Manunuzi aliexpress posta wameniambia mpaka niwe na slp

Manunuzi aliexpress posta wameniambia mpaka niwe na slp

Hili shirika lina matatizo sana, juzi nimeenda kufungua sanduku halifunguki nikarudi kaunta nikauliza mbona mmefunga sanduku wakati sidaiwi wakaniambia hatujafunga nikawauliza kwa nini halifunguki wakaniambia kajaribu tena nikaenda na mlinzi aliepo hapo posta halikufunguka tukarudisha jibu, wakaniambia leta funguo zote mbili ili tukubadilishie nikawaambia ninayo moja nyingine sijui ilipo maana sanduku ni la marehemu mzee wangu, chaaaa eti wakaniambia lipa elfu 20 tukupe funguo nyingine, nimewaambia sitaki hata funguo ziwe mbili waangalie walichofanya nifungue niende zangu, wananijibu lazima ulipe 20, sasa sijui ya nini?! sielewi kama wapo hapa hebu fafanueni jamani hamjionei hata huruma mlivyochoka?!
 
oooh thanks kaka nitajaza tu namba ya simu? vp kuhusu posta husika? au mpaka ukifika ndo utaambiwa umefika posta fulani?
Weka jina la mji unaokaa. Mfano: Usa-river Arusha
 
care of ndo nn mkuu?
Kupitia anuani ya MTU. Kubali kupoteza mizigo yako. Unaona shida kumiliki lako kwa shs 30,000/? Mjasiriamali gani we we? Once per year. Gawa kwa 12(miezi). Sawa na she 2500/ kwa mwezi wakati umeagiza mzigo Wa USD 25.
 
Exactly. una

andika tu P.O box .....Iringa. automatically inakuja Iringa.
Ndibalema ukiandika number ya Posta isiyo yako utapoteza mzigo. Kama huna SLP tafadhali usibahatishe. Weka number ya simu then mji (Iringa). Ukikwama nenda kamuone Mzee mmoja anaitwa Lugomola kitu kama hicho. Ndiye boss hapo.
 
Kuna malipo mengine baada ya mzigo kufika? Au ni ukishanunua ndio umemaliza.
 
m
Samahani naomba niulize, hivi aliexpress ushawahi order na wao ukapata mzigo? nilitaka niwatumie lakini nikawa na wasiwasi. TIA
Mimi huwa natumia Aliexpress ila mpaka mzigo ufike kama ni wa umuhimu utakesha especially ukiwa unatumia free shipment ni kama 30-60 days
 
Kuna malipo mengine baada ya mzigo kufika? Au ni ukishanunua ndio umemaliza.
Kama ni kamzigo kadogo utapokea dirishani mimi huwa nalipia shiling 1000 ila kama mzigo ni mkubwa hapo ndo unapokutana na mafisi wa T.R.A watakupgia charges za hatari
 
Kama ni kamzigo kadogo utapokea dirishani mimi huwa nalipia shiling 1000 ila kama mzigo ni mkubwa hapo ndo unapokutana na mafisi wa T.R.A watakupgia charges za hatari

Napenda sana kuagiza mizigo nje ila sijui njia naomba unifahamishe
 
Mimi naorder sana vitu nimepokea vyote kama order 20 tofauti kasoro kimoja kimepotelea njiani (kipindi cha December kuna vurugu sana kwa sababu ya holiday shopping), unaweza ukaweka dispute kama haujapata na hatimaye utarudishiwa hela. Sina uhakika kama unaweza kutumiwa kitu bila SLP.
Nimeagiza kuanzia laptop ya $200 mpaka HDMI cable za $2.

Kuibiwa aliexpress sio rahisi maana hela inashikiliwa na aliexpress wenyewe na hiendi kwa mwuzaji mpaka wote mkubali kuwa kitu kimefika, pia angalia rating ya mwuzaji na review za wanunuzi wengine.

