Manyara: Mwanafunzi auawa, mganga wa kienyeji atajwa chanzo cha mauaji

Manyara: Mwanafunzi auawa, mganga wa kienyeji atajwa chanzo cha mauaji

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Polisi mkoani Manyara bado wanamsaka mganga wa kienyeji anayetuhumiwa kutoa utabiri wa uongo uliosababisha kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne.Mwanafunzi huyo, Yohana Konki (17), alidaiwa kupigwa hadi kufa na wenzake baada ya kuaminiwa kuwa ameiba kompyuta mpakato (tablet).

Yohana, ambaye alikuwa akisoma katika Shule ya Sekondari Qash, wilayani Babati, Manyara, alifariki dunia asubuhi ya tarehe 16 Agosti 2025 baada ya kushambuliwa na wanafunzi wenzake waliomtuhumu kwa wizi huo.

Akizungumza na gazeti la The Citizen Jumatatu, Septemba 1, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani, alithibitisha kuwa mganga huyo alikimbia na familia yake mara baada ya tukio na bado hajapatikana.
Kamanda Makarani alisema kuwa wanafunzi 11 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

“Polisi wa Mkoa wa Manyara bado wapo kwenye msako wa kumsaka mganga wa kienyeji anayedaiwa kuwa chanzo cha mauaji haya kufuatia utabiri wake wa uongo, baada ya kutoweka mara tu baada ya tukio,” alisema Kamanda Makarani.

Ameongeza kuwa jalada la kesi dhidi ya wanafunzi hao 11 tayari limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), ambayo itaamua iwapo watashtakiwa au la.
1756699318712.png
1756699430329.png
 
Hii habari ina kama 2 weeks ndio mnaleta na leo, au hukuwa na Bando😀
 
Jina la shule linaakisi ushirikina tu. Wala sio ajabu kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom