Manyara: Mwanafunzi auawa kwa kubakwa, atobolewa macho, mwili wake watupwa shambani

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Wakazi wa Kata ya Galapo, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wamegubikwa na huzuni, kufuatia taarifa za kubakwa na kuuawa kikatili kwa Suzana Samweli (13), mwanafunzi wa darasa la sita ambapo wananchi wamelaani vikali na kuitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia ya marehemu, Suzana hakurudi nyumbani kwao jioni ya Aprili 29, 2025, baada ya kutoka shuleni, na mwili wake ulipatikana Mei 1 katika shamba kijijini hapo huku taarifa zikieleza kuwa mtoto huyo alibakwa kabla ya kuuawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP Ahamed Makarani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa, Elias Daniel (26), mkazi wa Kijiji cha Gedamar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: Clouds FM
 
Hii habari imeniuma Sana.
Ningekuwa na uwezo huyu mtuhumiwa wangeniachia Mimi niishi nae nyumbani kwangu,
Sidhani kama kungekuwa na uhalifu tena Tanzania
 
Yeah! Huyo unaishi nae tu ndani angejutia kuzaliwa na kujuta kwanini alifanya hiko kitendo cha kinyama..

Watu kama hao inatakiwa wawe wanaachiwa kwa raia tu ku confess dhambi zao.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP Ahamed Makarani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa, Elias Daniel (26), mkazi wa Kijiji cha Gedamar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Polsi wangekuwa wanajua kusoma finger prints wangewatia mbaroni wahusika
 
Wakazi wa Kata ya Galapo, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wamegubikwa na huzuni, kufuatia taarifa za kubakwa na kuuawa kikatili kwa Suzana Samweli (13), mwanafunzi wa darasa la sita ambapo wananchi wamelaani vikali na kuitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia ya marehemu, Suzana hakurudi nyumbani kwao jioni ya Aprili 29, 2025, baada ya kutoka shuleni, na mwili wake ulipatikana Mei 1 katika shamba kijijini hapo huku taarifa zikieleza kuwa mtoto huyo alibakwa kabla ya kuuawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP Ahamed Makarani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa, Elias Daniel (26), mkazi wa Kijiji cha Gedamar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: Clouds FM
Hii tarifa ni ya awali lakini kama vilivyo vifo vingine vyote hapa Tanzania hii imeisha.

Wabakaji huwa hawaui mtu, wakifnya hivyo basi kulikuwa na jambo jingine nje ya nyege
 
Back
Top Bottom