Manunuzi ya umeme wa Ethiopia ni wizi tusiwe wajinga!

Hii michezo ya Tanesco inajulikana toka zama za Msoga empire. Kulikuwa na IPTL na Richmond walichokuwa wanafanya sote tunakijuašŸ˜‚!

Kikubwa ni mtu anatafutiwa ulaji tu humo. Hio Arusha na moshi walikuwa wanatumia nini siku zote kabla ya tamko hilo? Au Makonda alikuwa analala gizani na raia wake?

Tu hakikishiwe ile kampuni aliyepo mtoto wa Mama Samia Abdul ya umeme haipo kwenye tender yeyote kuanzia huko Kenya
 
kwamba umeme uliopo hapa tanganyika hautoshi au?
basi si bora yale majenereta ya kigoma myapeleke huko kaskazini kuongeza nguvu.kuliko kununua umeme.hyo ni dharau
Bwawa lile sio lenu tena jiandae kisaikolojia, sio mpaka mvujishiwe kila taarifa zilivyo kwa lazima utafutwe mbadala ndio huo tununue umeme Ethiopia huu wa Rufiji sio wa kwetu
 
Shida ya kuchukua hoja juuu bila kufikiria,,,unafikiri eti umeme utatoka moja kwa moja Ethiopia ndo uje Tanzania,,,jua kwamba Ethiopia wanawauzia umeme Kenya,,hivyo umeme utachukuliwa Kenya mpkani na kuingizwa Tanzania
wanakurupuka na story zao za vijiweni
 
Tu hakikishiwe ile kampuni aliyepo mtoto wa Mama Samia Abdul ya umeme haipo kwenye tender yeyote kuanzia huko Kenya
Kama yule dogo ana kampuni inayohusu mambo ya umeme hayo baaaassss tumekwishaaa!
 
Bwawa lile sio lenu tena jiandae kisaikolojia, sio mpaka mvujishiwe kila taarifa zilivyo kwa lazima utafutwe mbadala ndio huo tununue umeme Ethiopia huu wa Rufiji sio wa kwetu
Bwawa sio letu kivipi jamani? Si lipo ndani ya mipaka yetu!?
 
Nilishasema kuhusu umeme tangu 2021

Bwawa sio letu kivipi jamani? Si lipo ndani ya mipaka yetu!?
Sio kila kilichopo mikononi mwenu ni chenu, hata ardhi ipo kubwa sana ila sio yenu huwezi ukainuka ukavamia tu ardhi huko Songwe ukaanza kulima ukaulizwa unasema yetu yenu na nani sasa wenye ardhi wakija ndio utajua hapo utaelewa kwanini kila unachosema chenu sio chenu ni chao, chetu yetu haipo hio
 
Hii nchi inahitaji sana kuwa reformed sio kiuchaguzi tu hata kimgawanyo wa rasilimali. Haiwezekani bwawa limejengwa na matangazo kibao halafu mseme sio letu. Ndio maana Mwendazake aliwavuruga vuruga wawekezaji wahuni bora kulipa fidia kuliko kushikilia mikataba ya kinyonyaji
 
Ndio ishakua hivyo tena hapo hakuna lingine la kufanya zaidi ya kununua umeme nje wakati rasilimali mnayo mnaiuza nyinyi mnabakia kutangatanga poor leadership skills
 
Shida ya kuchukua hoja juuu bila kufikiria,,,unafikiri eti umeme utatoka moja kwa moja Ethiopia ndo uje Tanzania,,,jua kwamba Ethiopia wanawauzia umeme Kenya,,hivyo umeme utachukuliwa Kenya mpkani na kuingizwa Tanzania
Hamna maana hata hivyo kuna haja gani sasa ya Stiglers?kama bado tunategemea kununua umeme?
 
Hii nchi inahitaji sana kuwa reformed sio kiuchaguzi tu hata kimgawanyo wa rasilimali. Haiwezekani bwawa limejengwa na matangazo kibao halafu mseme sio letu. Ndio maana Mwendazake aliwavuruga vuruga wawekezaji wahuni bora kulipa fidia kuliko kushikilia mikataba ya kinyonyaji
Sio letu vipi wakati ndio kauli mbio ya wale mabawana wa mitano tena
 
Shida ya kuchukua hoja juuu bila kufikiria,,,unafikiri eti umeme utatoka moja kwa moja Ethiopia ndo uje Tanzania,,,jua kwamba Ethiopia wanawauzia umeme Kenya,,hivyo umeme utachukuliwa Kenya mpkani na kuingizwa Tanzania
Mkulima analima mahindi. Baada ya kuvuna, anapata uvivu wa kupeleka mashineni yasagwe na kupata unga wa kula kwa kuona kwamba ni gharama kuyaosha na kuyaanika juani na baadae kuyasaga.

Anaamua kuyauza na kisha kwenda dukani kwa mangi kununua sembe.

Nauliza, umeme uliokuwa unapelekwa mikoa ya kaskazini, baada ya serikali kuamua kununua mwingine kutoka nje..

Umeme huo utapelekwa wapi?
Au ndio utakao uzwa nje na serikali hiihii?
Au tutalazimika kuzima mitambo kwakuwa tutakuwa na ziada ambayo haitumiki kokote?

Swali la mwisho. Kuna umeme wa ziada kwanini watanzania bado wanagharimikia umeme huo kwa bei ambayo uwezekano wa kupungua ungekuwepo lakini bado hamtaki kupunguza gharama?
By ChoiceVariable
 
Majizi ya Ccm ni majitu yasiyo na aibu hata kidogo
 
Back
Top Bottom