Mchambuzi hii ni bonge ya ujumbena chujio lenye lengo ni kuonyesha Watanzania, Tanzania BORA na Watu BORA wenye SIHA na akili Timamu wapotayari kulijenga TAIFA.
Katika chaguzi kuu, Wagombea wa nafasi kama vile ubunge na udiwani, wanaweza jaribu kusema THE RIGHT THINGS kuhusu THEIR HONEST OPINION kuhusu MASUALA mbalimbali ya KISERA kwa manufaa ya TAIFA, lakini wanajua fika kwamba kwa wananchi - ‘WHAT THEY SAY' has much less importance than ‘WHAT THEY DO' to demonstrate that they Care about them or they have a FOLLOWING/Wafuasi/wanakubalika; In order to make a ‘gain' therefore, they have to invest katika kutembeza viloba vya pesa na aina nyingine za ‘tangible rewards' to prospective supporters/voters;
KIlichotoke!!!!
Mchambuzi hapa ndio tatizo uanzia,mara baada ya Mwalimu kungatuka na vision yake ya Ujamaa wa kiafrika na kwa kuwa alikuwa yeye ndio oversee wa kila kilochokuwa ndani ya serikali basi ukosefu wa taasisi hakikishi na ng'amuzi za kikatiba kwenye mfumo ombwe likazaliwa.Mwalimu alijitahidi sana kujenga ujamaa wa kiafrika,lakini kama binadamu akapungukiwa kutengeneza economical, financial and national security heathly watchdogs and monitors.Hapa nguvu nyingi zake akaziweka kwenye ujenzi wa wananchi wajisikie kutumikiwa na serikali yao na si wao pia kuitumikia serikali yao kwa uaminifu na kwa kujivuna kwa uzalendo.
Mapungufu yetu ambayo yametokana na toka mwanzo kwa sisi, kutokuwa na taasisi zilizoundwa kwa nguvu ya usimamizi wa kikatiba katiba,yani Constitutionalise Institutions, hasa kwenye sekta ya uchumi, usalama, fedha, na mengineyo mambo muhimu kama governmental and all citizen constitutional norms.
Nikupitia aina hiyo ya uelewa wa chaguzi wananchi wanapokea wasichotaka na wanasiasa wanatoa wasiyoyamini.
Kifanyike nini!!!
Kupitia ujio wa katiba mpya taasisi za usimamizi, utekelezaji, hakikishi na ungamuzi ziwepo kama nguzo mama kupitia kwenye katiba majukumu yake yatambulike kikatiba dhidi ya sekta nyeti na muhim kama uchumi,Afya,elimu, Huduma za Umma, uchumi, fedha na maliasili.Vipewe jicho la kikatiba kwa miaka hamsini ijayo mbele toka sasa!!Mpaka pale kizazi kilichopo sasa chenye umri wa miaka 15 kitapokuwa na umri wa miaka 65 kinaweza kufanya marekebisho kuondoa baadhi ya articles ili kukidhi muongo huo wa nusu karne kutosha kupitia mabadilko ya kitamaduni, kisiasa na uchumi.Vinginevyo pale patakapo kuwepo wito wa dharula ya Taifa ufanye mabadiliko ya kifungu kwa mujibu wa lazimiko la ridhaa ya umma.
Mchambuzi said:
ya kujadili kwa kina dhana ya ECONOMY OF AFFECTION na jinsi gani inachochea rushwa, ningependa kusema tu kwamba – katika Tanzania, rushwa inachangiwa sana pia na FAMILY TIES; Family pressures are so pervasive; Juu kabisa kwenye pyramid of the patronage wapo Mawaziri na Maafisa waandamizi wa Serikali ambao maofisini na majumbani kwao, kutwa kuna mistari mirefu ya relatives, acquaintances, voters n.k, ambao wanaenda to air their complaints or seek material/economic support; Viongozi wengi wanakuwa hawana jinsi bali kutumia vibaya madaraka yao na kujilimbikizia mali ili kukidhi such irrational demands;
Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their respect, wealth, prestige and social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Viongozi husika ni lazima wawe loyal to their communities kwani ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE, wengi hutumia the STATE as a PREY (kama sehemu ya kuchuma) and milk it in order to feed their communities, na hali hi itaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu; Na hoja hii inatuingiza kwenye mjadala wa kina juu ya ECONOMY OF AFFECTION;
Hapa nakili kuwa ili ndilo gonjwa kubwa pia kwa jamii,yani ngazi ya familia ambayo ndio nchi namba moja, imezalisha uovu mbaya wa kifikra kwa wanajamii wake, kiasi kuwa mwenye uwezo kwenye familia yani anae jiweza kimapato [Hasa Ukwasi] basi mwanafamilia huyo atapewa heshima kubwa sana na wanafamilia kupita ata anaemzidi umri ndani ya familia husika.
