Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh kukosa kuoa tu hadi afanye hayo?Mahakama ya Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imemhukumu Shamsudini John maarufu SIKUKUU mwenye miaka 35 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwauwa kwa kukusudia kwa kuwanyonga kwa kanga mkewe Asia John aliyekuwa na umri wa miaka 25 na mtoto wake Ahmed Shamsudini aliyekuwa na miaka Tisa (9) baada ya mke wake kumkatalia kuongeza mke wa pili.
Hukumu hiyi namba 13 ya mwaka 2020 imetolewa leo Disemba 07 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara na Jaji Devota Kamzola ambapo ameieleza mahakama kwamba mshtakiwa alitekeleza mauaji yao kwa kukusudia.
Awali Jaji Devota aliieleza mahakama kwamba mshatakiwa huyu Shamsudini John alikuwa na ugomvi na mkewe Asia John baada ya kutaka kuoa mke wa pili ndipo marehemu mkewe alikataa jambo hilo na kupelekea mumewe kufanya mauaji hayo katika Kijiji cha Hidet wilayani Hanang mkoani Manyara.
Jaji Devota aliendelea kwa kusema, mshtakiwa Shamsudini alitekeleza mauaji hayo kando ya Bwawa la Hidet wilayani Hanang umbali wa zaidi ya kilo mita moja kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na kwamba mshtakiwa alianza kumnyonga mkewe Asia kwa kutumia kanga, huku mtoto wao Ahmed Shamsudini akipiga kelele baada ya kuona mama yake ananyongwa na kisha kunyonga na mtoto wao na kumtupa kwenye bwawa hilo, kabla ya kumtoa na kisha kuondoka na mwili wa mkewe hadi nyumba.
Imeelezwa kuwa mshtakiwa alipofika nyumbani alianza kuchimba shimo kwa minajili ya kuuzika mwili wa marehemu Asia, kabla ya mke mdogo kumuona na kumuhoji mshtakiwa ambaye alijibu anachimba shimo la taka na kuuzika jirani na nyumba waliyoishi.
Imeelezwa mahakamani hapo kwamba mshatakiwa alikana kuhusika na vifo hivyo na kueleza kwamba mke wake na mtoto walikufa maji, huku shahidi namba tatu ambaye ni daktari alithibitisha vifo hivyo vilisababishwa na kukosa hewa na siyo kufa kwa maji kama alivyojitetea mshtakiwa lakini baadaye Shamsudini alikiri kutenda matukio hayo na kuwapeleka polisi mahali alipouzika mwili wa mke wake na ulipo mwili wa mtoto kando ya bwawa.
Mshtakiwa amekutwa na hatia kinyume na vifungu vya Kanuni ya 196 na 197 vya kanuni ya adhabu Sura namba 16 Toleo mwaka 2002.
My take: Jamaa anastahili adhabu zaidi ya kunyongwa kwa kitendo hiki cha kikatili kabisa, ingefaa afungwe jiwe zito shingoni kisha atupwe mto Kagera akawe chakula cha mamba.
we jamaa acha kujitoa ufahamu. shamsuduni, aisha, ahmed haya majina ya dini gani? Ni mwislam mwenzako nini huyo jamaa.Majina ya wazazi wao.
Kwa hiyo kuolewa kupo pale pale?😂Vitendo vya ulawiti kwa wafungwa wa condemn ni nadra Sana kutokana na ugumu wa mazingira ya huko wafungwa wanaishi kipweke mno kila mtu analia na mungu wake kutokana na makosa makubwa waliyofanya. Muda wote wafungwa wamejiinamia Tu wanajuta wanafikiria kitanzi . Wataalam wanasema wafungwa waliohukumiwa kifo ( condemned prisoners) hupata torture kubwa ya kiakili sometimes huchanyikiwa hivyo mpaka apate hisia ya kufanya mapenzi si mchezo😂😂
Angalia majina ya baba zao ,HatubishanI!!we jamaa acha kujitoa ufahamu. shamsuduni, aisha, ahmed haya majina ya dini gani? Ni mwislam mwenzako nini huyo jamaa.
