Manusura pekee wa Air India aongea kwa mara ya kwanza

Ajali ya ndege ya Air India imetufundisha masomo mengi ya maisha yenye nguvu.

Kwanza, kulikuwa na familia iliyokuwa imepanga kuhamia Uingereza. Ndoto hiyo ilipangwa kutimia miaka sita iliyopita, lakini kutokana na kucheleweshwa na kuweka mambo mengine mbele, iliendelea kuahirishwa.

Hili linatukumbusha kwamba mara nyingi tunabeba majukumu na ndoto nyingi kwa ajili ya baadaye — lakini haijalishi ni kiasi gani tumepanga, wakati wetu ukifika, kila kitu kinapoteza maana.

“Tunabeba vitu vingi kila siku kwa ajili ya baadaye, lakini wakati wako ukifika, hakuna kitakachojali tena.”

Pili, kulikuwa na mwanamke ambaye alipaswa kuwa kwenye ndege hiyo. Alifika amechelewa na alisisitiza kuruhusiwa kupanda, lakini hakuruhusiwa. Alivunjika moyo sana mwanzoni — hadi aliposikia kuhusu ajali hiyo.

“Wakati mwingine, kile tunachokitaka si kile kilicho bora kwetu, na kile tusichokitaka ndicho hasa tunachohitaji. Haikuwa wakati wake. MwenyezMungu alimwokoa kweli.”

Tatu, kulikuwa na mwanaume aliyenusurika. Alitupwa nje kwa sababu ndege ilipasuka mara mbili — na kwa miujiza, alinusurika.

Kwa kifupi, haikuwa wakati wake.

Hivyo, maadamu uko hai, una afya, na bado unapumua — usisubiri kesho ili utafute furaha,
fanya sasa.

Maadamu bado una muda
.View attachment 3369142
Mimi nina ushuhuda wangu mkuu..car crash hii June 3..gari ilipinduka 3 times.

Nimetoka na kovu dogo sana mkononi.
Source ya ajali ni boda mbili zilizobeba watu sita.Kwenye kona kali yenye mtelemko,walijiachia plus njia ya vumbi.

Hili swala naliota kila siku..sijui nitaponaje.
 
Attachments

  • Screenshot_20250616_084050_Google.jpg
    Screenshot_20250616_084050_Google.jpg
    123.6 KB · Views: 17
Mkuu Mshana Jr . Hili la kuruka wataalam wengi walishalikataa tangu uvumi ulipotoka. Hata mimi halikuniingia kwenye akili. Asingepona. Ukweli ni kwamba ''he was just at the correct place at the wrong time''. Unajua ajali inapotokea hata mhusika wa ajali anaweza kupata kiwewe na kujikuta anazungumza mambo ambayo hayakutokea. Pia wasikilizaji wanaweza ku-interpret kivingine mambo anayosema.
Huo ndo ukweli, yule jamaa hata haelewi anachokisema. Amenusurika mwili ila akili haijanusurika, na the more anahojiwa ndivyo anatoka taarifa zisizoeleweka. Sidhani kama utapata taarifa sahihi kutoka kwake.
 
Kitu kimoja kwa hakika alijikuta yuko nje
 
Kinadharia, nadhani baada ya ndege kujibamiza, eneo lake yeye na kiti alichokalia lilirushwa na msukumo kama kipande kilichovunjika, kabla ya ndege kulipuka akaangukia kwa pembeni mbali kiasi, akikingwa na kiti chake hicho na kuchubuka kiasi, akafungua mkanda na kuondoka(jambo pekee analolikumbuka) , hivyo kulipuka kwa ndege hakukuathiri haraka eneo alikorushwa... Hiyo ndiyo ponapona yake na si kwa umahiri wake wa kucheza filamu za kihindi.

Kila kitu kilifanyika ndani ya sekunde chache kwa kasi kubwa ambayo akili haiwezi kunakili kinachofanyika.
 
Ajali ya ndege ya Air India imetufundisha masomo mengi ya maisha yenye nguvu.

Kwanza, kulikuwa na familia iliyokuwa imepanga kuhamia Uingereza. Ndoto hiyo ilipangwa kutimia miaka sita iliyopita, lakini kutokana na kucheleweshwa na kuweka mambo mengine mbele, iliendelea kuahirishwa.

Hili linatukumbusha kwamba mara nyingi tunabeba majukumu na ndoto nyingi kwa ajili ya baadaye — lakini haijalishi ni kiasi gani tumepanga, wakati wetu ukifika, kila kitu kinapoteza maana.

“Tunabeba vitu vingi kila siku kwa ajili ya baadaye, lakini wakati wako ukifika, hakuna kitakachojali tena.”

Pili, kulikuwa na mwanamke ambaye alipaswa kuwa kwenye ndege hiyo. Alifika amechelewa na alisisitiza kuruhusiwa kupanda, lakini hakuruhusiwa. Alivunjika moyo sana mwanzoni — hadi aliposikia kuhusu ajali hiyo.

“Wakati mwingine, kile tunachokitaka si kile kilicho bora kwetu, na kile tusichokitaka ndicho hasa tunachohitaji. Haikuwa wakati wake. MwenyezMungu alimwokoa kweli.”

Tatu, kulikuwa na mwanaume aliyenusurika. Alitupwa nje kwa sababu ndege ilipasuka mara mbili — na kwa miujiza, alinusurika.

Kwa kifupi, haikuwa wakati wake.

Hivyo, maadamu uko hai, una afya, na bado unapumua — usisubiri kesho ili utafute furaha,
fanya sasa.

Maadamu bado una muda
.View attachment 3369142
Imetokea lini hii
 
Back
Top Bottom