Imefikia hatua wazazi wanawatoto kadha ndani linapotokea jambo la muhimu la familia kama Msiba au Harusi za kifamilia, aliye kwenye uwezo kimaisha kwa misingi ya kipato kikubwa japo aweza kuwa ana umri mdogo kupita wenzie basi familia husika mwenyekipato ndie atakuwa wa kwanza kutaarifiwa tukio husika na kisha yeye kuwa na jukumu la kuwajulisha wengine.Na kama ikitokea akawa na mahusiano yasiyo mazuri na wenzie basi wenzi wake hao hawatapata nafasi ya kujua kinacho endelea kwenye familia yao zaidi ya kusikia kutoka kwa wanajamii wengine yaliyojili.
Hivyo tabia na mwenendo uliozalishwa na jamii uku baadhi ya kabila zikiwa na tamaduni za kuthamin mali [materilism] na hivyo kuambukiza jamii za makabila mengine kupitia mahusiano ya kuona zimezaliwa tabia ambazo kwa serikali uenda zinaonekana kama ni tabia binafsi lakini ukweli zina madhara sana kwenye familia na hatimae Taifa zima kwa ujumla.
Wakoloni walijifunza sana tabia za makabila yetu mengi hivyo kufikia hatua ya kujua kabila gani litumike wapi kwa wingi kwenye eneo lipi. Japo ilikuwa ni kwa faida ya serikali ya kikoloni lakini kuna sehemu zilileta matunda mazuri,ukiondoa ile ya kuwagawa watu kwa nia ya kutawala.Inaeleweka sana wakurya wanaufanisi sana katika kazi za ulinzi, wasukuma ni wachapa kazi n.k.
Llakini sijui na sina ushahidi kwa ili kama kweli serikali yetu inajua ina Taifa [National stereo type] la watu wenye aina gani za tabia,ukizingatia mwingilino wa tabia za makabila tofauti tofauti [50/50] kwa sasa kutokana na kuona.Kama familia hapo zamani zilioana kwa kuangalia mambo ya msingi toka familia moja kwenda nyingine kama UKOMA,UCHAWI,WIZI,UONGO nk.Sembuse Serikali kuangalia watu wake na watendaji wake kwenye msingi hiyo ya kuhakiki tabia za wanajamii zake ambao kwa ujumla wake uzaa Tabia za TAIFA ambazo ndio uzalisha jumuisho la picha ya jamii ilivyo.Tukiwaona omba omba mitaani ni zao la tabia zetu ambazo zimezalisha matatizo hayo na mzigo ule wa omba omba umebaki kuwa kuwa omba omba ni ishara ya tatizo la familia husika,lakini mwisho wa yote inakuja kuwa ni mzigo wa serikali,ambayo nayo haitaki kutambua na kushiriki kama mlezi number moja kabla ya familia.Kwa mfano mdogo wa omba omba tulio nao mitaani ukijiuliza tumefikaje hapo walipo na nani anajukumu nao!!!wakija wageni wanatupima pia kupitia omba omba hao.
Uwa nasikia kichefu chefu sana pale ikitokea mwanasiasa au mtendaji wa serikali akabanwa na jambo kama la kuulizwa kuhusu ombaomba anaweza kukwambia mbona sie tunao wachache uko marekani au uk wako wengi zaidi sana!!!ni aibu kwamba uchache wa omba omba kwetu ni reference kwa wengine,why not sisi tusiwe wa kwanza kuonyeshewa kidole kuwa watanzania hawana omba omba duniani,kama tunavyooshewa kidole kuwa ni nchi pekee yenye tanzanite, na baraka za madini tele kama almas, dhahabu, ruby n.k.
