Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo? !
Mzee Mwanakijiji, Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa hili, hata kama rais ungekuwa wewe, ungewajibika kuyafanya yote hayo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Hii ya kwenye asubuhi na mapema, ni humane side ya JK. Lazima tukubali JK ni mtu wa watu, anajichanganya sana, tena nadhani urais ni kikwazo kwake otherwise angeendelea kuripoti Msondo pale Amana, kujiwe cha Saigon etc.
Hata hivyo, hili la kuwa mtu wa watu, sio excuse ya madhaifu yake judgment, kwenye issues ndogondogo tusizikuze, hakuna ubishi JK ni mtu wa avarage inteligence, hatuna sababu ya kumvua nguo hata kwenye issues zinazohitaji average common sense.
Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?
If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!
You really think this was a good business strategy?
Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:
Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?
wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!
Kwa hili, 'You really think this was a good business strategy?' nakiri sio eneo langu la kujidai lakini lazima tukubali kuwa kwenye bussiness strategies, Tanzania bado tuko nyuma, kazi ya kupromote use ya uwanja wa taifa kwa kombe la dunia, we are late, but better late than never.
'Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?'. Tutayapima mafanikio ya mpango huu pamoja na kujustfy its 7 Billion budget wakati wa kufanya mrejesho baada ya fainali, pia mtapatiwa hesabu za faida ya bilioni 7 mara 70 itakayozalishwa!.
'Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!!' - kwa hili nakuunga mkono, tutengeneze kina Bayi, Nyambui na Shahanga wengi kadri tuwezavyo. Miaka ya 70, tulikuwa ni sisi machampioni, Kenya wameibuka na kutuacha kama ilivyo kwenye lugha ya Kiswahili.
JK anafanya makosa mengi tuu kwa sababu hana watu wa kumwambia ukweli, waliomzunguka wengi ni wapambe, kazi yao ni kutoa nyimbo za sifa na mapambio, ila JK japo kiburi na madharau, pia kisirisiri ni msikivu, ndio maana kuna mahali nilikuambia Mwanakijiji, kama bado hujatafutwa, basi the time is near, utatafutwa simply because your too critique but sometimes constractive.
Niliwahi kusema, unawasidia sana hawa, laiti kama ungekubali kusaidia na upande wa pili kama ulivyoahidi kwenye 'Change' basi safari ndio imeanza!.
Mzee Mwanakijiji, you are Great!, sometimes hivi vitu vidogovidogo viache vipite isijeonekana its a crusade against!. Tupunguze malalamiko, turudi kwenye kupanga strategies, tufanye actions, tusonge mbele!.