Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Polisi wa Tanzania ni janga la Taifa.Wakazi 8 wa Mererani Wilaya Simanjiro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kukejeli na kushangilia kifo cha Rais John Magufuli.
Rais John Magufuli amefariki Machi 17 kwa matatizo ya moyo na atazikwa Machi 26, Chato, Mkoani Geita. Taifa lipo katika maombolezo ya siku 21, huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
Kuna huzuni na wakati mwingine kuna furaha. Kuna wanaolia na kurarua mavazi kumbe wanashangilia. Kilio kilichojaa furaha. Katika misiba mingi unafiki unaweza ukafikia 75%Kheeee!!
Ni zaid ya makanjanja wale wakosa akili wao wamemiliki Tekno za kutupa pale Manzese washakua waandish..uandishi ni kaz kama kaz nyngne au nasema uongo ndugu zanguuuhSasa Kilimanjaro inafanya nini kwenye title?
Ben saanane Family.Kuna huzuni na wakati mwingine kuna furaha. Kuna wanaolia na kurarua mavazi kumbe wanashangilia... Kilio kilichojaa furaha. Katika misiba mingi unafiki unaweza ukafikia 75%
Sent using Jamii Forums mobile app
Iron lady.Siku Margaret Thatcher alikufa watu walikesha barabarani wakinywa pombe, mpaka tukio la msiba lilikosa coverage.
Ile mitano ya nyongeza angeipata bila kupingwa na hata mingine mitano. Nchi aliiweka mfukoni mwake.Yaani mzee ameondoka, lakini bado nguvu yake imeendelea kutamalaki!! Angemaliza hii miaka mitano mingine, hakika tusingekuwa na tofauti na wale raia wa Korea ya Kaskazini walio chini ya utawala wa yule dogolasi Kim Jong Un! 😇