Uwa naumia sana sana,pale nipona jamii kulazimisha kwamba swala la MAADILI ya Jamii kuwa ni swala la FAMILIA,HAKIKA KUTOKA MOYONI MWANGU,NAAMINI KWA DHATI KABISA KUWA TAIFA LIMEFIKA HAPA LILIPOFIKA BAADA YA SERIKALI KUJITOA KWENYE KUSIMAMIA MAADILI YA TAIFA NA MAADILI YA SERIKALI NA VIONGOZI WAKE.
Zamani jamii ngazi ya mtaa walikuwa na uwezo wa kuwa na wazee wakiwa na kamati maalum ya watendaji mtaani wenye busara zinazokubalika na watendaji wakuu wa serikali, kamati hiyo ndogo ngazi ya mtaa walikuwa na uwezo wa kumuonya na kutoa amri ambayo ingefuatwa na watendaji wa serikali dhidi ya kijana, mtoto au mwanajamii yoyote ambae matendo yake yana athari kwa jamii husika mtaani.Lakini leo thubutu!!!!!!!!!!!!!!.
Picha inayopatikana hapo ni TAIFA KUTOKUWA NA MAADILI na maendeleo yake maadili yanayozalishwa ugeuka kuwa tabia na kama jamii ina maadili ya kiovu na hakuna wa kuyasimamia basi jamii itegemee kupokea ushenzi wa maadili hayo iliyochagua.
Nini Kifanyike!!
Serikali kupitia ujio wa katiba mpya kujiandaa na institutional zitakazo kuwa na kazi ya kujenga maadili ya FAMILIA yani KAYA UMMA yani JAMII, MAADILI YA VIONGOZI yani Watendaji wa SERIKALI na Watendaji wa Vyama vya Siasa na Mashrika ya Umma na yasiyo ya Umma,MAADILI YA SEKTA BINAFSI, na MWISHO UZALENDO WA KULIFIA TAIFA.Leo hii popote pale mmarekani alipo anajua haki yake na yuko proud kulitangaza TAIFA lake.
Kuna wakati nilipata kusikia mahojiano ya kingereza ya sauti ya BBC,ilikuwa ikiwahoji raia wa kinajelia Nchini mwao,swali la mtangaji wa BBC lilikuwa "ARE YOU READY TO DIE FOR NIGERIA?". Kati ya walio hojiwa hakuna aliyesema YES!!!Ndio kusema walikofika wao kiupeo kwao HAKUNA MOTHERLAND bali mimi binafsi naona kama wapitaji.Kupitia accent yao kila mmoja aliekuwa anaohojiwa alikua anajibu "WHY SHALL I DIE FOR NIGERIA YOOOO, WHAT AS IT DONE FOR ME YOOOOO?] yani mtangazaji aliishia kuulizwa swali huku alikusudia kujibiwa swali.Tusifike huko ambako eti jukumu la kuifia nchi linabakizwa mikononi mwa wanajeshi [JWTZ] na kumbe wale ni walinzi wa AMANI TU lakini mlinzi wa NCHI ni MWANAWANCHI.
Ndio maana na wewe Mchambuzi unakuja na swali je rushwa ya Tanzania aka UFISADI tiba yake itatolewa na watu wawili MANGULA na KINANA?Kumbe wawili hawa si lolote lile bali ni tone dogo sana ndani ya bahari kubwa sana.Itakuwa na nguvu ya soda kwa kuwa kwa kutegemea watu hao wawili kuimaliza RUSHWA au UFISADI umetamalaki, nao watapita na uenda wakawa mark,kama ilivyodesturi yetu kwenye misemo ya kiswahili ya kuwa wewe nani walikuwepo kina fulani walishindwa sembuse wewe wa juzi juzi.Hivi hatuwezi kusema jambo na tukatenda kama tulivyosema.Siko hata kuwapigia dege magufuri na mwakyembe,hawa jamaa wamepewa nafasi za kimaamuzi kwa kiasi wameonyesha kuwa wanaweza.Hivi kiukweli toka moyoni mawaziri wote wakawa na sura ya MAGUMWAKYE hakika tutakuwa na miaka mitatu watanzania watasupport Taifa lao na Nchi itaamia eneo tofauti sana kimuonekano na hata siha na akili ya wananchi.
