Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
Mh. Rais wetu amesha tueleza tujihadhari na tuwaepuke watu wenye nia mbaya na nia ovo ya nchi yetu.
Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo?
Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?
If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!
You really think this was a good business strategy?
Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:
Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?
wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!
Mwanakijiji
Nadhani unalako binafsi na JK, huu ukosoaji sasa umezidi na unakera.kama umekosa hoja bora utulie na usubiri pumba za CCM uziandikie.
kwa taarifa yako kuna watu muhim wanakufa hata huko ulaya sports inatumika kama njia moja wapo ya kujifariji, michezo si siasa, michezo ni njia moja wapo ya kujifariji.kama wewe unaona JK alikosea sijui ni wawapi wewe...naona tangu uweke picha ya JK yupo hospitali anaazindua machine pale muhimbili umekua hauna hoja.
he was right to go there....Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
Mzee Mwanakijiji, Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa hili, hata kama rais ungekuwa wewe, ungewajibika kuyafanya yote hayo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Hii ya kwenye asubuhi na mapema, ni humane side ya JK. Lazima tukubali JK ni mtu wa watu, anajichanganya sana, tena nadhani urais ni kikwazo kwake otherwise angeendelea kuripoti Msondo pale Amana, kujiwe cha Saigon etc.Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo? !
Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?
If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!
You really think this was a good business strategy?
Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:
Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?
wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!
Mzee Mwanakijiji, Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa hili, hata kama rais ungekuwa wewe, ungewajibika kuyafanya yote hayo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Hii ya kwenye asubuhi na mapema, ni humane side ya JK. Lazima tukubali JK ni mtu wa watu, anajichanganya sana, tena nadhani urais ni kikwazo kwake otherwise angeendelea kuripoti Msondo pale Amana, kujiwe cha Saigon etc.
Hata hivyo, hili la kuwa mtu wa watu, sio excuse ya madhaifu yake judgment, kwenye issues ndogondogo tusizikuze, hakuna ubishi JK ni mtu wa avarage inteligence, hatuna sababu ya kumvua nguo hata kwenye issues zinazohitaji average common sense.
Kwa hili, 'You really think this was a good business strategy?' nakiri sio eneo langu la kujidai lakini lazima tukubali kuwa kwenye bussiness strategies, Tanzania bado tuko nyuma, kazi ya kupromote use ya uwanja wa taifa kwa kombe la dunia, we are late, but better late than never.
'Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?'. Tutayapima mafanikio ya mpango huu pamoja na kujustfy its 7 Billion budget wakati wa kufanya mrejesho baada ya fainali, pia mtapatiwa hesabu za faida ya bilioni 7 mara 70 itakayozalishwa!.
'Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!!' - kwa hili nakuunga mkono, tutengeneze kina Bayi, Nyambui na Shahanga wengi kadri tuwezavyo. Miaka ya 70, tulikuwa ni sisi machampioni, Kenya wameibuka na kutuacha kama ilivyo kwenye lugha ya Kiswahili.
JK anafanya makosa mengi tuu kwa sababu hana watu wa kumwambia ukweli, waliomzunguka wengi ni wapambe, kazi yao ni kutoa nyimbo za sifa na mapambio, ila JK japo kiburi na madharau, pia kisirisiri ni msikivu, ndio maana kuna mahali nilikuambia Mwanakijiji, kama bado hujatafutwa, basi the time is near, utatafutwa simply because your too critique but sometimes constractive.
Niliwahi kusema, unawasidia sana hawa, laiti kama ungekubali kusaidia na upande wa pili kama ulivyoahidi kwenye 'Change' basi safari ndio imeanza!.
Mzee Mwanakijiji, you are Great!, sometimes hivi vitu vidogovidogo viache vipite isijeonekana its a crusade against!. Tupunguze malalamiko, turudi kwenye kupanga strategies, tufanye actions, tusonge mbele!.
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
Msiba wa Kawawa kwa kiasi kikubwa umekuwa tofauti sana na msiba ule wa Mwalimu. Kwenye msiba wa Mwalimu zilitangazwa siku 30 za maombolezo ya kitaifa na kwa kweli katika kipindi hicho uliweza kufeel kweli tupo kwenye Maombolezo. Nakumbuka hata ukitizama redio na televisheni za hapa nchini ulikuwa unapata feeling kwamba tunaomboleza.
Sio nia yangu kuingia kwenye mjadala wa nani ni zaidi kati ya Mwalimu na Kawawa (naamini hili lipo wazi mno). Lakini kwa hakika kwa jinsi msiba ulivyoendeshwa na namna tunavyoomboleza hizi siku saba nasita kuamini kwamba tumemtendea/tunamtendea Kawawa anavyostahili.
Nimejaribu kupitia hii thread lakini bado sijapata kinagaubaga majibu ya maswali haya:
- Rais wa Tanzania anapotangaza siku kadhaa kuwa ni za maombolezo ya kitaifa maana yake ni nini? Au kwa kifupi, Maombolezo ya kitaifa ni nini? Je tuna sheria au taratibu inayoongoza jambo hili?
- Mambo gani Rais anaweza kufanya au hawezi kufanya katika kipindi hicho (kisheria au kimaadili)?