Manyerere Jackton: Kila ukikutana na Mwalimu Nyerere unahisi nguvu fulani ya ajabu

Wademkaji wa kizazi hiki hamuwezi kukaribia hata robo ya personality ya Nyerere, kama viatu vya magu havikutoshi vya Nyerere utafanya nyumba ya kulala kabisa.....
Hata magu,hakuwa mtu wa kawaida,mwaka 1992 kwenye jubilee ya kanisa katoriki mwanza,kipndi cha uongzi wa mhasham Antony mayalla,alikuwepo mwinyi,benny mkapa,dkt william shija,baba wataifa alipoitwa kusema neno,aliinuka na kuota,ally,kuna kijana mmoja hapa anaitwa john,yupo hapa?,huyu kijana yupo nyanza,ally akainuka akamwita mkuu wa mkoa WILLIAM shija,akauliza huyo kijana unamjua?, akasema labda John pombe magufuli,mwl akajibu ndio,jpm akainuka toka nyuma kanisani,alipofika madhabahuni mwl akainua fimbo na kumsonta jpm,akasema kijana hongera sana kwa kujitoa mhanga na kupambana na wahujumu wa nyanza,tazania inahitaji wazalendo kama hawa,kipndi kile mwenyeti wa nyanza malaki lupondije,meneja enock massele,maneja masoko mabula mageta,
 
Somesheni watoto wetu wapate kuwa viongozi, achaneni na hizi propaganda hazisaidii zama hizi ulimwengu umeshafunguka[emoji16]
 
Somesheni watoto wetu wapate kuwa viongozi, achaneni na hizi propaganda hazisaidii zama hizi ulimwengu umeshafunguka[emoji16]
Mganji...
Tatizo si kusomesha watoto.
Kumpeleka mtoto shule kuanza darasa la kwanza si jambo kubwa sana.

Wala isikupitikie kuwa napoteza muda wangu hapa kufanya propaganda.
Hapana.

Nayajua ninayoandika na yana ushahidi.

Rais Mkapa aliomba apewe ushahidi na ushahidi alipewa kupitia kitabu cha Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings...'' (2002).

Aliyoyasoma yalimtisha.
Uamuzi ukawa bora kitabu kipigwe marufuku.

Kitabu kifungiwe.
Kitabu kisisomwe.

Si kwa sababu ni kitabu kiovu bali ukweli ule si wa kusambazwa kwa wananchi wakajua ukweli wa dhulma inayolalamikiwa.

Sasa nakushauri usome kitabu cha Njozi kipo hapa mtandaoni.
Kisome kwanza kabla hujaendelea na mjadala huu.

Nimekuandikia haya kwa kuwa najua hujui.
Hii ni nafasi yako ya kujuwa ukweli.

Inaelekea hujapendezewa na historia ya Waislam walivyopambana na ukoloni.
Lazima itakuchoma.

Sikulaumu ni historia ambayo ilifutwa hadi nilipotafiti na kuandika kitabu.
Ulikuwa huijui na ndiyo maana umekimbilia kusema ni ''propaganda.''

Historia hii si propaganda.

Kuandika vitabu kuelimisha matatizo imesaidia sana katika utatuzi wa matatizo na kuepusha vurugu hasa katika nchi kama hizi zetu.

Umesema kweli ulimwengu umefunguka na watu wanajua ukweli wa kila kitu.

Miaka ya nyuma nisingeweza kukusomesha kama ninavyokusomesha hapa na kukuwekea rejea ya vitabu vilivyopigwa marufuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…