Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Sugu fighter kitambo
Salute sana kwake

Ova
 
Leo hii huko Mbeya Mjini kulikuwa na ziara ya manunuzi ya nyanya na mishikaki iliyofanywa na Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo bilionea Joseph Mbilinyi ambaye pia anafahamika kama Sugu au RealJ ongwe kama anavyofahamika siku hizi, ama waweza kumtambua kama mfungwa wa kisiasa.

Kama masihara tu akaibuka kwenye soko la Igawilo ambako alienda kununua nyanya na vitunguu, yaani viungo mbalimbali zikiwemo karoti na pilipili hoho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake, na baadaye wadau wakampeleka hadi eneo la kuchomea mishikaki, ili waitafune kidogo.

Basi bwana kufumba na kufumbua akajikuta amezungukwa na umati ambao haufahamiki ulikotokea! Hakika huyu jamaa anapendwa Mbeya Mjini! Kwa kifupi ni kwamba shughuli za soko ni kama zilisitishwa kwa muda kupisha Sugu anunue nyanya! Yaani ilifika wakati tukahofia kwamba huenda polisi wangevurumisha mabomu ya machozi, maana umati wake unazidi ule wa mechi ya Yanga dhidi Al Hilal ya Sudan kwa Mkapa.

Kwenye Hili nimejifunza jambo moja kubwa sana, kwamba usishindane na aliyejaaliwa, utadhalilika sana. Wazaramo wana msemo mmoja kwamba, "Acholile kachora".
Uzi bila picha ni batili
 
Baada ya kupita kimya kirefu takribani miaka miwili siku ya jana aliyewahi kuwa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi Maarufu kama Sugu, alionekana mitaani huku akishangiliwa kwa nguvu sana na Vijana.

Hii ni picha inayoashiria kuwa amerejea kwenye kutafuta jimbo ambalo kwasasa linashikiliwa na Tulia Ackson Spika wa bunge la JMT.

Wananchi mbalimbali wa Mbeya wametoa maoni yao kuwa Sugu akiamua kugombea tena Mwaka 2025 ataibuka na ushindi wa kishindo.

Huu ndiyo muda wa Siasa tunazozipenda.

Welcome back Sugu.
Kwani Tulia alishinda? Au alipewa na mwendazake?
 
Picha ipo wapi mzee baba...
 
Tulia alipewa tu hilo jimbo na yule jamaa yenu. Hakushinda kwa kura.
Sio kweli mkuu tulia aliweza kujenga Imani ya wana mbeya na alishinda ila awami ya 6 wameua Imani yote ya wana mbeya kwa ccm hivyo sugu atashinda tena kama akigombea wanambeya waje kuniprove wrong usiongee kishabiki
 
Back
Top Bottom