Taaluma za watu hawa wawili muhandisi na mwanasheria ni moja ya vigezo ambavyo pia vimechangia kwa ukweli jamaa hawa kudeliver kwenye misingi isiyo na hofu.Kwa watu waliopita shule wanajua hili, mtu yoyote aliyepata elimu yake kimagumashi na hata siku akipewa nafasi pia utendaji wake utakuwa ni wakimagumashi pia hivyo tuna dhohofisha jamii.
Kuna pia swala la UAFRIKA hapa hakika serikali yapaswa kukaa na wazee, wanajadi na viongozi wa dini zote na kupata kikosi kazi [TASK FORCE] ya kulivusha TAIFA toka kwenye hili,manake ili nalo limekuwa ni tatizo ambalo NCHI imefika hapa sababu ya mashindano yaliyokosa watu wa kuomba BUSARA na NGUVU ya KIMUNGU. Na kwa upande mwingine kwa wale watu wa zamani kuomba ruksa ya wazee [Ancestors] yani kana kwamba baadhi ya wanajami wamekosa mwongozo wa wazee wa jadi na kila mmoja amekuwa akijamulia kutenda yake na kudhuru wengine na hakuna wa kumemea.Kwa walio na jadi inaeleweka kuwa kuna wazee wanaongoza misingi mizima kwenye eneo hilo na kuzuia na hata kumuazibu yoyote au chochote kinachotendwa na mwanajamii kinyume na wanajamii wenzie.Zamani wanajadi waliongozwa na machifu wakishrikina na wazee!! Machifu bado wapo kwa kushirikiana na serikali huku nao wakipewa heshima kama viongozi wa kijamii wenye nafasi basi jamii italekebishwa kwa kupitia kabila husika chini ya miongozo ya machifu na wazee wa jadi husika na kama mhusika akionekana kuzidi nguvu ya kabila au jamaa yake basi vyema kupata msaada wa wazee wa jaai na machifu wa jamii nzingine za karibu.
Leo hii tunao waona mafisadi kwenye jamii,wakiitwa mbele ya viongozi wa dini wakaambiwa kutubu,sijui lakini kwa maono yangu wengi wataitikia usoni lakini ndani ya dhamila zao ni wachache sana watakubali kuwa ZAKAYO mtozo ushuru.Ila hao hao wakisikia wanaitwa na viongozi wao wa kikabila watu kama machifu na wazee wengine muhimu kwenye kabila husika basi kitakacho jili yatakuwa maajabu kwa watu kuona aliyekuwa FISADI amegeuka kuwa MPINGA ufisadi mpaka anaingia kaburini.UAFRICANIZATION bado unachukua nafasi kubwa sana kwenye jamii yetu,ndio maana Nyerere na ukubwa wake kama Rais lakini nae alikuwa akifika Butyama anakuta kuna kiongozi wake kwenye kabila lake.
Vivyo hivyo Serikali ikisisitiza na kuimarisha mifumo ya elimu za kifamilia na kusoma mazingira ya familia za kitanzania ambavyo zinaishi na kutumia mfumo ule kukuza na kujenga elimu ya kueneza kwa jamii,na hakika utakuta kuwa, kila familia ina kiongozi wake ambae pia nao kwa kujua wana nafasi kwenye jamii basi serikali ikatengeneza forum ambazo zinatoa nafasi kwa viongozi wa familia kuhudhuria na kutoa mafundisho kwa viongozi hao ambao nao uenda kuzitoa kwa wale wanaowangoza kutoka katika kaya wanazoziwakilisha kwenye familia za makabila husika.
Kuna famila moja siku za karibuni walifikishana mahakamani kupinga uamuzi wa baadhi ya wanafamilia kumchagua mwenzao ambae alionekana kupingwa na upande mweingine.Kupitia aina hiyo ya muonekano wa kiongozi wa familia kupingwa mahakamani basi serikali yaweza kuona ni muhimu kiasi gani hawa wadau kwenye sekta ya MAADILI walivyo muhimu.
