Mangungu ni Kama alishtukia kamchezo ka mhindi wa Bombay alikotaka kukafanya ili na yeye akae pembeni afanikishe jambo lake lakini mtoto wa mjini akausoma mchezo kwa umakini na kuupangua!
Bwana kanjibhai karudisha wajumbe wa bodi wale wale kina try again Sasa unajiuliza kulikuwa na haja Gani ya wajumbe hao kujiuzulu?
Wanajiuzulu asubuhi alafu jioni wanarudi Tena???
Wajumbe hao si ndio waliosema wanajiuzulu kwa kushindwa kufikia malengo ya klabu imekuwaje Tena wanarudishwa na wanakubali kurudi?
Ina maana kulikuwa na kamchezo kanafanyika ili kusudi apigwe pia mangungu presha ya kujiuzulu na jopo lake Kisha mhindi arudishe jeshi lake lilelile kwa mlango wa nyuma afanye yake!
Nampongeza mangungu kwa intelijensia yake Kali na aendelee kushikilia hapo hapo kumbe Kuna watu wanataka kuipora Simba kirejareja!
Try again alijiuzulu akaomba mhindi arudi kuwa mwenyekiti wa bodi, Kisha mhindi amemteua Tena kuwa mjumbe wa bodi hivi vichekesho tunaviona Simba tu walahi!