Manqoba Atoa Maagizo Mazito Yanga Dhidi ya Gaborone United

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amewataka washambuliaji na mabeki wake kuingia uwanjani wakiwa na umakini wa kiwango cha juu, akisisitiza kuwa ufanisi wa kufunga na uimara wa safu ya ulinzi ndizo zitakazokuwa silaha kuu za kuing’oa Gaborone United ya Botswana.

Mchezo huo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Kocha Manqoba akiweka wazi kuwa timu hiyo haina nafasi ya kufanya makosa ikiwa inataka kutinga hatua inayofuata.

Ufanisi Eneo la Hatari Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Shalulile pamoja na Selemani Mwalimu imepewa presha kubwa ya kuhakikisha inatumia vyema kila nafasi itakayopatikana. Mwalimu, ambaye alikuwa shujaa katika mchezo wa kwanza baada ya kufunga bao la kusawazisha nchini Botswana, anatarajiwa kuendeleza makali yake.

“Kutengeneza nafasi ni jambo moja, lakini kuzitumia ni jambo jingine la msingi zaidi. Tunahitaji kuwa na utulivu na ufanisi Mkubwa tunapofika eneo la hatari ili kumaliza mchezo mapema,” alisema Manqoba.

Nidhamu na Uimara Eneo la Ulinzi Kocha huyo raia wa Afrika Kusini hakuiacha nyuma safu yake ya ulinzi, akiwataka mabeki kucheza kwa nidhamu ya juu na kutogawa nafasi rahisi kwa washambuliaji wa Gaborone United. Ametaja kuwa uimara wa safu ya ulinzi ndio utakaotoa amani kwa timu nzima kutafuta mabao.

Kibarua cha Dimba la Chamazi Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi siku ya Jumamosi, Septemba 12, katika mchezo huo wa marudiano. Mashabiki wa Wananchi wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mbinu za Manqoba zitakavyowavusha kuelekea hatua inayofuata.
1788865651083.png
 
View attachment 3665755
Amrudishe kwanza mshikaji wake wa set pieces alimpa ulaji, timu inapata faul na kona nyingi kila mtu anajiputulia hakuna hata mchezaji special kwa mipira ya set pieces

Nmeona timu nyingi zinazofundishwa set pieces kisasa faul zikipigwa mbele ya mstari wa mabeki huku kwetu bado wanapiga faul kizaman za kwenda juu ya mstari walijipanga wachezaji🚮
 
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amewataka washambuliaji na mabeki wake kuingia uwanjani wakiwa na umakini wa kiwango cha juu, akisisitiza kuwa ufanisi wa kufunga na uimara wa safu ya ulinzi ndizo zitakazokuwa silaha kuu za kuing’oa Gaborone United ya Botswana.

Mchezo huo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Kocha Manqoba akiweka wazi kuwa timu hiyo haina nafasi ya kufanya makosa ikiwa inataka kutinga hatua inayofuata.

Ufanisi Eneo la Hatari Safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Shalulile pamoja na Selemani Mwalimu imepewa presha kubwa ya kuhakikisha inatumia vyema kila nafasi itakayopatikana. Mwalimu, ambaye alikuwa shujaa katika mchezo wa kwanza baada ya kufunga bao la kusawazisha nchini Botswana, anatarajiwa kuendeleza makali yake.

“Kutengeneza nafasi ni jambo moja, lakini kuzitumia ni jambo jingine la msingi zaidi. Tunahitaji kuwa na utulivu na ufanisi Mkubwa tunapofika eneo la hatari ili kumaliza mchezo mapema,” alisema Manqoba.

Nidhamu na Uimara Eneo la Ulinzi Kocha huyo raia wa Afrika Kusini hakuiacha nyuma safu yake ya ulinzi, akiwataka mabeki kucheza kwa nidhamu ya juu na kutogawa nafasi rahisi kwa washambuliaji wa Gaborone United. Ametaja kuwa uimara wa safu ya ulinzi ndio utakaotoa amani kwa timu nzima kutafuta mabao.

Kibarua cha Dimba la Chamazi Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi siku ya Jumamosi, Septemba 12, katika mchezo huo wa marudiano. Mashabiki wa Wananchi wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mbinu za Manqoba zitakavyowavusha kuelekea hatua inayofuata.
View attachment 3665755
yes,hizo ndio tabia za makocha wakubwa
 
Binafsi sijui!
 
Kilichotokea Gaborone kimemua nguo. Kuna mwenzake naye aliwahi kufanyiwa hivi hivi na wale Waarabu wa USM Alger kama sijakosea! Waarabu walikuwa wanajiangusha tu uwanjani kutafuta sare, huku Yanga ikihitaji ushindi ili isonge mbele.

Mwisho wa siku tule kocha alitimuliwa. Kocha bora unatakiwa uwe na mbinu mbadala za kupambana na timu zinazopaki basi na kushambulia kwa kishtukiza.
 
Vip hajatoa historia za wacheza
ji wote wa Gaborone ubutu wao, ukali wao dimbani, walikotokea, nk? Maana hicho ndo anachokiweza!!!! hakuna kocha mle wakati utaongea hamalizi msimu
 
Huyu jamaa acha ninyamaze kwa sasa kabla ya kuja na hitimisho.
 
Back
Top Bottom