Mchambuzi said:
Jamii yetu ya Tanzania inaendeshwa chini ya mfumo wa
Economy of Affection. Maana yake ni: People make personal investments in reciprocal relations with other individuals as a means of achieving goals that are seen otherwise impossible to attain – such as prestige, social status, wealth n.k; katika mfumo huu, informal institutions ni muhimu kuliko formal institutions, na hata resources allocation hufanyika under the mechanism of informal institutions; Kuna kanuni kadhaa za mfumo wa Economy of Affection lakini muhimu ni tatu:
- Kwanza – Whom You Know is More Crucial Than What You Know;
- Pili - Sharing Personal Wealth is More Crucial Than Investing in Economic Growth;
- Na Tatu - A helping Hand Today Generates Returns Tomorrow;
Familia zetu nyingi zimejengwa na walioathrika na swala hilo wamejikuta waanga.Waliobezwa kwenye ngazi ya familia kama Baba aliyekuwa hana kitu mbele ya ndugu zake,akajitahidi kusomesha watoto wake,na watoto waliolelewa na Baba aliyenyanyapaliwa na ndugu zake wenye uwezo wanakuwa na kilema cha kuamini ili uwe bora na kuthaminika kwenye jamii ni lazima uwe na kitu/mali [Materiliasm] basi kwa liwalo liwe kwa halali na haramu watoto wale wataangaika ili walipize/compasate maonezi ya kisaikolojia aliyopitia mzazi wao.
Kwa picha hiyo ya ngazi ya familia,mtoto huyo uenda alijibiidisha kusoma na kufanikiwa kupata elimu nzuri iliyomfikisha kupewa dhamana ya ofisi au taasisi.Basi madhara ya kilema chake kilichotokana na mateso ya kisaikolojia ya baba yao basi watalipiza kwa kujilimbikizia saana kwanza kulipiza kwa watesi wao, pili kwa ajili ya self defense kuwaandalia watoto wao wasije wakambuna na aibu.Na wanasahau MUNGU pia anamakusidio yake kwa watoto wao pia.Vilema hivyo vingi vingi na tofauti toka toka familia na makabila mengi mengi tofauti ndio vimejaa na kuzalisha JAMII UBINAFSI.Manake RUSHWA kwa lugha nyepesi ni UBINAFSI yani kilichopaswa kipatikane kwa wengi kwa misingi ya usawa, atakipata mmoja kwa misingi ya umaalumu [Privilege].
Mchambuzi said:
unachochewa sana na mfumo huu; Hii ni pamoja na ukweli kwamba, mambo ambayo wananchi wengi (hasa vijijini) wana hitaji au wanathamini katika maisha yao ya kila siku - kwa mfano goods, services, information, etc, kwa mtazamo wa wengi, all these can only be obtained from others; Ni jadi kwa watanzania kutegemeana for such valued resources na wanapeana haya kupitia informal process of exchanges ambazo ndio zinazoendesha community institutions; Exchanges muhimu hapa ni pamoja na Rewards (e.g., Cheo, Status, Power) Or Punishments (e.g., Kura ya Hapana kwa mgombea nafasi ya uongozi), na hii inategemea iwapo upande husika delivered the promise or didn't deliver;
Kwa mfano, voters may deny political patrons kwa sababu they did not deliver their immediate promises of rewards, hence they punish the patrons kwa kura ya Hapana; Kwa upande mwingine, pia Political patrons wanaweza punish voters iwapo hawatapiga kura kwa kiasi kilichotarajiwa, na adhabu inaweza kuwa pamoja na serikali husika kutopelekea huduma za kijamii katika maeneo fulani n.k; Kuna utafiti mmoja uliofanywa na Chuo cha UCLA na unaonyesha jinsi gani Wilaya fulani fulani zilipewa adhabu hii na CCM katika kipindi cha 1997 – 2007 (see Laura Weinstein: The Politics of Government Expenditures in Tanzania: 1997 - 2007);
Watanzania wengi (hasa wa vijijini) are not rational when it comes to decision making; na ni inachangiwa sana na Weakness of the State in the hinterland i.e. absence of Civic Institutions to play a prominent, leading and legitimate role over and above community institutions; Katika nchi za wenzetu zilizoendelea zaidi in terms of Strong & Consolidated States, kwa mfano, classical microeconomic theory inatoa mwongozo wa kimaamuzi ndani ya jamii husika, ambapo kwa mfano - hakuna long term relations between economic exchange partners; hii ni tofauti na Tanzania ambapo social and economic exchanges zinapendelea partners wa muda mrefu, hasa kwa kutegemeana na Rewards vis a vis punishments, katika mazingira ya Economy of Affection;
Ni kwa picha hii pia jamii kwa utambuka wake umetumia kipato cha mgombea kujipatia manufaa binafsi.Kuna Mheshimiwa mmoja ambae ni marehemu [R.I.P] alikwenda nyumbani kwao kugombea,akitokea Dar es Salaam,lakini kabla siku za nyuma akiwa mtendaji wa umma nae ni mwenyeji wa kutoka moja ya makabila yanayoheshimu undugu sana,baadhi ya ndugu zake walipokuwa wakifunga safari kuja Dar es salaam toka nyumbani kwao Mheshimiwa huyo,wakifika kwake wanakutana na mama mwenye nyumba ambae ni mwenyeji wa mikoa ya kaskazini, basi kwa haiba ya upande wa pili ya kutopenda mlundikano wa watu nyumbani akawa anawaludishia mlangoni.Basi wanajamii wale toka kanda ya ziwa magharibi walipokuwa wanatimuliwa na wanafungasha mizigp kuludi zao kijijini na kuja kumshtaki jamaa yao kwa wanajamii wao.
