Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maana yake ni nini?Huyo mwanao mwite Kilimbatzz
Iwe Kheri shangazi mtoto akikua nitatupia picha hapa. .Much congratulations mkuuu watoto ni baraka!!
Mungu ni mwema atasaidia arekave mapema na kusiwe na changamoto zozote zitokanazo na oparie!
Allah Awajalie afya njema furaha na maisha marefu wewe mama na wanao IJN!
Hongera ndg. YanguAmen. .
Ningekuwa ulaya kwa haya maneno ningelia kabisa kama wanavyofanya kwenye movie ila kwa kuwa tuko bongo ngoja nisilie wasije kusema vibaya. Maneno mazuri sana Mungu akubariki zaidi. .Big up sana Chifu, hapo unazidi kuwa na mzuka wa kupambania familia yako maana nakala za uzao wako tayari zimeshaonekana ungali hai na mwenye nguvu tele.
Ikimpendeza Mungu namwomba akuwezeshe vyema katika malezi bora ya familia yako.
Aya mekuShukrani sana Meku. .
Una uhakika huu hautaisha watafanya jambo nianze kula maembe😂😂😂😂Nikuunganishe na washikaji wangu makapera😀
[emoji120]Ningekuwa ulaya kwa haya maneno ningelia kabisa kama wanavyofanya kwenye movie ila kwa kuwa tuko bongo ngoja nisilie wasije kusema vibaya. Maneno mazuri sana Mungu akubariki zaidi. .
Hiyo ni mitaa yangu mkuu.napitapita sana. I hope kila kitu kimeenda poa kabisa.How did you know[emoji854]
Niko Istiqama I am surprised you know it. Niko hapa chumba private, niko na mwanangu namngojea mama yake atoke operation room. .
View attachment 2569605
HapanaUkiwa na miaka 36 nasikia unakuwa na mvi kidevini😀
Hebu kaa na usocialize na mkeo acha, anakuhitaji sana wewe kuliko sisi unaotuhadithia. Sisi hatukusaidii chochote.Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF,
Leo asubuhi tarehe 29/03 ni siku ya furaha kwangu kwa sababu kuu mbili. Kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa mke wangu mpendwa, ametimiza miaka 29[emoji846]. Namtakia kheri ya kuzaliwa na ningependa kusheherekea nanyi ndugu zangu.
Pili, Leo hii tuko hospital magomeni hapa. Mda huu amepangiwa c section (kujifungua kwa operation). Huyu akiwa mtoto wetu wa pili. Hivi navyoandika hapa yuko chumba cha upasuaji (Theatre) na mimi niko nje nasubiri.
Ndugu zangu huu ni mwezi wa Kwaresma na pia ni mwezi wa Ramadhani. Tuwe pamoja na kheri njema ya maombi yenu.
Ndugu yenu Gily . .
Updates:
07:41 Nimefurahi sana ndugu zangu nimepata mtoto wa kiume. Niko nae hapa analia kinyama mpaka natamani nilie. Mungu kanipa hitaji la moyo wangu, nilikuwa natamanj sana kuwa na mtoto wa kiume. .
Mke wangu bado yuko chumba cha upasuaji. Nimepewa taarifa she is doing fine ila bado wanamshona na kumsafisha. I can't wait to see her.
Updates:
08:00 mke wangu katoka chumba cha upasuaji. Tuko chumba cha wodi private. Anaendelea vizuri madaktari wanampima pressure iko vizuri kabisa. .