individuals to Gain Status ni pamoja na kuwa na
watumishi wengi na wa kila aina,
Kuwa na Wake wengi, au
acquisition of clients/patrons/supporters; Suala hili linaendelea kuwa sehemu muhimu ya social structuration nchini Tanzania; Ni katika mazingira, haya,
spending money conspicuously ni njia muhimu for one to gain ‘STATUS' and ‘INFLUENCE';
Tukirudi kwenye mjadala juu ya local community institutions vis a vis civic institutions, katika jamii yetu Tanzania, mtanzania wa leo (hasa mwanasiasa), anakuwa na advantage zaidi iwapo anakuwa associated na anakuwa na LOYALTY zaidi kwenye local community (udini, ukabila, ukanda n.k) institutions kuliko Civic Institutions of the State (raia na Utaifa), ingawa the latter (civic institutions) ni muhimu zaidi kwa ujenzi wa Utaifa, Uzalendo, na Maendeleo ya nchi kwa ujumla; Kuna mifano mingi juu ya hili lakini mfano mmoja ni kwamba - Watanzania wengi wapo tayari kufanya ufisadi na kula rushwa ili kuwa na uwezo
to spend lavishly kwenye private ceremonies ambazo hazina umuhimu kwa Maendeleo ya taifa, kama vile misiba, kitchen party, birthdays, kipa imara, wedding anniversaries, harusi n.k; Wengi hawapo kuwekeza katika civic order kama vile kulipa Kodi TRA au kuwekeza katika economic growth kama njia ya kuchangia ujenzi wa taifa leo la Tanzania; Je, ni kwa nini inakuwa hivi?
It is based on my earlier argument juu ya umuhimu wa informal and community based institutions
vis a vis civic institutions; Kwahiyo kwa watanzania wengi hasa wenye nafasi zao, ni muhimu sana kujilimbikizia mali ili kuwa na uwezo wa kutumia fedha kukidhi matakwa ya community institutions; Pamoja na kwamba ni less rrelevant kwa Maendeleo ya taifa, kufanya hivyo demonstrates their commitment to local community institutions ambapo ndio source yao ya support, respect and social status (badala ya utanzania based on loyalty to civic institutions of the state), or they do so in order to earn enough respect from elders, and at times, women;
Ni vizuri tukajadili japo kidogo suala hili katika muktadha wa chaguzi zetu za ndani na nje ya vyama;
Katika chaguzi kuu, Wagombea wa nafasi kama vile ubunge na udiwani, wanaweza jaribu kusema
THE RIGHT THINGS kuhusu THEIR HONEST OPINION kuhusu MASUALA mbalimbali ya KISERA kwa manufaa ya TAIFA, lakini wanajua fika kwamba kwa wananchi -
‘WHAT THEY SAY' has much less importance than ‘WHAT THEY DO' to demonstrate that
they Care about them or they have a FOLLOWING/Wafuasi/wanakubalika; In order to make a ‘gain' therefore, they have to invest katika kutembeza viloba vya pesa na aina nyingine za ‘tangible rewards' to prospective supporters/voters;
Katika chaguzi mbalimbali, tumeona jinsi gani political actors katika mazingira ya uchumi wetu wa mahaba, wapo tayari kutoa perks mbalimbali kwa potential followers/voters; Hii ni tofauti na tabia ya political candidates katika nchi zilizokomaa kidemokrasia na zenye stronger STATES kama vile Ulaya na Marekani ambapo promises are
‘VERBAL'; Katika uchumi wetu wa mahaba,
accountability at election time is immediate – the candidate must demonstrate personal generosity as part of the process of political campaigning; katika demokrasia zilizokomaa na zenye stronger states, suala hili huja baadae,
especially only if the candidate wins and gets into political office;
Kabla ya kujadili kwa kina dhana ya ECONOMY OF AFFECTION na jinsi gani inachochea rushwa, ningependa kusema tu kwamba – katika Tanzania, rushwa inachangiwa sana pia na FAMILY TIES; Family pressures are so pervasive; Juu kabisa kwenye pyramid of the patronage wapo Mawaziri na Maafisa waandamizi wa Serikali ambao maofisini na majumbani kwao, kutwa kuna mistari mirefu ya relatives, acquaintances, voters n.k, ambao wanaenda
