Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 55,705
- 104,843
Na muhimu zaidi ni kuelewa watu wamezaliwa na silika mbalimbali.Tungeumbiwa ulimwengu lainilaini tungekuwa mazoba sana.Aache kujiliza kwa huruma,ni mpambano kwenda mbele.Hayo matatizo yapo kila mahali,cha muhimu fanya kilichokuleta hapo,ukimaliza nenda nyumbani kwako.
Upendo utaukuta kwa familia yako baada ya kupiga kazi kwa bidii na kujihakikishia kupata ujira,by the way upendo haulazimishwi,atakaekuzingatia basi mzingatie,atakayekuona miyayusho naww muone miyayusho tu...makazini now days kuna mambo mengi,ya gizani na hadharani..Dah!Kwa hiyo tusilazimishe,tusilazimishane wala kulazimisha UPENDO?Au siyo?
100% halafu pia usipende kuzoeana sana na workmates sijui kutembeleana tembelea nyumbani... siku zote mtu akishakujua sana ndo chanzo cha kuharibiana..Fika job kwa wakati,fanya majukumu yako inavyopasa,pokea mshahara wako rudi nyumbani kainjoi na familia,huwezi kupendwa na kila mtu sehemu ya kazi...
Ongeza roho mbaya na wivu1.Chawa.
2. Wajivuni.
3. Wafitini/ wakoloni.
Bila shaka wewe utakuwa miongoni mwao!Toa saa tabia au sifa za hao tunaoomba Dua wahamishwe
Bila kutaja hizo sifa hii mada itakuwa haina maana kuijadili ni heri ingebaki rohoni mwako..
POLE KWA STRESS KAZA ROHO
Nashukuru sana Kwa Mungu,Nina mapungufu kama Binadamu,niliwahi fanya kazi mahali ya usalesman kwa kweli niliacha Alama iliyo njema! Nilikuwa nasafiri na maaskari kwa kweli,walikuwa wananifurahia kusafiri nao, maana safari zikiwa mbili wanaombea kusafiri na Mimi.Ishi na watu vizuri, maana tunategemeana.Mada nzuri na mawazo mema,vijana zingatia haya ya Bure ukaishi!Jitahidi sana maisha yako yawe baraka kwa wengine hata ukitoka sehemu watu waone wamepungukiwa , kuna aina ya watu huwa wakitoka sehemu watu waliobakia wanasema afadhali hayupo , hii ipo sana maofisini kuna aina ya watu uwepo wao tu ni kero kwa wengine hadi wafanyakazi wenzake wanaomba dua usiku na mchana huyo mtu ahamishwe ili wapumue. Jitahidi sana kuwa barua iliyo njema ,
Hata wafanyakazi wa chini WAMO!Hii imekaa kwa MaHR wengi, ulevi wa madaraka huwa unawasumbua
Wengine ni wanoko by nature!Wafanyakazi wengi ni wavivu na wezi sasa akitokea mchapa kazi na mpenda haki wanamwona mnoko , akiondoka lazima wapumue na kufurahia.
Nimejaribu tu kutazama jambo hili kwa jicho jingine 🤔Wengine ni wanoko by nature!
Ni Kweli kabisa!Nimejaribu tu kutazama jambo hili kwa jicho jingine 🤔