Mangungu: Basi la Timu limeuzwa, haliko kwenye matengenezo kama ilivyotajwa awali

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Yaliyomo yamo, habar kamili [emoji116]

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu ameeleza kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na halipo kwenye matengenezo tofauti na ilivyoelezwa hapo awali.

Murtaza amesema hayo leo, Januari 20, 2022 wakati akifanya kampeni za kuomba kura za kuendelea kushikilia nafasi hiyo Uenyekiti katika uchaguzi utakaofanyika Januari 29, 2023.

"Basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa mjumbe wa bodi wala Mwenyekiti wa timu kama nilivyo sasa lakini baada ya kufuatilia hili suala lilipelekwa kwenye bodi ya klabu na wajumbe tumefuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata taratibu,” amesema Mangungu.



 
Mbona bus liliuzwa kitambo tu na matangazo yalitolewa? Ama ni bus gani tena limeuzwa?
Linalozungumziwa ni basi walilopewa na Sports Pesa. Hili liliuzwa na utaratibu ulitangazwa.Sio haya mapya.Aliyosema yapo matengenezo yapo na mojawapo lilitumika kuwabeba Simba Queens kwenye mechi yao huko Lindi Jumamosi iliyopita. Wacheni majungu Utopolo.
 
Utopolo ni nani?
 
Mbona bus liliuzwa kitambo tu na matangazo yalitolewa? Ama ni bus gani tena limeuzwa?
Waandishi wameamua kata kipande cha mwanzo alichosema Mwaka 2020/09 alipoingia kazini alikuta basi limeuzwa sababu utengenezaji wake ulikuwa gharama sana na ulifata taratibu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…