Nisaidie nifanyeje ili niweze kununua online maana kuna vitu nimetafuta sana madukani nimekosa ila naviona ebay nawezaje kununua ? Naomba msaada
 
Kama ni kamzigo kadogo utapokea dirishani mimi huwa nalipia shiling 1000 ila kama mzigo ni mkubwa hapo ndo unapokutana na mafisi wa T.R.A watakupgia charges za hatari
Mzigo mkubwa ndo unakuaje mkuu. Je kwa mfano laptop au simu vinalipiwa kodi ?
 
Napenda sana kuagiza mizigo nje ila sijui njia naomba unifahamishe
Kwanza kabisa inabidi upate card iliyowezeshwa kufanya malipo mtandaoni, mfano mimi nilipata card yangu Banc ABC ni process ya masaa machache sana

  • Nenda bank ya ABC ukiwa na kitambulisho chako waambie unahitaji card kwa ajili ya malipo ya mtandaon na gharama za card hiyo sh 15000 za watakupatia nawe utakuwa tayar kuanza kufanya manunuzi.
  • Nenda kajiunge na mtandao unaouza vitu kama ebay, Amazon, Aliexpress ila katika hyo mitandao inatofautiana njia za ulipaji yaani ipo inayotaka ufanye malipo yako kupitia paypal na ipo unayofanya malipo kupitia direct your card hapa sasa itategemeana na wewe unataka kununua kitu wapi kama unataka kununua kitu kutoka Ebay lazima uwe na paypal ila kama unataka kununua kitu Aliexpress huitaji paypal
uzuri wa paypal ni kwamba unakuwa na uhakika na usalama wa pesa zako kulinganisha na kutumia card yako direct kufanya malipo amabapo unaweza kutana na wezi wa mtandaoni wakaiba taarifa za cad yako kwa kitu tunachokiita phishing.

mpaka ukifikia hapo utakuwa ushafanikisha hatua kubwa sana na iliyobaki ni kidogo sana
 
Mzigo mkubwa ndo unakuaje mkuu. Je kwa mfano laptop au simu vinalipiwa kodi ?
Sina experince na vitu kama simu na laptop ila kuna ndugu niliwahi tu kuagiza nguo kama 8 hivi nkaishia kudaiwa kodi karibia 20000 sasa sijui kwa vitu kama hivo ila kuna uzi mmoja wa Mwl CRT alieleza vizur sana jaribu kuutafuta
 
Kuwa makini na aliexpress matapeli wengi, mizigo kuchelewa, kuibiwa ela kwenye akaunti.. Secured online purchase na uhakika wa kufika mizigo kwa haraka utapata ebay na amazon..
1492152429885.jpg
1492152444115.jpg
 
hiy
Kuwa makini na aliexpress matapeli wengi, mizigo kuchelewa, kuibiwa ela kwenye akaunti.. Secured online purchase na uhakika wa kufika mizigo kwa haraka utapata ebay na amazon..
View attachment 496163 View attachment 496164
hyo ni kweli kabisa mkuu ila mimi huwa nanunua vitu vidogo sana ambavo siwezi umia kichwa hata posta hawawezi hangaika kupata tamaa
 
Attachments

  • Screenshot (55).png
    Screenshot (55).png
    37.7 KB · Views: 74
Sina experince na vitu kama simu na laptop ila kuna ndugu niliwahi tu kuagiza nguo kama 8 hivi nkaishia kudaiwa kodi karibia 20000 sasa sijui kwa vitu kama hivo ila kuna uzi mmoja wa Mwl CRT alieleza vizur sana jaribu kuutafuta
Asante kwa maelezo
 
Vipi gauni ni 2.5$ na shipping cost 6.23$. Je hii inamaana kuwa gauni hadi lifike Tz gharama Itakuwa ni 8.73$ ? Pia na TRA Je? Gharama si kubwa. Em nisaidie nijue cz nataka nifanye biashara, nimechoka kutegemea mshahara.
 
unaona kama hyo hapo ni receipt ya T.R.A ya mwaka huu na hapo mzigo ulikuwa n blouse kama 8 hivi kila moja 2$ na shipping 1$ na nlipewa discount ya 2$ so total mzigo gharama ilikuwa ni 22$
 
Attachments

  • Tra.jpg
    Tra.jpg
    206.3 KB · Views: 71
Back
Top Bottom