Hili shirika lina matatizo sana, juzi nimeenda kufungua sanduku halifunguki nikarudi kaunta nikauliza mbona mmefunga sanduku wakati sidaiwi wakaniambia hatujafunga nikawauliza kwa nini halifunguki wakaniambia kajaribu tena nikaenda na mlinzi aliepo hapo posta halikufunguka tukarudisha jibu, wakaniambia leta funguo zote mbili ili tukubadilishie nikawaambia ninayo moja nyingine sijui ilipo maana sanduku ni la marehemu mzee wangu, chaaaa eti wakaniambia lipa elfu 20 tukupe funguo nyingine, nimewaambia sitaki hata funguo ziwe mbili waangalie walichofanya nifungue niende zangu, wananijibu lazima ulipe 20, sasa sijui ya nini?! sielewi kama wapo hapa hebu fafanueni jamani hamjionei hata huruma mlivyochoka?!