tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Sakata la mali za John Komba kupigwa mnada kufuatia deni la Tsh bilion 1.2 analodaiwa na benki ya CRDB limefikia tamati baada ya mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bw Yusuf Manji, kununua shule na baadhi ya mali zake zote ambazo zilikuwa zipigwe mnada ili kufidia deni.
Komba alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa shule zake kupigwa mnada (na kufungwa jela) ili kufidia deni hilo alilokopa CRDB miaka 5 iliyopita.
Source: Mwananchi.
MAONI YANGU
Komba amshukuru sana Manji kwa kumuokoa kwenda jela na kupigwa mnada kwa mali zake. Sipati picha kama Komba angefungwa jela kile kitambi chake angekificha wapi. Lazima kingenywea kama puto lililotoboka. Hivi alidhani kuendesha shule ni sawa na kuimba kwaya na kusimamia bendi? Chezea mkopo wewe!