Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Duh kwa nafsi yako kabisa unaamini tulia alishinda Ubunge halali Mbeya...?

Mungu hadhihakiwi....
Anayetangazwa mshindi, ndie mshindi!. The end justifies the means!. Kwenye the African democracy, ushindi does not depends on the vote cast, but the vote count!. Hivyo kama Dr. Tulia ameshinda kwa vote count akiwa just Naibu Spika!, akiwa Spika atapita bila kupingwa!.
P
 
mtafutieni Jimbo lingine , vinginevyo mtapoteza spika wenu
Kiukweli wengi humu ni very short sighted, wengine ni myopia!. Samia aliposema 2025 tunataka kusimamisha mgombea mwanamke, jee mnamjua ni nani?.
Open your eyes!.
P
 
Brother unampigia mbuzi gitaa huyo jamaa kanywa maji ya bendera hasikii wala hambiwi.
Huna lolote wewe , subiri posho tu , mtu ambaye hata chama chenyewe hakijui anawezaje kuwa na sauti ? ataburuzwa tu na akina Pinda , angalia timu iliyorudi madarakani baada ya yeye kuapishwa
 
Huna lolote wewe , subiri posho tu , mtu ambaye hata chama chenyewe hakijui anawezaje kuwa na sauti ? ataburuzwa tu na akina Pinda , angalia timu iliyorudi madarakani baada ya yeye kuapishwa
Unatembea na kiwiliwili tu kichwa umewapa hao wa puuzi wenzio, wamekugeuza sigara kali wana kuwasha mbele na nyuma kwa maana wewe mwenyewe hujuelewi kama sigara kali.
 
Leo hii huko Mbeya Mjini kulikuwa na ziara ya manunuzi ya nyanya na mishikaki iliyofanywa na Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo bilionea Joseph Mbilinyi ambaye pia anafahamika kama Sugu au RealJ ongwe kama anavyofahamika siku hizi, ama waweza kumtambua kama mfungwa wa kisiasa.

Kama masihara tu akaibuka kwenye soko la Igawilo ambako alienda kununua nyanya na vitunguu, yaani viungo mbalimbali zikiwemo karoti na pilipili hoho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake, na baadaye wadau wakampeleka hadi eneo la kuchomea mishikaki, ili waitafune kidogo.

Basi bwana kufumba na kufumbua akajikuta amezungukwa na umati ambao haufahamiki ulikotokea! Hakika huyu jamaa anapendwa Mbeya Mjini! Kwa kifupi ni kwamba shughuli za soko ni kama zilisitishwa kwa muda kupisha Sugu anunue nyanya! Yaani ilifika wakati tukahofia kwamba huenda polisi wangevurumisha mabomu ya machozi, maana umati wake unazidi ule wa mechi ya Yanga dhidi Al Hilal ya Sudan kwa Mkapa.

Kwenye Hili nimejifunza jambo moja kubwa sana, kwamba usishindane na aliyejaaliwa, utadhalilika sana. Wazaramo wana msemo mmoja kwamba, "Acholile kachora".
View attachment 2395663
View attachment 2395664
View attachment 2395665
View attachment 2395668

Siku wakiruhusu siasa itakuwa raha Sana. Huku Wenje, kule mnyika, kushoto Sugu, kulia Madam Ruge, kule pambalu, huku Mwaioaya, pale malisa, hapa Heche na Salum Mwalimu. Long live CHADEMA my only party since I was born.
 
Haaaaaaaaah nimecheka sana Huyu Sugu ambaye habari yake imeisha Mbeya
 
Watu wako busy na maisha,, siku hizi, anyway weka video tuone
Walimpokea kwa shangwe wakijua atanunua vitu kibao kumbe fix tu

Mtu yeyote ukienda hilo soko na kule kwa wauza Michele barabarani wanakupokea kama mfalme Wakitarajia biashara zao zimepata mtu watauza!! Alienda kuuza sura sokoni.Sokoni sio sehemu ya kuuza sura ni kwenda kununua.Kawapotezea muda wao kwawaacha na njaa zao mauzo sifuri

Yeye yuko tu anawapita kwenda kununua vimishkaki vya elfu 20
 
Back
Top Bottom