MAOMBI YA MUDA MREFU: Upumbavu wa imani yetu ya kikristo ambao hata mahusiano ya kibinadamu hayakubaliani nayo!

Ndugu hayo ni mambo ya rohoni na imani otherwise mengine utajua utakapoondoka dunia hii. Ila ukweli Mungu yupo na ndiye aliyeumba vitu vyote and there is no dispute about that. Ni wa kuogofya sana na mwenye hasira sana kwa watendao dhambi.
 
Mbinguni kuna usiku na mchana?? Mafundisho ya wapi hayo tena?? Umenikatisha hata tamaa ya kuendelea kukujibu hoja zako zingine!
Ni kweli mbinguni hakuna usiku wala mchana. Ila tunapokuwa duniani tunawaza hivyo. Lakini ahsante kwa kunisahihisha.
 
Umeongea vema mkuu
 
Mkuu itakuwa kuna mahali hauko sawa, Yesu ilifika hatua akawaambia akina Petro mmeshindwa kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? Kwenye kuomba huombei mahitaji yako tu mkuu, kuna kuombea wengine unaombea wagonjwa, wasiojiweza ili Mungu awakumbuke,
 
Bila shaka Mungu ni kiziwi ama ana kiburi kwani kukesha ama kushinda ukiomba kwa makelele inatia shaka.Lakini kwenye African folklore sadaka ya mnyama hutolewa madhabahuni kama kisindikizia maombi na hivyo hakuna kelele wala kukesha.Au ni kwa kuwa mizimu ya kiyahudi haiwajui?
 
Mjinga wewe mtoa mada.

Yaani wewe umekosa akili kiasi Cha kubeza imani badala ya kuwaonya wakristo kwa mtindo wa ibada na maombi!

Hakika kwa ulichochoandika wewe Ni kuni tu motoni
 
Hiv hayo mafundisho ya yohana mbatizaj yanapatkanaje?
 
Umenena vema kulingana na mtazamo wako mkuu, sincerity haipimwi kwa wingi au uchache wa maneno, ukubwa au udogo wa sauti, muda mrefu au mfupi. Ila jambo lolote, ombi lolote, sala yoyote ikitendeka kwa imani thabiti, kwa unyenyekevu bila ubinafsi Mungu ni mwaminifu sana.

"Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo"
Matendo 10:34

"Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu."
Marko 11:24

YESU mwenyewe akafundisha namna ya kusali, ukisoma kuanzia Luka 11:1-14 utaelewa.
"Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni." Luka 11:2

Lakini pia Mungu alijitambulisha kwa Musa kuwa yeye ni "NIKO AMBAE NIKO" hii ina maana kubwa sana kwahiyo usimlinganishe na mwanadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…