nyie watoto wa miaka ya 2000s hamjui mambo ya ukabila na athari zake katika nch. mmeshindwa hata kujifunza kwa kuangalia tu hapo jirani Kenya au Rwanda na burundi. hivi hii Elimu ya miaka hii inawaelimisha nini?
Mtu...
Katika nchi za Afrika ya Mashariki ukabila kutoka wakati wa ukoloni ulikuwa ni tatizo Kenya na Uganda.
Kenya tatizo la ukabila liikuwa kati ya Wakikuyu na Wajaluo.
Tanganyika hapakuwa na tatizo la ukabila.
Hapakuwa na makabila ambayo walikuwa wanasigana.
Tatizo la Tanganyika toka ukoloni lilikuwa udini.
Kenya na Uganda hapakuwa na tatizo la udini kwa kuwa Ukristo ndiyo ulikuwa umetamalaki ka dini kuu.
Waislam walikuwa wachache Kenya na Uganda kiasi hawakuwa tishio.
Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi wa kuonekana.
Natumia neno, ''tishio,'' kwa maana ya kuwa walikuwa na uwezo wa kuutikisa ukoloni.
Wajerumani walionja nguvu hii katika Vita Vya Maji Maji.
Waingereza waliishuhudia nguvu hii wakati wa siasa za utaifa baada ya Vita Vya Pili katika harakati za kupigania uhuru.
Ilikuwa tabu kuwatenganisha Waislam na joto lililokuwa linafukuta ndani ya TANU dhidi ya Waingereza.
Udini uliokuwapo Tanganyika wakati wa ukoloni ulikuwa kutoka kwa Waingereza na Wamishionari kutoka mataifa kadhaa ya Ulaya ambayo serikali iliwaachia kutawala elimu na wakaitoa elimu hii kwa kuwabagua Waislam.
Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika baada ya kuondoka Wajerumani baada ya Vita Kuu Vya Kwanza, Wajeruamani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo.
Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya. Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika.
White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa.
Hii ndiyo sababu harakati za kupambana zilipoanza Waislam walikuwa kitu kimoja jicho lao likimlenga adui ambae hawakuwa na shida kumtambua.
Waislam hawakupata hata siku moja kumwangalia Mwafrika Mkristo kama adui.
Hii ndiyo sababu Julius Nyerere aliweza kuchaguliwa kuongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na akawa kipenzi cha Waislam.
Udini na Ukabila haya yalikuja baada ya Tanganyika kuwa huru mwaka wa 1961.
Jambo la kusikitisha ni kuwa haya yalifanywa na Mwafrika mwenyewe baada ya kushika madaraka ambayo kabla ya uhuru yalishikwa na Mwingireza.
Maana ya ''udini,'' ikachukua maana nyingine.
Ikawa neno hili maana yake ni kuwa pale Muislam anapohoji, ''mbona nabaguliwa?''
Huyu ataitwa mdini.
Muislam hatakiwi kuuliza hilo.
Akiuliza ataambiwa analeta ''udini.''
Hapa ndipo tulipo miaka 61 baada ya uhuru.
Ndugu yangu Mtu...
Kabla hujatupia jicho Kenya na Burundi tupia kwanza jicho nchi yako na jifunze historia ya Tanganyika kwa ukweli wake.
Ukienda Kilwa na Songea katika kumbukumbu za Vita Vya Maji Maji majina haya ndiyo utayokutananayo kuwa walinyongwa na Wajerumani kwa kunyanyua silaha dhidi yao:
Waingereza wao walipambana na hao unaowaona hapo chini: