buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 180
Katika hali isiyo ya kawaida aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Peter Toima Kiroya anadaiwa kumshushia kipigo mkewe, Philomena Toima mpaka kufikia hatua ya kukimbizwa hospitalini kupatiwa matibabu.
Tayari suala hilo limeshatinga polisi ambapo mwanamke huyo alifika katika kituo cha polisi cha Komolo mnamo Novemba 16 mwaka huu na kufungua jalada la shambulio nambari KML /RB /137/2019.
Chanzo cha ugomvi huo kinadaiwa kuwa Toima kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa takribani miaka mwili sasa na mwanamke anayetambulika kwa jina la Scolla Mollel ambaye kwa sasa anaishi naye kama mke mdogo.
Tukio hilo linadaiwa kutokea nyumbani kwa wanandoa hao Novemba 15 mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni nyumbani Komolo ambapo kulitokea mabishano makali na ndipo Toima alianza kumshushia kipigo mkewe na ndipo alipokimbilia katika kituo kidogo cha polisi cha Komolo kutafuta msaada.
Akihojiwa na waandishi wa habari mwanamke huyo alisema kwamba mme wake amekuwa na desturi ya kumpiga ,kumtishia kwa silaha ,kumdhalilisha sanjari na kumtukana matusi ya nguoni.
Philomena, alitaja chanzo cha matatizo kwenye ndoa yake kilianza mwaka juzi baada ya mme wake kumwajiri Scolla kama mtunza fedha katika taasisi waliyoianzisha yeye na mmewe inayotambulika kwa jina la ECLAT Development Foundation.
Alieleza kuwa mara baada ya kubaini mme wake ana uhusiano na mwanamke huyo alimuuliza kuhusu madai hayo lakini cha ajabu alimwondoa kazini na kwenda kumjengea nyumba ambayo wanaishi mpaka sasa.
"Nilipobaini kwamba mume wangu ana uhusiano na huyo mwanamke nilimfuata na kumweleza lakini cha ajabu alimhamisha akawa anafanya shughuli za ofisi akiwa nyumbani alipomjengea "alisema Philomena
Hata hivyo, Alisisistiza kuwa tangu mumewe aanze uhusiano na mwanamke huyo ndoa yake imekosa amani huku mmewe akitumia rasilimali mbalimbali za taasisi yao kama fedha ambapo Scolla amekuwa akichukua fedha za taasisi kwa idhini ya mme wake.
"Kitu cha ajabu huyu mwanamke amekuwa akitumia fedha za taasisi mwezi wa tisa na kumi kuna mahali ameenda kuchukua milioni tatu kwa idhini ya mme wangu" Alisisistiza Philomena.
Alipotafutwa kwa njia ya simu Toima alikanusha vikali madai hayo na kusema kwamba suala hilo liko mikononi mwa wazee wa ukoo huku akasisitiza kwamba kumekuwa na watu wa pembeni walio karibu na mkewe wanaomrubuni na kumpotosha.
"Hilo suala litakuja kumletea shida kubwa Sana huyu mwanamke kwa kuwa liko kwa wazee alafu kuna ndugu zake wanaompotosha "alisema Toima.
Alipoulizwa kuhusu madai ya kumpiga mara kwa mara mkewe na kutumia rasilimali fedha za taasisi hovyo kwa kumpatia mwanamke huyo alikanusha vikali na kusema kuwa kwa sasa yuko safarini nyanda za juu Kusini na pindi akirejea mkoani Arusha atafunguka kuhusu tukio zima.
Kwa upande wake mwanamke anayedaiwa kuvuruga ndoa ya wawili hao (Scolla) alipohojiwa alisema kwa kifupi kwamba endapo angekuwa anavuruga ndoa hiyo angeshafikishwa mbele ya vyombo vya dola vikiwemo polisi na kisha kukata simu.
Mwisho.
Picha ya kwanza ni Mkuu wa Wilaya mstaafu nchini, Peter Toima inayofuata akiwa na mkewe wa ndoa, Philomena Toima.
Picha nyingine ni mke wa mkuu huyo wa wilaya, Philomena Toima na picha nyingine ni mwanamke anayedaiwa kuvuruga ndoa ya wawili hao, Scolla Mollel.