Manyanyaso na chuki kazini zimepelekea kuugua ugonjwa wa figo

MCHIMWA

Member
Joined
Apr 21, 2024
Posts
18
Reaction score
38
Habari zenu watanzania wenzangu popote mlipo, mimi nikiwa member hai wa forum napenda kutoa ushuhuda wa manyanyaso kazini yalivyopelekea kuangukia kwenye ugonjwa sugu wa figo.

Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani serikalini, nimeajiliwa 2007, katika kupata kwangu ajila sikuwahi kufikilia kwamba makazini kuna chuki na manyanyaso yanayotokana na ukabila na muonekano wa mtu,ushirikina na maslai binafsi ya mtu.

Katika maisha yangu ya kuajiliwa sikuwahi kupata furaha ya kazi hii ninayoifanya tofauti na siku ninayopokea mshahara, kazi hii niifanyayo ni kazi ambayo kama mwanao ataajiliwa huku na hukumjengea misingi halali ya upatikanaji wa pesa ni vyema umuambie ajiendeleze kielimu angalau anaweza kupata nafuu.

Mimi baada ya kuajiliwa nikapangiwa huko mikoa ya kanda ya ziwa nikaanza kazi kwa kukaribishwa na manyanyaso ya kikabila, hapa ndipo nikaanza kupata joto la kazi yangu, ebu fikilia kuna kazi ya malipo mazuri ya pesa mezani alafu wewe upo hapo na umeiomba au unaitaji lakini mtu kwa mamlaka yake na kwa kutumia ukabila anampa mtu mwingine ambaye ni kabila lake ambaye anatafutwa akiwa hajui hili wala lile.

Sasa mambo kama haya yamenitokea zaidi ya mara Mia moja na katika nyakati hizo zote moyo wangu ulikuwa unaumia nikiwaza kwa maumivu makali ya moyo kwamba kwanini mimi nanyanyasika hivi, sababu ni muonekano wangu au kabila langu au elimu yangu au nimelogwa, lakini mwisho majibu yakaja kuwa ni ukabila na ushirikina .

Kwa kuwa sikuwa mtu wa kujiongeza niliishi maisha ya dizaini hii kwa miaka mingi huku nikiamini kuwa ni mambo yatakayoisha tu baada ya muda flani,lakini imekuwa ni endelevu mpaka hatma ya mwisho ya mates ya moyo yalipojitokeza.

Nikiwa sifahamu kwa undani elimu ya maradhi ya moyo ambayo kiuhalisia wakati naumia kwa manyanyaso niliyokuwa nayapata nikweli wakati nawaza moyo ulikuwa unaumia sana kwa kusikia kabisa yale maumivu.

Hatma ya yote .mwaka 2024 mwezi wa 4 nikiwa kazini kwangu nikapata habari njema kutoka kwa rafiki yangu kwamba kuna kazi ya pesa ipo nisiondoke, mimi nikakubaliana naye na nikawa naisubilia mpaka jua lilipozama, kitu kilichonitokea usiku ule ni funzo kwa wanangu na wale wote wanaotegemea kupata kwa visivyo halali.

Mimi nilisubiri sana lakini kilichonishangaza ni kuona watu ambao wahusika wa mchongo wakitawanyika mmoja mmoja, mimi nikaona kwamba huu ndio muendelezo wa yaleyale ambayo nayakataa na baada ya kuona hali ile mimi nikaamua kuondoka kurudi nyumbani.

Nikiwa nyumbani nikapigiwa simu na yule aliyenipa ule mchongo kwamba rudi halaka, nikapanda gari nikarudi niliporudi katika kuakikisha kazi ninayotaka kuifanya nikawa najaribu kuwauliza baadhi ya wahusika lakini sikupewa ushirikiano wowote, kilichoniuma zaidi ni baada ya kusikia mtu wangu wa karibu ambaye alinidokeza ishu iyo kwamba wenzake wamechukizwa na kitendo cha kunishirikisha mimi ivyo hata yeye hawezi kuhusishwa tena.

Mimi baada ya kusikia kauli iyo nikaondoka nikiwa na hasira na maumivu makali ya moyo, kwa kuwa usiku mnene ulishaingia sikwenda tena nyumbani, badala yake nikaenda kwa mwanamke fulani ambaye mimi nilikuwa na mahusiano naye lakini nilikuwa nashiriki naye kwa tahadhari na kwa kutumia condom.

Usiku ule nilikwenda kulala kwake na nilishiriki naye bila condom kitu ambacho sio kawaida yangu, nilifanya kama sehemu ya faraja yangu lakini niliishia kwenye stress kubwa ya nadharia ya kuambukizwa ukimwi, baada ya siku iyo ikaja kwamba kabla ya masaa 72 niwe nimempima na nimepima HIV.

