Manka Chuga, ambaye amekuwa akijulikana mitandaoni kwa kuonyesha ujasiri wake wa kunywa pombe kwa kiasi kikubwa, ametangaza kuacha matumizi ya pombe na sasa anaomba msaada wa kiafya.
Kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Manka amesema "Naomba radhi kwa watanzania wote wakubwa kwa wadogo, pombe nimeacha naombeni mnichangie afya yangu haipo sawa nipate matibabu ya haraka kabla hali yangu haijawa mbaya"
Kauli hiyo imeibua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya watu wakimpongeza kwa uamuzi huo na kumtaka apewe msaada unaofaa ili kuendelea na maisha yake vizuri.