to air their complaints or seek material/economic support; Viongozi wengi wanakuwa hawana jinsi bali kutumia vibaya madaraka yao na kujilimbikizia mali ili kukidhi such irrational demands;
Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their respect, wealth, prestige and social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Viongozi husika ni lazima wawe loyal to their communities kwani
ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE, wengi hutumia the STATE as a PREY (kama sehemu ya kuchuma) and milk it in order to feed their communities, na hali hi itaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu; Na hoja hii inatuingiza kwenye mjadala wa kina juu ya ECONOMY OF AFFECTION;
Jamii yetu ya Tanzania inaendeshwa chini ya mfumo wa
Economy of Affection. Maana yake ni: People make personal investments in reciprocal relations with other individuals as a means of achieving goals that are seen otherwise impossible to attain – such as prestige, social status, wealth n.k; katika mfumo huu, informal institutions ni muhimu kuliko formal institutions, na hata resources allocation hufanyika under the mechanism of informal institutions; Kuna kanuni kadhaa za mfumo wa Economy of Affection lakini muhimu ni tatu:
- Kwanza – Whom You Know is More Crucial Than What You Know;
- Pili - Sharing Personal Wealth is More Crucial Than Investing in Economic Growth;
- Na Tatu - A helping Hand Today Generates Returns Tomorrow;
Ufisadi unachochewa sana na mfumo huu; Hii ni pamoja na ukweli kwamba, mambo ambayo wananchi wengi (hasa vijijini) wana hitaji au wanathamini katika maisha yao ya kila siku - kwa mfano
goods, services, information, etc, kwa mtazamo wa wengi,
all these can only be obtained from others; Ni jadi kwa watanzania kutegemeana
for such valued resources na wanapeana haya kupitia informal process of exchanges ambazo ndio zinazoendesha community institutions; Exchanges muhimu hapa ni pamoja na
Rewards (e.g., Cheo, Status, Power) Or
Punishments (e.g., Kura ya Hapana kwa mgombea nafasi ya uongozi), na hii inategemea iwapo upande husika delivered the promise or didn't deliver;
Kwa mfano, voters may deny political patrons kwa sababu they did not deliver their immediate promises of rewards, hence they punish the patrons kwa kura ya Hapana; Kwa upande mwingine, pia Political patrons wanaweza
punish voters iwapo hawatapiga kura kwa kiasi kilichotarajiwa, na adhabu inaweza kuwa pamoja na serikali husika kutopelekea huduma za kijamii katika maeneo fulani n.k; Kuna utafiti mmoja uliofanywa na Chuo cha UCLA na unaonyesha jinsi gani Wilaya fulani fulani zilipewa adhabu hii na CCM katika kipindi cha 1997 – 2007 (see Laura Weinstein: The Politics of Government Expenditures in Tanzania: 1997 - 2007);
Watanzania wengi (hasa wa vijijini) are not rational when it comes to decision making; na ni inachangiwa sana na Weakness of the State in the hinterland i.e. absence of Civic Institutions to play a prominent, leading and legitimate role over and above community institutions; Katika nchi za wenzetu zilizoendelea zaidi in
terms of Strong & Consolidated States, kwa mfano,
classical microeconomic theory inatoa mwongozo wa kimaamuzi ndani ya jamii husika, ambapo kwa mfano - hakuna long term relations between economic exchange partners; hii ni tofauti na Tanzania ambapo social and economic exchanges zinapendelea partners wa muda mrefu, hasa kwa kutegemeana na Rewards