Siku iliyofuata nikafanya vipimo mwenyewe na yeye majibu ni NEG, shida ikaja kwamba asubuhi yake nikaenda kuvicheki kama vimebaki kama vilivyo nikakuta kwake inaonyesha mistari mitatu mimi ni uleule mmoja, hapa nilikuwa sina uelewa wa vipimo.

Nilikuwa najitaidi kabla ya masaa 72 niwe nimejua kila kitu, baada ya majibu kuwa vile nikamshirikisha nesi fulani kwa kumtumia picha za vipimo vingine ambavyo tulipima naye usiku wa siku ile ya pili, nesi akasema mbona kama naona mstali kwa mbali hebu njoo na mwenzio, nikamjulisha ila alikuwa mbali ivyo nikaenda mwenyewe tu na kunishauri kwa kuwa muda unaisha ni bora nianzishe tu dawa ile ya ndani ya masaa 72, nikachukua na kukinywa bila kula licha ya kushauriwa lazima niwe nimekula.

Nikiwa na stress ya juu na mapigo ya moyo ya juu nikiwa nimekunywa kidonge ,yule dada akaja nanikamuelekeza aende hospitality akapimwe na alivyokwenda na kupimwa akakutwa hana maambukizi.

Siku mbili baadaye tumbo likaanza kuniuma bila kuharisha ila choo nilikuwa napata kwa shida,sometimes nilikuwa nikienda aja kubwa natoa uteute kama kamasi nyeupe na mkojo nilikuwa nakojoa mara kwa mara, nikanywa dawa mbalimbali nikidhani ni amiba,nikaenda kupima magonjwa yote lakini hakuna kilicholeta unafuu.

Baada ya mwezi nikaanza kukosa usingizi nikama napata mawenge,kukooa wakati nimelala, na maumivu ya kichwa baadaye nikaona miguu inavimba hapo nikaona naitaji kwenda hospitality kubwa,nikaenda na kupimwa na kuelezwa figo zangu hazifanyi kazi kwa ufanisi kwa kuwa damu inaonyesha sumu zipo 130 kwa viwango vyao wenyewe wanajua nikashauriwa nifuate mtindo bora wa kura itanisaidia kupunguza uwezekano wa muendelezo wa ugonjwa.

Sasa katika hali hii niliyonayo ninaamini kwamba kama ningelikuwa na kazi nyingine mfano:UALIMU.nisingepata ugonjwa huu kutokana na nature ya kazi hiyo inatoa nafasi kubwa ya muajiliwa kuwa huru na kufanya shughuli zako nyingine.

Lakini pia napenda kuhitimisha kuwa makazini tupendane hata kinafiki kuna wengi wanapata maradhi kutokana na tabia za viongozi au wafanyakazi wenzako mimi ni mfano wa wahanga waliadhiriwa na ukabila,ukanda,chuki na mambo mengine kazini hasa ukiwa mpole na husiye na makuu na husiye na muonekano wa kuwafuraisha wengine.

Asanteni.
 
Pole mno Ila nachojua upendo ni illusion yaani ni nadharia and doesn't exist, anayebisha abishe tuone, hakuna cha upendo wa mzazi ama mtt kwa mzazi yaani what's being done is just exchanging of values aka trading if no values then you become nothing,hata inzi wenyewe Kama huna kidonda ama jalala kwako wanasepa Sasa unadhani binadamu yeye ni nani
 
Mwanzo nilijua wewe ni ke. Kwa kifupi tu mkuu huna maamzi ya kiume kama umeajiliwa 2007 hadi sasa na upo kwenye dimbwi la mateso namna hiyo basi una matatizo kwenye kichwa chako.

Samahani sana kwa lugha ngumu.Lakini amini ya kuwa uliajiliwa kwa sbabu una afya njema bila kuwa na afya njema usingeajiliwa sasa kwanini ung'ang'anie hiyo ajira?

Uwezekano wa kuhama au kuacha kazi hiyo haupo au utanyongwa? Sisi tunafanya kazi ambazo wala hatujazisomea na pia huo ubaguzi upo popote tu japo kuna baadhi ya makabila umekithiri.

Hapa nilipo kuanzia super,formen na supervisor ni kabila moja tena super na formen ni mtu na mdogo wake tumbo moja baba mmoja!!

Ukija huku chini sasa wamejazana watoto wa dada zao nk yaani wakina mwamposa wapo kibaoo

Ushauri ni mmoja afya yako ni bora sana kuliko hako ka mshahara kako.
Afya yako ndio mtaji wako fanya maamzi
 
images.png
 
Habari zenu watanzania wenzangu popote mlipo, mimi nikiwa member hai wa forum napenda kutoa ushuhuda wa manyanyaso kazini yalivyopelekea kuangukia kwenye ugonjwa sugu wa figo.

Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani serikalini, nimeajiliwa 2007, katika kupata kwangu ajila sikuwahi kufikilia kwamba makazini kuna chuki na manyanyaso yanayotokana na ukabila na muonekano wa mtu,ushirikina na maslai binafsi ya mtu.

Katika maisha yangu ya kuajiliwa sikuwahi kupata furaha ya kazi hii ninayoifanya tofauti na siku ninayopokea mshahara, kazi hii niifanyayo ni kazi ambayo kama mwanao ataajiliwa huku na hukumjengea misingi halali ya upatikanaji wa pesa ni vyema umuambie ajiendeleze kielimu angalau anaweza kupata nafuu.

Mimi baada ya kuajiliwa nikapangiwa huko mikoa ya kanda ya ziwa nikaanza kazi kwa kukaribishwa na manyanyaso ya kikabila, hapa ndipo nikaanza kupata joto la kazi yangu, ebu fikilia kuna kazi ya malipo mazuri ya pesa mezani alafu wewe upo hapo na umeiomba au unaitaji lakini mtu kwa mamlaka yake na kwa kutumia ukabila anampa mtu mwingine ambaye ni kabila lake ambaye anatafutwa akiwa hajui hili wala lile.

Sasa mambo kama haya yamenitokea zaidi ya mara Mia moja na katika nyakati hizo zote moyo wangu ulikuwa unaumia nikiwaza kwa maumivu makali ya moyo kwamba kwanini mimi nanyanyasika hivi, sababu ni muonekano wangu au kabila langu au elimu yangu au nimelogwa, lakini mwisho majibu yakaja kuwa ni ukabila na ushirikina .

Kwa kuwa sikuwa mtu wa kujiongeza niliishi maisha ya dizaini hii kwa miaka mingi huku nikiamini kuwa ni mambo yatakayoisha tu baada ya muda flani,lakini imekuwa ni endelevu mpaka hatma ya mwisho ya mates ya moyo yalipojitokeza.

Nikiwa sifahamu kwa undani elimu ya maradhi ya moyo ambayo kiuhalisia wakati naumia kwa manyanyaso niliyokuwa nayapata nikweli wakati nawaza moyo ulikuwa unaumia sana kwa kusikia kabisa yale maumivu.

Hatma ya yote .mwaka 2024 mwezi wa 4 nikiwa kazini kwangu nikapata habari njema kutoka kwa rafiki yangu kwamba kuna kazi ya pesa ipo nisiondoke, mimi nikakubaliana naye na nikawa naisubilia mpaka jua lilipozama, kitu kilichonitokea usiku ule ni funzo kwa wanangu na wale wote wanaotegemea kupata kwa visivyo halali.

Mimi nilisubiri sana lakini kilichonishangaza ni kuona watu ambao wahusika wa mchongo wakitawanyika mmoja mmoja, mimi nikaona kwamba huu ndio muendelezo wa yaleyale ambayo nayakataa na baada ya kuona hali ile mimi nikaamua kuondoka kurudi nyumbani.

Nikiwa nyumbani nikapigiwa simu na yule aliyenipa ule mchongo kwamba rudi halaka, nikapanda gari nikarudi niliporudi katika kuakikisha kazi ninayotaka kuifanya nikawa najaribu kuwauliza baadhi ya wahusika lakini sikupewa ushirikiano wowote, kilichoniuma zaidi ni baada ya kusikia mtu wangu wa karibu ambaye alinidokeza ishu iyo kwamba wenzake wamechukizwa na kitendo cha kunishirikisha mimi ivyo hata yeye hawezi kuhusishwa tena.

Mimi baada ya kusikia kauli iyo nikaondoka nikiwa na hasira na maumivu makali ya moyo, kwa kuwa usiku mnene ulishaingia sikwenda tena nyumbani, badala yake nikaenda kwa mwanamke fulani ambaye mimi nilikuwa na mahusiano naye lakini nilikuwa nashiriki naye kwa tahadhari na kwa kutumia condom.

Usiku ule nilikwenda kulala kwake na nilishiriki naye bila condom kitu ambacho sio kawaida yangu, nilifanya kama sehemu ya faraja yangu lakini niliishia kwenye stress kubwa ya nadharia ya kuambukizwa ukimwi, baada ya siku iyo ikaja kwamba kabla ya masaa 72 niwe nimempima na nimepima HIV.

