LGE2024 Manyara: RC Sendiga apeleka nyama ya nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ili kushawishi kujiandikisha katika daftari la makazi

LGE2024 Manyara: RC Sendiga apeleka nyama ya nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ili kushawishi kujiandikisha katika daftari la makazi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hii habari kwa upande wng sijaielewa,si mara ya kwanza kusikia habari kama hii kwa ndugu zetu wahadzabe ila huwa najiuliza ulazima na umuhimu wa kufanya hivyo upo wapi na ulizingqtia hii ni jamii ya wawindaji.naomba anayeelewa hii issue vzr atueleweshe tafadhali.
 
I wish watanzania wasusie huu utapeli unaoitwa kuchagua viongozi, bora kila mtu kujiongoza mwenyewe tu kuliko hizi porojo na utapeli wa chaguzi.
Hata wakisusia, daftari tayari lina wapiga zaidi ya 25M na zishaingia kwenye hesabu tayari.
 
Chadema walikutombea mkeo au mama ako? Mbona unawaandama sana tena hata thread haiwahusu.
Sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kutoa matusi makali kiasi hicho mkuu mpaka unavuka msitali unamuingiza mama wa mtu. Tu heshima wazazi wa mtu mwingine kama wewe unavyo waheshimu wazazi wako
 
Whatever, but ukweli wanaujua
Ndio maana mwamko wa kujiandikisha umeshuka sana, imebidi tuweke majina tu kutoka hewani, sasa tuna wapiga kura 32M. Yaani twende au tusiende kupiga kura, utaambiwa waliojitokeza ni 90% ya waliojiandikisha.
 
Wakati yamebaki masaa kabla ya kukoma kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la makazi kufikia ukomo leo Oktoba 20, Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga tarehe 19.10.2024 alitembelea jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha MONGO-WA-MONO wilayani Mbulu ambao maisha yao bado yanategemea uwindaji na kuokota matunda na asali ambapo amewahimiza kujiandikisha katika daftari la makazi ili waweze kuchagua viongozi wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Soma Pia: Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu aamua kutembelea ofisi mbalimbali kuhamasisha Watu wakajiandikishe katika Daftari la Kupiga Kura

Sendiga alifika katika kijiji hicho kilichopo kata ya Yaenda Chini wilayani Mbulu akiwa na zawadi ya kitoweo cha nyama ya nyumbu ili kushawishi jamii hiyo kuwa na utulivu wa muda kujiandikisha katika daftari la makazi kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo Oktoba 20 ili waweze kushiriki katika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia amewata kushiriki kuwachagua viongozi wa jamii yao wenye uwezo wa kuwaongoza kuharakisha juhudi za maendeleo katika eneo lao wakati wa uchaguzi huo.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao baada ya kupokea zawadi hiyo na ujumbe wa kujiandikisha, Salum Joseph Duduqwe na Zuberi Mathayo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwathamini kwa kuwatembelea, ambapo wamemweleza kuwa asilimia kubwa tayari wameshajiandikisha na wameahidi kuendelea kuwashawishi wengine ambao bado wakajiandikishe kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo.

aise mbona kazeeka kuliko sa100
 
Hata wakati wa sensa walipelekewa nyama pori ya kutosha sana. Baada ya hapa watasubiri tena hadi mwakani ndio wakumbukwe. Washamaliza nyani wote kwa uwindaji, miaka si mingi wataanza kula matembele na majani ya maboga.
Wasije tu wakaanza kula binadamu aisee
 
Wasije tu wakaanza kula binadamu aisee
Hawawezi mkuu, ni watanzania wenzetu jamii ya wafugaji. Serikali ingekuwa inawaruhusu kipindi cha uwindaji wanapelekewa nyumbu wa kutosha. Watu wenyewe si wengi (1300 tu)na nyumbu hujaa na kufurika Serengeti.
 
Hata wakati wa sensa walipelekewa nyama pori ya kutosha sana. Baada ya hapa watasubiri tena hadi mwakani ndio wakumbukwe. Washamaliza nyani wote kwa uwindaji, miaka si mingi wataanza kula matembele na majani ya maboga.
Wale vyakula vya kawaida bhana
 
Na sisi wa Iringa hatuendi hadi tuloetewe ulanzi

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hakika JF raha sana kiongozi
Na wahaya tuletewe Lubisi na senene[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom