Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Manispaa ipi ya Dar imeendelea zaidi?

Mbona rais # 2 anaishi huko

Na kuna wazito wengi tu huko

Dar kila maeneo kuna sehemu zingine ni nzuri na watu wanaishi

Hiyo kiluvya tu kuna mahali ukienda watu wamejenga tena kuko kimpangilio wamejaa mashuwa tu

Kivule pia kuna maeneo,mitaa iko vizuri tu watu wanaishi safi

Ova
Mkuu raisi wa 2 anaishi huko au ulitaka kumaanisha alizaliwa huko?

Maana ninachojua ana majumba yake huko ostabay ambayo ni Kinondoni. Sina uhakika kama ana mjengo huko uliposema.
 
Ishu vipi wakuu,

Wakubwa leo kuna swali linalosumbua baadhi ya watu wanaoishi katika jiji letu kubwa la Dar es salaam. Swali lenyewe linahusu wilaya zetu tano za mkoa huu wa Dar es salaam. Yani wilaya

1) Kinondoni
2) Ilala
3) Ubungo
4) Temeke
5) Kigamboni

Swali lililopo ni watu kutaka kujua kati ya hizo wilaya tano ni wilaya gani ambayo inaongoza kuwa na sifa zifuatazo hapo chini:

a) Wajanja wengi.
b) Watu wenye vipato vya juu.
c) Mijengo ya maana.
d) Maendeleo yanayoonekana kama vile barabara nzuri, hospital na shule nzuri za serikali na private.
e) Miundo mbinu mizuri na hali ya hewa safi.
f) Upatikanaji wa maji na meme.
g) Kuchangamka kibiashara.
h) Vilevile ni sehem ipi katika wilaya hizo ambayo unaiona inafaa wewe binafsi kuishi aidha kwa kupanga au kwa kujenga nyumba yako mwenyewe?

Kwa wale ambao hawazifahamu vizuri kata za wilaya hizo naomba niziorodheshe hapo chini ili kuwarahisishia watu ambao hawafahamu kata fulan ipo katika wilaya fulan nk.

Kata za wilaya ya KINONDONI ni:
Kinondoni, Bunju, Hananasif, Kawe, Wazo, Kigogo, Kijitonyama, Kunduchi, Mabwepande, Magomeni, Makongo, Makumbusho, Mbezi juu, Mbweni, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala, Mzimuni, Ndugumbi, Tandale.

Kata za wilaya ya ILALA ni:
Ilala, Kariakoo, Buguruni, Gerezani, Chanika, Gongo la mboto, Jangwani, Kisutu, Kipawa, Kimanga, Kinyerezi, Kitunda, Kivukoni, Kiwalani, Majohe, Mchafukoge, Mchikichini, Msongola, Pugu, Segerea, Tabata, Ukonga, Upanga mashariki, Upanga magharibi, Vingunguti.

Kata za wilaya ya UBUNGO ni:
Ubungo, Kimara, Mbezi, Goba, Kibamba, Mabibo, Kwemba, Makuburi, Makurumla, Manzese, Mburahati, Msigani, Saranga, Sinza.

Kata za wilaya ya TEMEKE ni:
Temeke, Azimio, Buza, Chamazi, Chang'ombe, Tandika, Charambe, Keko, Kibonde maji, Kiburugwa, Kijichi, Kilakala, Kulungule, Kurasini, Makangarawe, Mbagala, Mbagala kuu, Mianzini, Miburani, Mtoni, Sandali, Toangoma, Yombo vituka.

Kata za wilaya ya KIGAMBONI ni:
Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Kimbiji, Kisarawe, Pembamnazi, Somangila, Tungi, Vijibweni.

Wakuu wenye uelewa mpana na jiji letu, pamoja na wilaya zetu karibuni tuchangie ili tupate kujua wilaya ipi inayobeba hadhi nzima ya jiji letu la Dar es salaam na nchi kwa ujumla.
upatikanaji wa meme😂😀Ivi kwan ulikua unakimbizwa huku una type?
 
Mkuu raisi wa 2 anaishi huko au ulitaka kumaanisha alizaliwa huko?

Maana ninachojua ana majumba yake huko ostabay ambayo ni Kinondoni. Sina uhakika kama ana mjengo huko uliposema.
Ameishi huko muda tu hajawahi kukaa obay au masaki
Hata igp mstaafu anamjengo huko
Kuna matop wengi wanaishi huko

Ova
 
Ameishi huko muda tu hajawahi kukaa obay au masaki
Hata igp mstaafu anamjengo huko
Kuna matop wengi wanaishi huko

Ova
Ok nilikuwa sifahamu, hilo la IGP mstaafu nalifahamu mkuu.
 
Majengo kumi tu ya pale Posta yanaweza kua na thamani yamajengo 5000 ya kinondoni
Pspf towers,TPA Tower,Mnf Tower, pension fund Tower Benjamin mkapa....
Hayo majengo yanaweza safisha vibanda 5000 vya kinondoni
 
Majengo kumi tu ya pale Posta yanaweza kua na thamani yamajengo 5000 ya kinondoni
Pspf towers,TPA Tower,Mnf Tower, pension fund Tower Benjamin mkapa....
Hayo majengo yanaweza safisha vibanda 5000 vya kinondoni
😂😂😂
 
Back
Top Bottom