Hiki kitu unafanya kilifanywa na mama yangu mzazi way back 2004. Lakini kwa hali ya ajira ya sasa sidhani kama inawezekana kuona faida ya elimu kirahisi ushindani ni mkubwa na nafasi ni chache.
Na ni vigumu private sector kuajiri mwanamke mdogo mwenye watoto kuanzia wawili. Mabinti niliograduate nao chuo wakaolewa instantly wote hamna aliyepata ajira. Mtu kamaliza chuo kaolewa, kaenda honeymoon, kalea ndoa, kapata mimba, kajifungua, kalea uzazi. Mwaka na nusu umekata ndio kaanza kutafuta kazi mara siku ya interview mtoto kaamka anaharisha. Sasa wewe una watoto wanne.
Nikisema utafute mtaji ufanye biashara siko sahihi sana, biashara sio suluhisho la walioshindwa maisha. Ni passion na uwezo. Hata mama kabla hajaenda kusoma alianza na genge akashindwa akauza mazao akashindwa. Akaenda zake kusoma ndio akafanikiwa. Ila that time ajira zilikuwepo sio kama sasa.