MAOMBI YA MUDA MREFU: Upumbavu wa imani yetu ya kikristo ambao hata mahusiano ya kibinadamu hayakubaliani nayo!

MAOMBI YA MUDA MREFU: Upumbavu wa imani yetu ya kikristo ambao hata mahusiano ya kibinadamu hayakubaliani nayo!

Hao

Hao wazee ni jinsia gani ? Kwanini 24 na sio 50 au 10 ? Nani aliwahi kuwaona ? Wapo sayari ipi? Ipo nje ya solar system? Wapo kwenye milky way galaxy yetu au adromeda galaxy?? Vp wana mawasiliano na sayari nyingine ay duniani tu nduo tuna taarifa nao?
Ndugu hayo ni mambo ya rohoni na imani otherwise mengine utajua utakapoondoka dunia hii. Ila ukweli Mungu yupo na ndiye aliyeumba vitu vyote and there is no dispute about that. Ni wa kuogofya sana na mwenye hasira sana kwa watendao dhambi.
 
Mbinguni kuna usiku na mchana?? Mafundisho ya wapi hayo tena?? Umenikatisha hata tamaa ya kuendelea kukujibu hoja zako zingine!
Ni kweli mbinguni hakuna usiku wala mchana. Ila tunapokuwa duniani tunawaza hivyo. Lakini ahsante kwa kunisahihisha.
 
Wewe una mzazi wako halafu unaenda kukaa hapo mlangoni usiku kumpigia maombi ya kuomba ada au hela ya kununua daftari au kalam au pesa ya mtaji wa biashara. Usiku kucha unampigia mzazi makelele......baaba....... baaaaba. Au una mpenzi wako kitandani unampigia makele usiku kucha unaomba akununulie gari!!! Ndio hawa wakristo wasiojua maandiko wanachokifanya.

Hakuna Mungu anayesikiliza huo upumbavu. Ukisema umesoma kwenye biblia kwamba Yesu alikuwa akienda kusali usiku kucha unaelewa maana yake ? Wewe una one to one communication na huyo Mungu unapobwabwaja maneno usiku kucha?

Una maongezi na Mungu au unaongea na mtu ambaye nusu saa wala hakujibu???? Huo ni upumbavu. Umesoma hata hilo andiko kwenye lugha mama au umesoma tafsiri ya kiswahili au kiingereza ya mtu aliyetafsiri kwa muono wake?

Mungu huangalia SINCERITY OF THE HEART na siyo wingi wa maneno au muda . God is infinite. Kwake hakuna tofauti kati ya 1 na 100000000000000000. Infinity has no measures!
Umeongea vema mkuu
 
Mkuu itakuwa kuna mahali hauko sawa, Yesu ilifika hatua akawaambia akina Petro mmeshindwa kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? Kwenye kuomba huombei mahitaji yako tu mkuu, kuna kuombea wengine unaombea wagonjwa, wasiojiweza ili Mungu awakumbuke,
 
Bila shaka Mungu ni kiziwi ama ana kiburi kwani kukesha ama kushinda ukiomba kwa makelele inatia shaka.Lakini kwenye African folklore sadaka ya mnyama hutolewa madhabahuni kama kisindikizia maombi na hivyo hakuna kelele wala kukesha.Au ni kwa kuwa mizimu ya kiyahudi haiwajui?
 
Mjinga wewe mtoa mada.

Yaani wewe umekosa akili kiasi Cha kubeza imani badala ya kuwaonya wakristo kwa mtindo wa ibada na maombi!

Hakika kwa ulichochoandika wewe Ni kuni tu motoni
 
Facts, hili swala wanafunzi wa YESU waliliona wakamwabia Bwana tufundishe sisi kusali.....

1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
Luka 11:1

2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
Luka 11:2

3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
Luka 11:3

4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
Luka 11:4
Hiv hayo mafundisho ya yohana mbatizaj yanapatkanaje?
 
Umenena vema kulingana na mtazamo wako mkuu, sincerity haipimwi kwa wingi au uchache wa maneno, ukubwa au udogo wa sauti, muda mrefu au mfupi. Ila jambo lolote, ombi lolote, sala yoyote ikitendeka kwa imani thabiti, kwa unyenyekevu bila ubinafsi Mungu ni mwaminifu sana.

"Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo"
Matendo 10:34

"Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu."
Marko 11:24

YESU mwenyewe akafundisha namna ya kusali, ukisoma kuanzia Luka 11:1-14 utaelewa.
"Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni." Luka 11:2

Lakini pia Mungu alijitambulisha kwa Musa kuwa yeye ni "NIKO AMBAE NIKO" hii ina maana kubwa sana kwahiyo usimlinganishe na mwanadamu.
 
Back
Top Bottom