Huyo ni mvaa kobazi mwenzako full stop.Angalia majina ya baba zao ,HatubishanI!!
John wazazi wao ni waislamu?Huyo ni mvaa kobazi mwenzako full stop.
Khe.! Hivi wanavyosemaga mnaoa kwa ridhaa ya mke wa kwanza huwa wanapuyanga? Unasemaje amekosea kukataa? Alivyoona mme ameenda kuoa kaepusha shari kaondoka sasa kosa lake nini. ?!Ni kweli uko sahihi.
Lakini pia, mke hakua sahihi kumkatalia kuongeza mke, japokua kama ulivyosema hatua aliyochukua jamaa ni sio sahihi pia hata kidogo. Angempa talaka tuu.
Sana yaani. All in the name of muheshimu mume.Ukatili mkubwa.
Unamuua mama huku mtoto anatazama, haitoshi unamuua na mtoto.
Wanawake tunanyanyaswa
Hapo mtabishana hadi asubuhi. We mkubalie tu kuwa hao ni wakristo kweli. Maana Ahmed, Aisha ni waislam mbon hata habari imeeleza. Hataki kukubali kwamba ndugu yao kapuyanga. Watu na imani zao😂we jamaa acha kujitoa ufahamu. shamsuduni, aisha, ahmed haya majina ya dini gani? Ni mwislam mwenzako nini huyo jamaa.
Acha chuki na ubaguzi wa kijinga. Manyara na bangi wapi na wapi. Km Hujafika sehemu bora ukae kimya. Kuna watu nchi hii akisikia ukanda fulani ni chuki tu. Hii nchi ni moja kwanini uchukie sehemu ya nchi yako? Hata hivyo mauaji haya yanatokea kila kona ya nchi. Nachukia mtu mbaguzi kwa msing wowote ule. Ukimwuliza Manyara ni wapi hata hapajui.Kanda hiyo wengi wavuta bangi matukio ni daily
Manyara ndo vinara kwa mihadarati, bangi, ulevi na matukio ya kikatili kama hayo,, hutaki kufaAcha chuki na ubaguzi wa kijinga. Manyara na bangi wapi na wapi. Km Hujafika sehemu bora ukae kimya. Kuna watu nchi hii akisikia ukanda fulani ni chuki tu. Hii nchi ni moja kwanini uchukie sehemu ya nchi yako? Hata hivyo mauaji haya yanatokea kila kona ya nchi. Nachukia mtu mbaguzi kwa msing wowote ule. Ukimwuliza Manyara ni wapi hata hapajui.
Katangulie kaburini mbaguzi wewe.Manyara ndo vinara kwa mihadarati, bangi, ulevi na matukio ya kikatili kama hayo,, hutaki kufa
Unune usinune ndo iko hivyo,Katangulie kaburini mbaguzi wewe.
Kwenye kufanya makosa, vifuatavyo huwa vinasingiziwa sana;Itakuwa jamaa alikuwa ana magonjwa ya akili sio kawaida
Bora uoe au uolewe na malaya, atacheat ila jion atarudi, watoto watakula, watasoma, watalala.
Ila ukiolewa na mgonjwa wa akili yani mentally unstable atafanya jambo la hatari mda wowote ndio hao wakupiga risasi wake zao
Na ukioa mgonjwa wa akili anaweza wafanya watoto wako kama mawe, unakuta mwanamke anampiga mwanae kama anampiga mnyama au mti kumbe kamzaa mwenyew
Kwenye uchumba tu ukiona tu dalili zozote za uchizi chizi, hasira za kijinga, sheria za kipumbavu, mipaka isiyo namantiki, bora umwepuke mapema.
Sheria ifuate mkondo wake.