Mangungu: Basi la Timu limeuzwa, haliko kwenye matengenezo kama ilivyotajwa awali

Mangungu: Basi la Timu limeuzwa, haliko kwenye matengenezo kama ilivyotajwa awali

Yaliyomo yamo, habar kamili [emoji116]

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu ameeleza kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na halipo kwenye matengenezo tofauti na ilivyoelezwa hapo awali.

Murtaza amesema hayo leo, Januari 20, 2022 wakati akifanya kampeni za kuomba kura za kuendelea kushikilia nafasi hiyo Uenyekiti katika uchaguzi utakaofanyika Januari 29, 2023.

"Basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa mjumbe wa bodi wala Mwenyekiti wa timu kama nilivyo sasa lakini baada ya kufuatilia hili suala lilipelekwa kwenye bodi ya klabu na wajumbe tumefuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata taratibu,” amesema Mangungu.

Hilo basi analosema limeuzwa ni lipi? Lililouzwa kabla hajaingia madarakani tunalijua liliuzwa Mtwara. Hili la Africarriers tuliloambiwa na Ahmed Ally nalo limeizwa?
 
Hilo basi analosema limeuzwa ni lipi? Lililouzwa kabla hajaingia madarakani tunalijua liliuzwa Mtwara. Hili la Africarriers tuliloambiwa na Ahmed Ally nalo limeizwa?
Yote Mkuu ndiyo maana timu yetu siku hizi inakodi daladala za Buza
 
Sasa nimeanini kwanini wale wazee wakiongozwa na Kilomoni walikataa kukabidhi Nyaraka muhimu za klabu kwa Wahuni.
Wahuni awatabiriki.[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Linalozungumziwa ni basi walilopewa na Sports Pesa. Hili liliuzwa na utaratibu ulitangazwa.Sio haya mapya.Aliyosema yapo matengenezo yapo na mojawapo lilitumika kuwabeba Simba Queens kwenye mechi yao huko Lindi Jumamosi iliyopita. Wacheni majungu Utopolo.
Sports pesa hawajawahi kutoa basi najua TBL ndio walitoa basi kwa simba, yanga na TFF.
 
Linalozungumziwa ni basi walilopewa na Sports Pesa. Hili liliuzwa na utaratibu ulitangazwa.Sio haya mapya.Aliyosema yapo matengenezo yapo na mojawapo lilitumika kuwabeba Simba Queens kwenye mechi yao huko Lindi Jumamosi iliyopita. Wacheni majungu Utopolo.
Kwa kuweka tu kumbukumbu sawa; zile Yutong zilinunuliwa na mdhamini wa kipindi hicho (Kilimanjaro Lager).

Sportpesa waliyapaka tu rangi na kuweka nembo yao, baada ya hizo timu mbili kumaliza mkataba wao na hiyo bia ya Kilimanjaro.
 
Duuuh kumbe bus wamejiuzia wenyewe hao viongozi wa Simba [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Ona hili hapa nimelipata [emoji116]
Fj7H1diWYAYi88t.jpg
Screenshot_20230120-223518.jpg
 
Back
Top Bottom