vis a vis punishments, katika mazingira ya Economy of Affection;
Mfano mwingine ni kwamba, wakati
classical microeconomic theory assumes kwamba actors engage in set of
independent transactions that are aggregated into markets, katika Tanzania,
exchanges are built on premises that actors engage in recurring interdependent exchanges with partners with specific pertners over time and they remain partners as long as they fulfill their promises in the context of the Economy of Affection;
Haya ni baadhi ya masuala yanayochangia kwa kiasi kikubwa tatizo la rushwa ‘kimfumo', hasa ufisadi;
Katika bandiko langu namba moja la mjadala huu, nili ahidi kumalizia mjadala wangu kwa kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike katika kutatua changamoto hizi; Lakini kufanya hivyo nadhani itakuwa sio kuiwatendea haki wadau wengine humu kwani mawazo yenu yatakuwa ni muhimu sana katika kuhitimisha mjadala huu; Kwahiyo niseme tu kwamba hoja yangu ya msingi imekamiliika, kilichosalia ni the way forward, na hili haliwezi kutimia bila ya mchango wenu;
Vinginevyo kwa kifupi tu, ili kukidhi kiu pengine ya baadhi ya wadau humu, ningependa kuhitimisha kama ifuatavyo:
Dr. Slaa, Mangula pamoja na vyama vyao vya siasa havina uwezo wa kutatua tatizo la rushwa na ufisadi tanzania; Sana sana viongozi hawa wawili wanachofanya ni kuaminisha umma kwamba Rushwa katika jamii yetu haikubaliki na haivumiliki tena; As individuals, Dr. Slaa na Mangula, wote wawili wana moral authority kuzungumzia suala la Rushwa na ufisadi licha ya hoja za baadhi ya watu kwamba mangula hana such authority kutokana na kuwa sehemu ya chama ambacho kimeshindwa kutokomeza ufisadi; Nimejadili baadhi ya sababu kwanini vita dhidi ya ufisadi ni ngumu zaidi ya wengi wanavyodhania; CCM kulemewa na ufisadi haitokani moja kwa moja na sababu kwamba eti kuna baadhi ya watu wanaogopwa, bali ni kutokana na ukweli kwamba suala la Ufisadi na rushwa Tanzania ni la kimfumo; Hata Chadema ikifanikiwa kuingia Ikulu 2015, haitaweza kutatua tatizo la ufisadi na badala yake, inaweza kujikuta katika mazingira yanayokaribiana na CCM ya sasa; Moja ya njia sahihi za kujaribu punguza matatizo yanayotokana na makali ya ufisadi kwa vyama vyote hivi viwili ni pamoja na kulitizama tatizo hili kwa jicho kama letu ndani ya mjadala huu;
Ni muhimu kwa vyama hivi viwili kuja na consensus juu ya suala hili la rushwa badala ya kila upande kulitumia kama a political asset vis a vis political liability kuelekea 2015, huku equilibrium to wananchi walio wengi, kutokana na mchakato husika, ikiwa haina mwelekeo; It is about time sasa tuanze kushughulikia tatizo la Ufisadi kwa kuendeleza Formation and consolidation of the state of Tanzania kwani bado kazi haijaisha (e.g. kuna maeneo wananchi hawajui serikali ni nini, civics ni kitu gani, au economic, political and social justice vitu gani), kwani kwa kufanya hivyo, tutaweza kufanikiwa kuanza kuishi collectively in a modern state kama taifa na kuondokana na duality ya hivi sasa ambayo ipo dominated zaidi na community institutions and their informalities kama tulivyo jadili;
Moja ya njia effective za kuleta ufumbuzi ni kuanza kujenga Loyalty ya umma to the State and its civic institutions, na kundokana na Loyalty to local communities and their institutions kama zilivyo sasa, ambazo kama tulivyokwisha ona, zinachangia sana viongozi kuwa mafisadi; Ni muhimu tukaachana na Affective Society na tuka hamia kwenye Civil Society kwani Civic Society inatawaliwa kwa mujibu wa principles, rule of law, enhancement of citizen voice na universality unlike Affective Society;
Naomba kuwasilisha;