Siku ya siku muhusika nae ukafika wakati akapata fursa ya kuiingia kwenye siasa na kuona aende kwao kwa kuwa nyumbani ni nyumbani hata kama ni pangoni [Home Sweet Home].Kafika nyumbani wakampokea, akwaambia wanajamii wake ambao kwa hakika walimsikiliza na mwisho wa yote mpaka anatoka duniani hawakumpa tketi yao ya kuwawakilisha kwenye Bunge, pamoja na kuwa na vigezo marudufu kuzidi wapinzani wake lakini kamwe hawakumpa wakimuathibu kwa tendo la mkewe kuwaludishia mlangoni wakti kwa jadi yao ukibalikiwa kuwa na familia wageni wa jamii yako ni sehemu ya maisha yako.
Mchambuzi said:
mwingine ni kwamba, wakati classical microeconomic theory assumes kwamba actors engage in set of independent transactions that are aggregated into markets, katika Tanzania, exchanges are built on premises that actors engage in recurring interdependent exchanges with partners with specific pertners over time and they remain partners as long as they fulfill their promises in the context of the Economy of Affection;
Hapa Mkuu umepigilia msumali kama nilivyosema awali Mwalimu alipungukiwa ufahamu na ili silioni kwake kama kosa bali ndio uwezo wake kwa zama zile mtoto mchumgambuzi aliyesoma na kuja kuwa Rais lakini akatenda yale yaliyo ndani ya uwezo wake.
Mwalimu anaingia kwenye ofisi anakuta kuna sekta ya uchumi, fedha, mataifa, Afya, Elimu, biashara n,k.Yote hayo yanaitaji uyapambanue kwa kiwango chako ili utapopewa report nawe uamue kwa jinsi unavyoona inafaha basi haikuwa kazi nyepesi hata kidogo.Wahindi na waarabu waliokuwa na kulelewa toka watoto wakipokea change na kutoa change kwenye madirisha ya maduka ya baba zao wakiwa watoto,leo wanakuja kupimana na mtoto wakati wao wanapokea fedha dukani yeye anachunga mbuzi.Unaweza kuona uzoefu na ufahamu katika sekta ya biashara na uchumi.Japo wataalamu wanasema watoto uchukua asilimia 80% kwa kulithi akili za wazazi na asilia 20% inatokana na kuadapt mazingira wanayoishi.Hivyo akuweza kuwa genius kuweza kujua namna gani anaweza kujenga na kusimamia sera za uchumi wakati kipawa cha familia yake inherit ni kutawala jamii kwa amani.Wazanaki kwa asilia walikuwa ni watawala wazuri waliopenda majadiliano zaidi kuliko malumbano.Leo hii ukiwa Rais wa marekani wataalmu ufuatilia kwa umakini familia ya mgombea toka vizazi na vizazi.
Hakika tulilithi aina hiyo ya mfumo wa kibiashara watanzania wenye asili ya kiasia [Waarabu na Wahinid] matokeo yake tumefika hapo tulipofika.