Siku iliyofuata nikafanya vipimo mwenyewe na yeye majibu ni NEG, shida ikaja kwamba asubuhi yake nikaenda kuvicheki kama vimebaki kama vilivyo nikakuta kwake inaonyesha mistari mitatu mimi ni uleule mmoja, hapa nilikuwa sina uelewa wa vipimo.

Nilikuwa najitaidi kabla ya masaa 72 niwe nimejua kila kitu, baada ya majibu kuwa vile nikamshirikisha nesi fulani kwa kumtumia picha za vipimo vingine ambavyo tulipima naye usiku wa siku ile ya pili, nesi akasema mbona kama naona mstali kwa mbali hebu njoo na mwenzio, nikamjulisha ila alikuwa mbali ivyo nikaenda mwenyewe tu na kunishauri kwa kuwa muda unaisha ni bora nianzishe tu dawa ile ya ndani ya masaa 72, nikachukua na kukinywa bila kula licha ya kushauriwa lazima niwe nimekula.

Nikiwa na stress ya juu na mapigo ya moyo ya juu nikiwa nimekunywa kidonge ,yule dada akaja nanikamuelekeza aende hospitality akapimwe na alivyokwenda na kupimwa akakutwa hana maambukizi.

Siku mbili baadaye tumbo likaanza kuniuma bila kuharisha ila choo nilikuwa napata kwa shida,sometimes nilikuwa nikienda aja kubwa natoa uteute kama kamasi nyeupe na mkojo nilikuwa nakojoa mara kwa mara, nikanywa dawa mbalimbali nikidhani ni amiba,nikaenda kupima magonjwa yote lakini hakuna kilicholeta unafuu.

Baada ya mwezi nikaanza kukosa usingizi nikama napata mawenge,kukooa wakati nimelala, na maumivu ya kichwa baadaye nikaona miguu inavimba hapo nikaona naitaji kwenda hospitality kubwa,nikaenda na kupimwa na kuelezwa figo zangu hazifanyi kazi kwa ufanisi kwa kuwa damu inaonyesha sumu zipo 130 kwa viwango vyao wenyewe wanajua nikashauriwa nifuate mtindo bora wa kura itanisaidia kupunguza uwezekano wa muendelezo wa ugonjwa.

Sasa katika hali hii niliyonayo ninaamini kwamba kama ningelikuwa na kazi nyingine mfano:UALIMU.nisingepata ugonjwa huu kutokana na nature ya kazi hiyo inatoa nafasi kubwa ya muajiliwa kuwa huru na kufanya shughuli zako nyingine.

Lakini pia napenda kuhitimisha kuwa makazini tupendane hata kinafiki kuna wengi wanapata maradhi kutokana na tabia za viongozi au wafanyakazi wenzako mimi ni mfano wa wahanga waliadhiriwa na ukabila,ukanda,chuki na mambo mengine kazini hasa ukiwa mpole na husiye na makuu na husiye na muonekano wa kuwafuraisha wengine.

Asanteni.
aisee pole sana mkuu
 
Pole sana.

Kwanza naona huwezi kabisa kujichanganya na wenzako na ukaiva nao hata kama hawakupendi. Jitahidi hili ulifanyie kazi.

Pili; Unapata mshahara tosheka nao Kisha tengeneza mbinu ianze kufanya biashara, fungua hata duka la maji la jumla na vinywaji utapata hela na Kisha uachane na hayo madili.

Tatu; Kubariana na hari Ulio mayo Kisha songa mbele, kama una vyowaona vipofu na viziwi na walemavu wanavyosonga mbele na maisha nawe usikate tamaa.

Nne; Sio lazima ufanye kazi hiyohiyo, manaa maisha lazima yasonge mbele. Chukua mkopo kwa kutumia hiyo kazi, Kisha fungua biashara, tumia hiyo biashara kurudisha mkopo wa watu. Usipange kutolipa mkopo.
 
Kama akili yako ikipata tatizo inakimbilia uchawi na kuamini umerogwa basi unasafari ndefu sana

Mchawi ni wewe na akili yako, Mjinga daima anasingizia na kulaumu watu kwa makosa yake mwenyewe..Mwerevu anajisusha na kupiga hatua nyuma kutafakari alipokosea

Wabongo au Sisi waafrika wengi tunakwama kwasababu hatuna Self-control ya kusolve matatizo tunayokutana nayo

Mimi nasema HUJAROGWA wala HUCHUKIWI chukua muda soma vitabu acha umalaya kenge wewe Soma Vitabu Lisha huo ubongo madini uandishi wako tu unajiandikia kwa kutia huruma kama wewe ni kidume kaa ukijua DUNIA NI KATILI na HAINA HURUMA KAMWE
 
Kaz yako haina uhamisho?? Kazi za serikali mbona uhamisho ni rahisi
 
Back
Top Bottom