Wakazi wa Kata ya Galapo, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wamegubikwa na huzuni, kufuatia taarifa za kubakwa na kuuawa kikatili kwa Suzana Samweli (13), mwanafunzi wa darasa la sita ambapo wananchi wamelaani vikali na kuitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia ya marehemu, Suzana hakurudi nyumbani kwao jioni ya Aprili 29, 2025, baada ya kutoka shuleni, na mwili wake ulipatikana Mei 1 katika shamba kijijini hapo huku taarifa zikieleza kuwa mtoto huyo alibakwa kabla ya kuuawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP Ahamed Makarani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa, Elias Daniel (26), mkazi wa Kijiji cha Gedamar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Chanzo: Clouds FM