Tunaitaji mabadiliko yatakayo ratibiwa na Serikali,wakati mwingine Serikali kutoa Tender za Seriakli kwa makusudi zenye sura ya joint venture kati ya ethnics hizi za Wahindi, Waarabu na Waswahili,Yani kama kuna muhindi au Mwarabu au Mswahili wanajiweza kwenye Tender tajwa wanapewa hiyo Join venture kuondoa hizo tofauti za kimitizamo.Sio siri sekta ya biashara kubwa zimemezwa na makundi machache ya aina fulani ya watu kabila hasa wahindi na waarabu.Ila sehemu ambayo mimi mwenyewe nakili kuwa Mwalimu akuangalia kwa jicho la umakini ni swala la BIASHARA, FEDHA na UCHUMI na MAHUSIANO haswa kwa hawa ndugu zetu wenye asilia ya kiasia [Wahindi na Waarabu] aliwakumbatia sana na hakuwa na shaka na ushriki wao kwenye sekta tajwa.
Mchambuzi said:
Ni muhimu kwa vyama hivi viwili kuja na consensus juu ya suala hili la rushwa badala ya kila upande kulitumia kama a political asset vis a vis political liability kuelekea 2015, huku equilibrium to wananchi walio wengi, kutokana na mchakato husika, ikiwa haina mwelekeo; It is about time sasa tuanze kushughulikia tatizo la Ufisadi kwa kuendeleza Formation and consolidation of the state of Tanzania kwani bado kazi haijaisha (e.g. kuna maeneo wananchi hawajui serikali ni nini, civics ni kitu gani, au economic, political and social justice vitu gani), kwani kwa kufanya hivyo, tutaweza kufanikiwa kuanza kuishi collectively in a modern state kama taifa na kuondokana na duality ya hivi sasa ambayo ipo dominated zaidi na community institutions and their informalities kama tulivyo jadili;
Nami nakumbuka kusema siku zilizopita huko nyuma mara kadha wa kadha TUFIKE POINT TAIFA liunde
TANZANIA UFISADI RECONCILIATION COMMITTE [TURC] .Lengo litakuwa ni kuondoa SINTOFAHAMU, LETE USHAIDI, HUNA MORAL AUTHORITY, MBONA NI MIMI NA SIO YULE, na mengineyo mengi.
Ndani ya TURC wanakamati amabayo itakuwa na mandate kisheria yatakayobainika humu ndani kwa kipindi cha miaka miwili yatoe hitimisho kuhusu
corruption and fisaidim ndani ya Taifa.Ushauri wangu wanakamati wawe viongozi wa dini, viongozi wa jadi, wanasheria, wanadiplomasia makini.
Na toka kwenye TRUC Taifa lije na Taasisi za KiKATIBA [Constutional Institutions] zitakazo kidhi mahitaji ya kukomesha rushwa kama si kumaliza kabisa rushwa.Mfano Mkurugenzi wa TAKUKURU na UWT wateuliwe na Rais na kupigiwa kura na BUNGE.Na taasisi zao ziwajibike kwa BUNGE na kuwe na kamati maaalumu zisizo za kibunge zenye dhamana muhimu kama watchdog wa taasisi husika ambazo ziko tayari kuwajibika bungeni na kujibu maendeleo ya TAASISI husika wakishirikiana na Mkurugenzi husika.Hakika tumechelewa lakin tunaweza kuiwai treni PUGU na safari yetu kwenda mkoani bara ikawa ya heri..Tatizo kuna foleni [Traffic Jam] tunaitaji dereva mtundu, anaejua chocholo, anaejua lugha ya kuongea na trafiki wampe green right tupite kwa haraka atakae weza kuikwepa foleni hiyo na kuakisha kuwa tunafika PUGU kabla treni aijachukua kasi kuelekea Morogoro ,tusije anza tena kasi ya kuitafuta Morogoro kwa nia ya kuiwai huko.Tunaitaji dereva anaejua njia zitakazo tufikisha kituoc sahihi ya kudandia Treni halisi.
aKSANTE mCHAMBUZI kwa uchambuzi wenye KUFIKILISHA UBONGO!!!Manake tatizo la wanaotuongoza
1: Hawataki kufikilisha Ubongo
2: Hawapendi kuwa na vya kwetu ambavyo vitafanana nasi kwa tabia na matendo
3: Hawaitaji kujifunza au kusoma na hivyo kujua ishara za kuwa kesho itakuwaje ama uenda ikafananaje!!
4: Wamaamini wanajua kuliko umma unavyojua.
5: Wameupuuza Umma na Jamii na Jadi imeeacha ijiamulie ili mladi wao wako salama.