Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #61
DSN,
Namba 58 - hoja yako kuhusu ugumu wa bottom - up approach, hasa kuhusu jinsi gani kila mtu anachotafuta ni atoke ili asiwe kama wao tena, naikubali; ni moja ya vikwazo vikubwa sana, hasa kutokana na kukosekana kwa uzalendo, lakini muhimu zaidi, kutokana na uwepo wa a weak state ambayo sense of citizenship and civic duties ni kama haipo; Pia mchango wako juu ya suala hili unazidi kuthibitisha jinsi gani economy of affection ilivyokuwa na nguvu, hasa katika mjadala wako juu ya jinsi gani mtu akipata uongozi, ni muhimu kwa yeye kwenda kufanya ufisadi ili aje kununua tena nafasi ya uongozi kwa wale ambao hapo awali walikuwa ni wenzake (at the bottom), lakini sasa sio mwenzao tena;
Mfano wako juu ya Ullimboka - ni lazima watu wapoteze maisha, waumie, wafungwe, kwani kinachoendelea ni vita, sio mchezo wa kushindania kombe; bila watu kupoteza maisha, kufungwa n.k, hakuna la maana litakaloweza kutokea; umeona jinsi gani watu walivyo poteza maisha Libya, Tunisia, Algeria, Misri, na hata hivi sasa Syria; Kama kuna a political cause, watu kufa haitawazuia kujitafuta mabadiliko; Lakini hapa sina maana kwamba vita dhidi ya ufisadi ni lazima vifuate mkondo wa ghasia na mapinduzi, nia yangu ni kukueleza tu kwamba ikifikia hali hiyo, hayo ni maamuzi ya umma na kama wapo determined, watafanikiwa tu, bila ya kujalisha ni wangapi wamepoteza maisha; Vinginevyo, katika bandiko namba 59 nimeweka jedwali la kutusaidia tujadiliane iwapo tunahitaji a political party or a political movement kuondokana na mdudu ufisadi katika taifa letu;
Hoja yako kuhusu impact ya Jamiiforums katika jamii ya Tanzania - ni kweli, imetoa mchango mkubwa sana, lakini sidhani kama mtu ukiamua kuweka maslahi mbele na kujadili masuala badala ya watu utauawa, sana sana utatengwa, utatukanwa, utatishiwa maisha, na itaishia hapo; Lakini pia sishauri watu wajitokeze iwapo kazi yao ni kulipua tu mabomu na kuvua nguo viongozi, kwani hata kwa madogo haya ya kujadili CCM critically, kuna usumbufu wa hapa na pale unaojitokeza, na hata mimi nakumbana nao mara nyingi pamoja na vitisho vya hapa na pale, lakini kwa vile naamini zaidi katika taifa langu, na sivunji kanuni yoyote ya chama kama mwanachama au kutishia usalama wa nchi, sina haja ya kuogopa; Vinginevyo kwa kweli nasumbuliwa, na hata ikitokea siku nimepata matatizo, mjue nilitamka hilo;
Mwisho, kuhusu TAKUKURU mashuleni, kama ulinisoma vizuri, TAKUKURU haiwezi kufanya kazi ile kwa ufanisi bali NGO au taasisi yoyote yenye sura ya civil society; Kwa upande wa TAKUKURU, TISS, DPP, Polisi, sana sana ni kuboresha mfumo ili kuwepo na checks and balance ya kweli, sio ya ubabaishaji kama ilivyo hivi sasa;

Last edited by a moderator: