Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Mkuu huu mtizamo wako sipingani nao, ila ngoja tutaangalia katika comments za wachangiaji wengine ili tuone wapi panakimbiza kutokana na sifa zilizoorodheshwa hapo juu.
Yaah ila kama kuna sehemu inabeat Ilala utanijuza...kimiundombinu,kimajengo,kila kitu kipo Ilala pale
 
Yaah ila kama kuna sehemu inabeat Ilala utanijuza...kimiundombinu,kimajengo,kila kitu kipo Ilala pale
Yah nitakujuza mkuu, ila kuna mwana JF mmoja hapo juu aliandika kwamba Ilala inaongoza zaidi kibiashara, ila kwa sifa zingine hapo juu yeye kaipa Kinondoni.
 
Ishu vipi wakuu,

Wakubwa leo kuna swali linalosumbua baadhi ya watu wanaoishi katika jiji letu kubwa la Dar es salaam. Swali lenyewe linahusu wilaya zetu tano za mkoa huu wa Dar es salaam. Yani wilaya

1) Kinondoni
2) Ilala
3) Ubungo
4) Temeke
5) Kigamboni

Swali lililopo ni watu kutaka kujua kati ya hizo wilaya tano ni wilaya gani ambayo inaongoza kuwa na sifa zifuatazo hapo chini:

a) Wajanja wengi.
b) Watu wenye vipato vya juu.
c) Mijengo ya maana.
d) Maendeleo yanayoonekana kama vile barabara nzuri, hospital na shule nzuri za serikali na private.
e) Miundo mbinu mizuri na hali ya hewa safi.
f) Upatikanaji wa maji na meme.
g) Kuchangamka kibiashara.
h) Vilevile ni sehem ipi katika wilaya hizo ambayo unaiona inafaa wewe binafsi kuishi aidha kwa kupanga au kwa kujenga nyumba yako mwenyewe?

Kwa wale ambao hawazifahamu vizuri kata za wilaya hizo naomba niziorodheshe hapo chini ili kuwarahisishia watu ambao hawafahamu kata fulan ipo katika wilaya fulan nk.

Kata za wilaya ya KINONDONI ni:
Kinondoni, Bunju, Hananasif, Kawe, Wazo, Kigogo, Kijitonyama, Kunduchi, Mabwepande, Magomeni, Makongo, Makumbusho, Mbezi juu, Mbweni, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Mzimuni, Ndugumbi, Tandale.

Kata za wilaya ya ILALA ni:
Ilala, Kariakoo, Buguruni, Gerezani, Chanika, Gongo la mboto, Jangwani, Kisutu, Kipawa, Kimanga, Kinyerezi, Kitunda, Kivukoni, Kiwalani, Majohe, Mchafukoge, Mchikichini, Msongola, Pugu, Segerea, Tabata, Ukonga, Upanga mashariki, Upanga magharibi, Vingunguti.

Kata za wilaya ya UBUNGO ni:
Ubungo, Kimara, Mbezi, Goba, Kibamba, Mabibo, Kwemba, Makuburi, Makurumla, Manzese, Mburahati, Msigani, Saranga, Sinza.

Kata za wilaya ya TEMEKE ni:
Temeke, Azimio, Buza, Chamazi, Chang'ombe, Tandika, Charambe, Keko, Kibonde maji, Kiburugwa, Kijichi, Kilakala, Kulungule, Kurasini, Makangarawe, Mbagala, Mbagala kuu, Mianzini, Miburani, Mtoni, Sandali, Toangoma, Yombo vituka.

Kata za wilaya ya KIGAMBONI ni:
Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Kimbiji, Kisarawe, Pembamnazi, Somangila, Tungi, Vijibweni.

Wakuu wenye uelewa mpana na jiji letu, pamoja na wilaya zetu karibuni tuchangie ili tupate kujua wilaya ipi inayobeba hadhi nzima ya jiji letu la Dar es salaam na nchi kwa ujumla.
Kinondoni ni moto wa kuotea mbali mkuu asikudanganye mtu.
 
🤭kumbe waishio chanika,mvuti,msongola na kivule ni machizi(punguani kabisa)si eti?!!!!!
Hahaha naona yeye kazungumza kimisemo yetu ya mjini mjini mkuu, wala hakuwa na nia mbaya😀😀
 
Wilaya ni Kinondoni uende kuishi Chanika Una akili kweli wewe
Mbona rais # 2 anaishi huko

Na kuna wazito wengi tu huko

Dar kila maeneo kuna sehemu zingine ni nzuri na watu wanaishi

Hiyo kiluvya tu kuna mahali ukienda watu wamejenga tena kuko kimpangilio wamejaa mashuwa tu

Kivule pia kuna maeneo,mitaa iko vizuri tu watu wanaishi safi

Ova
 
Hapana aisee....

I wish hata angekuwa mimi....sema namfuatilia sana...jamaa yuko smart na video zake ziko poa
Ya ki ukweli jamaa video zake zinavutia sana kuangalia. Hata mimi ni mfuatiliaji wake mkubwa sana wa video zake.
 
Back
Top Bottom